FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari


Bora tuh kufanya hivyo,maana hamkawii kusema ya kwamba kwa kuwa Rais ni muislam wa Bara na Zanzibar,kwaiyo wanasimama upande wa wahalifu na kufanya uchunguz wa geresha tuh,ni bora kuweka uchunguz shirikishi ili kupunguza mihemko na kunyoosheana vidole kama wanavofanya baadhi ya watu kwa sasa..
 
mgosi TISS ni kitengo cha CCM, haiwezi kufanya lolote, bora hata jumuiya ya waganga wa kienyeji na wapiga ramli wanaweza kufanya uchunguzi.

Halafu,hv unajua haiwatumii waganga ipasavyo kwa maslah ya taifa?ila kwa maslah yao bnafsi rahs and ikitokea tu kesi ya uchawi au chochote kama ile ishu ya Mwakyembe kwenye waraka wake,watasema "serikali yetu haina dini wala haiamini uchawi"
Nonesense
 
Kweli Bora Ukose mali Upate Akili! 1998 watumishi wangapi wamarekani waliodhurika kutokana na milipuko ya Nairobi na Dar? Kwanini Waliodhurika walikuwa ni akina maganga peke yao? Bila kumung'unya maneno ile ilikuwa ni Inside JOB! Walikuwa wanataka kuhamia Bongo after JKN era!
WTC nayo ilikuwa ni Inside JOB, Uthibitisho upo wazi kabisa... Vita against Terrorism ni programu maalumu ya kumiliki rasilima za dunia hii. ni katika mwendelezo wa ku-establish new world order! Hao magaidi wakubwa tunaowasikia ni part ya CIA, NSA et al! wao hawana dini wala kabila WAO wanachokitaka ni kuendelea ku-enjoy Rasilimali za nchi mbalimbali...wamefanya hivyo Libya, Iraq, Kuwait, Misri, Tunisia, Equador, Bolivia, Panama, Vietnam, Korea, Japan nk.

Nchi yetu inamafuta mengi, tuna Gesi Nyingi hao tunaowategemea kwa upelelezi ndo waasisi wa machafuko yote yanayotokea hapa kwetu, Watakachokifanya ni kufunika madudu yote ili taarifa zisivuje! Najua wengi wetu tumetawaliwa na hisia kidini, kikanda na kikabila...si rahisi kuona mambo kwa mapana na marefu ILA Ukweli siku zote utabaki kama Ukweli na Utasimama mpaka Mwisho wa Sayari hii Dunia...
 
Tunalisubiri hili gazeti la mwanchi liombe radhi baada ya huu utumbo
Nakuunga mkono mkuu! Kuna gazeti lingine jana liliandika kuwa wauwaji wa Padri Mushi wamekamatwa huko Nairobi lakini Polisi wamekanusha vikali na kusema kuwa ni uongo na uzushi!! Hata hili siamini japo kweli Raisi alisema watafanya hivyo. Kwamba tayari washazungumza na kukubaliana siamini.
 
Yawezekana FBI wakaja na wasifue dafu(tusipate jibu)- tuna mifano mingi, kwani Scotland yard walipata nini kuhusu moto wa BOT au kifo cha Dr Ouko kule Kenya. Hapa uchunguzi ni wa kufunika siyo kufumbua.

waliota riport ila imekaliwa..kule kwa ouko walitoa riport na tena majina ya wabaya wa ouko yalikutwa yameorodheshwa nyuma ya picha kubwa iliyokuwa imetundikwa ukutani ndan ya nyumba ya ouko...ouko aliwajua wabaya wake
 
Naunga mkono asilimia mia hawa wapelelezi kutoka nje kuja. Na kama ingewezekana wangetusaidia upelelezi wa Utekwaji na Uteswaji wa Ulimboka! Yamkini wangemwokoa yule Mkenya anayeteseka mahabusu na huku hahusiki na suala la Ulimboka. Ngoja waje kwa sababu tangu makanisa yaanze kuchomwa Zanzbar sasa ni zaidi ya makanisa 40 kwa miaka takriban zidi ya mitano na hakuna mtu hata mmoja aliyetiwa mbaroni. Hadi hapo si tayari vyombo vyetu vimeshindwa? Nina wasiwasi na matokeo ya upelelezi wao! Yawekwe hadharani kila mwananchi ajue ni nani na ni nini hasa! Wakati wa utawala wa Raisi Mwinyi lilitokea tatizo la kutatanisha la kuchomwa kwa shule a Shauritanga kule Kilimanjaro. Scotland yard waliitwa kufanya upelelezi lakini wananchi hatukujuzwa matokeo. Lazima wakati mwingine tukubali kuwa wenzetu wameendelea katika taaluma za kujasusi na kiupelelezi kuliko sisi. Acha waje!!
 
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... “Ilatukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza.”

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... “Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu.”

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

“Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia,” alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.


Source: Mwananchi
ingawa majibu yanajulikana watakayotoa FBI, watafute na waliomteka Olimboka
 
Wakati bweni la Shule ya Sekondari Shauritanga lilipoteketea kwa moto mwaka 1994 ambapo wanafunzi zaidi ya 40 waliteketea katika mkasa huo, Serikali iliagiza wachunguzi kutoka nje ya nchi lakini mpaka leo hakuna anayejua kilichofanywa na wachunguzi hao, kilichogunduliwa na hata walichopendekeza. Ripoti hiyo imebaki kuwa siri ya Serikali japo kulikuwa na hisia za mkasa huo kuhusishwa na mambo ya imani za dini

Katika hili naamini pia hakutakuwa na la ziada zaidi ya kutumia fedha za wavuja jasho na kuishia kuambiwa kuwa uchunguzi umekamilika na serikali itafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa.
 
Mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.

Ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu. Hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague. Lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad. Tanzania nakupenda sana

Angeuliwa mdogo wako usingekuja na hoja mfu ulizonazo leo. Acha waje wewe kinachokuuma ni nini??
 
Ukweli ni kwamba JK anaona aibu kumkamata Ilunga anaona aibu kuwaadhibu Uamsho,anaona aibu kumuweka rumande maalimu Seif,anaona aibu kumkamata kamishna Musa Ali Musa anaogopa kumkamata Ismail Jussa anaogopa kumkaripia rais wa zanzibar ndg Shein anashindwa kuongoza nchi kwa sababu uhalifu unafanywa na watu anaowafahamu na dini yake anaamua kuwaita wamarekani kuja kutupelelezea waliomuua padri huku waliompiga risasi padri wakiwa bado hawajulikani...Wafuatao wanajua na kusababisha ugaidi Nchini
1.Balozi wa Irani hapa nchini
2.Ust.Ilunga Hamisi Kapungu
3.maalimu Seif Shariff Hamad
4.Chama cha Cuf
5.Ismail Jussa
6.Stephen Wasira
7.Said Mwema
8.Uamsho Zanzibar
9.Mohamed Abood Mohamed
10.Shehe Bungo
Hapo unataka nini tena maana hawa watu wanajieleza wenyewe kwa matendo yao...
 
Watanzania wenzengu nadhani imefika wakati wa kufanya maamuzi magumu!! nakumbuka mwaka fulani kuna mbunge mmoja alisema ni bora JESHI LA POLISI lifutwe tusiwenalo kabisa, nadhani aliona kuwa chombo hiki hakina faida yoyote kwa taifa zaidi ni kutia hasara kwa kwa tumia kodi zetu. Ni aibu kwa nchi km tanzania iliyokuwa inaogopewa kwa kuwa na ulinzi mzuri mipakani na hata ndani ya nchi, leo inaomba msaada wa kufanya uchunguzi wa mauaji ya padri kutoka vyombo vya usalama vya nchi zingine sikubaliani na hili. Naomba niulize TISS kazi yao hasa nini? au ndy hy ya kuwapeleka watu MABWEPANDE? Huyu mkuu wa kaya ni wakuondolewa kwa maandano km ya Tahriri Saa ya ukombozi ni sasa. kwa upuuzi huu mengi yaja, tusipo chukua hatua watanzania. TUIKOMBOE NCHI YETU KUEPUKA AIBU, NKUDHARAULIWA NA KUTUKANWA.
 
ingawa majibu yanajulikana watakayotoa FBI, watafute na waliomteka Olimboka

problem,action,solution=order out of chaos..ladies and gentlemen,and the show starts all over again,pleasee,welcome AMERICAN COLONIALISM EXPERTS......
 
mitaani wanadanganyana TISS ni ya 3 Afrika
Hivi ni kweli mnaamini TISS hawawajui wauaji?, acheni utani nyie, hadi wewe mwanaJF umepata vipeperushi vya kuhimiza mauaji halafu uniambie kuwa kachero aliyeajiriwa kwa kazi ya kupeleleza asijue, wanajua inawezekana wanawaogopa ndio maana ya kusakizia FBI ili kujitoa kwenye lawama kuwa mmetugeuka. fumbueni macho wakuu.
 
Kama uchunguzi wa vyombo vya ndani vinaweza kuwakamata wakina Joshua Mulundi, bora tu hao FBI wawasaidie. Pili suala hili lina hisia za kidini, viongozi wa vyombo hivi wa zanzibar ni wa dini inayohisiwa na wale wa serikali ya JMT ni wa dini hiyo hiyo, ili kuweka imani kuwa haki imetendeka ni vyema ucgunguzi huu ikiwahusisha watu wa nje.
 
Mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.

Ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu. Hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague. Lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad. Tanzania nakupenda sana

Mkulu

We have a limited capability kwenye mambo mengi hasa yale ya usalama ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea.

Tatizo ni kwamba tumekulia kwenye propaganda...ohh. tanzania ni nchi ya pili dunia kwa upelelezi baada ya Israel...LOL...chezea propaganda

 
Back
Top Bottom