Fatuma Karume: Zanzibar tunaishi kama wanyama!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Mwanadada jasiri na aliyejizolea umaarufu hivi karibuni Fatuma Karume AMELIPUKA, unaweza kusema. Akihojiwa na DW amesema sasa Zanzibar wanaishi kama wanyama maana hawafuati katiba. "Kama wameamu kuondoa utaratibu tuliyojiwekea sasa tuna tofauti gani na wanyama?"

Alipoulizwa kama vitisho vya CCM havimtishi na kama baba yake hamdhibiti, amesema. "Mimi siyo mbwa wala paka, nina haki yangu ya asili ya kujieleza na kutoa maoni" Amesema baba yake hawezi kuondoa uhuru wake kisa CCM.
"Wanataka baba anidhibiti? (kicheko) "nina miaka 46, tena baba ananihimiza kufanya nachoamini ni haki"

Alipoulizwa maoni yake kuhusu MCC amesema anasikia watu wanasema waZanzibar wako tayari kufa njaa lakini serikali iachwe huru. "Hivi tunahitaji serikali huru au watu huru? hapa tuna wakoloni wengine" Ameuliza "yaani watu wa Zanzibar wafe njaa kisa Shein awe rais?" haiwezekani!
 
Dada nchi hizi za Africa hatuna viongozi bali watawala. Watafanya chochote mradi wabaki kuwa watawala.

Kama hii ya Zanzibar imetuondolea sifa Africa na duniani na kutufanya tufanane na nchi zingine Africa zinazokandamiza democrasi kwa kisingizio chochote
 
Huyu naye ni mnafiki tu kama walivyo Wazanzibari.

Isingekuwa ubabe wa Baba yake, president Amani Karume ambaye aling’ang’ania madaraka hata Rais Ali Mohamed Shein alisingepatikana wala asingekuwa Rais wa Zanzibar.

Rais Ali Mohamed Shein ni by-product ya utawala wa Rais Amani Karume.
 
MsemajiUkweli
Shein kuwa pale ni mpango wa Kikwete kutaka Meghji awe makamu wake hivyo alibidi amtafutie wadhifa Shein
Mpango wake huo ulishindwa kama alivyoshindwa kumrithisha Membe
What a loser!
 
Kuna uzi mmoja humu ndani nimeuliza ''Hivi zenzi kuna Rais?''. Naungana na Fatuna kuwa Zanzibar hawana tofauti na kuku ambaye akiamuka asubuhi anawaza kupaluapalua bila kufuata utaratibu wowote.

Hivi Makamu wa kwanza wa Rais ni nani vile?
 
Huyu naye ni mnafiki tu kama walivyo Wazanzibari.

Isingekuwa ubabe wa Baba yake president Amani Karume ambaye aling’ang’ania madaraka hata Rais Ali Mohamed Shein alisingepatikana.

Rais Ali Mohamed Shein ni by-product ya utawala wa Rais Amani Karume.
Bado hiyo haina uhusiano na Fatma Karume Junior.
 
Kila Mtu anajua kuwa Dr. Bilal alikuwa chaguo la wa znz lakini akaporwa haki hiyo akapewa Babake na aliufyata. Znz inawezekana bila ya Familia yao asijikweze sana yeye ni mtu mdogo sana visiwani.
 
Kuna uzi mmoja humu ndani nimeuliza ''Hivi zenzi kuna Rais?''. Naungana na Fatuna kuwa Zanzibar hawana tofauti na kuku ambaye akiamuka asubuhi anawaza kupaluapalua bila kufuata utaratibu wowote.

Hivi Makamu wa kwanza wa Rais ni nani vile?
Unaulizia Makamu yupi wa Rais?
Bara, Makamu wa Rais ni mama Samia, na Zanzibar ni Balozi Idi.

Ila pia angalia katiba zinasemaje kuhusu upatikanaji wa Makamu wa Rais.
 
Bado hiyo haina uhusiano na Fatma Karume Junior.
Hiyo elimu aliyoipata ambayo inamfanya kubwabwaja unadhani angeipata kama siyo kuishi ndani ya Ikulu ya Zanzibar kwa kutumia mabavu ya baba yake. You must be joking!
 
Mhh sijui huyu dada anajiamini mini,any way dunia hii ina watu wachache sana wa namna hii.
And huwa namshangaa matamko yake anayatolea bara na si Unguja!, anawachonganisha wenzake huko Zanzibar ila yeye anakula maisha mazuri Tanzania Bara.
 
Haizuii kusema ukweli kuhusu hali ya kisiasa ilivyo Zanzibar, jadili hoja yake siyo kumjadili yeye inaonyesha kuwa inawezekana wewe ndiyo mwenye muwasho unaosababisha akili yako isifanye kazi sawa sawa,
Kila Mtu anajua kuwa Dr. Bilal alikuwa chaguo la wa znz lakini akaporwa haki hiyo akapewa Babake na aliufyata. Znz inawezekana bila ya Familia yao asijikweze sana yeye ni mtu mdogo sana visiwani.
 
Haya masuala angeyasema wakati babake anapewa urais Zanzibar na ccm kwa nguvu tungemuelewa.ila kwa sasa atulize kisharuala.
 
Back
Top Bottom