Fatma Karume Yamkuta Twitter, Ni Baada Ya Kusema Hajasomeshwa Na Serikali Ya CCM

Kwenye siasa hakuko hivyo wewe kama ni mtoto wa mwanasiasa ,baba akibugi sio kwamba ni familia nzima kuna watoto wangapi wa madikteta wamekuja kuwa watu wazuri baada ya wazazi wao kufariki??na kwa kesi ya zanzibar hadi hiyo hali kuiona hivyo kiasi fualani imechangiwa sana na baba yake kwani uhasama ulikuwa umefikia pabaya sana kipindi cha komandoo na hadi karume alipomuita maalim seif na kuweka mambo sawa hadi ccm wenzake wakamuona kuwa ni msaliti na kuanza kumuita majina ya ajabu ajabu tu!!alipotoka ndio balaa hilo la uchaguzi wa 2015,likatoea!!SHANGAZI toka baba yake yupo madarakani palipokuwa na la kusema alisema japo sio kwa kiwango hiki .
Kwa mara ya kwanza Tanzania ilizalisha wakimbizi huko Zenj kwa uongozi wa babake Shangazi,amewahi kuhoji wale watu waliouawa wakati wa utawala wa babaye??
 
Huyo binti anayejidai kuyaongelea sana MAPUNGUFU ya kisiasa hasa kwa wakati huu je ni kipi hasa anachopingana nacho na hakikufanywa na baba yake?!

Kama ni unyama wa kisiasa baba yake alimfanyia sana Yule bwana.Leo yaleyale eti anajifanya kuyapinga!

Je kipindi baba yake akiwafanyia wenzake hayo huyo binti hakuyaona?!
Kwa hiyo kama baba yake alifanya unyama hiyo ndiyo justification ya utawala huu kufanya unyama na yeye haruhusiwi kukemea????

Hizo shule mlienda kusomea nini labda kwa mfano?????????????
 
Trust me ulisoma na pesa za serikali ya CCM. Kama unajishebedua hapa umesoma na pesa ya wazazi wako na wazazi wako waliiba pesa ya umma. Umesomeshwa na CCM. Matusi yakuingie vizuri sasa!
Pathetic!
Utakuwa mpuuzi tu wewe hiyo pesa ya umma waliibia wapi? Kwetu hakuna aliyewahi kuwa mtumishi wa serikali kwa taarifa yako.
 
Afrika kuwapata wanawake aina ya Fatma Karume ni nadra sana.
Walikuwepo akina Bibi titi ambao walishiriki bega kwa bega kuipinga serikali dhalimu ya Kikoloni wakati huo.
Kwa Kizazi cha sasa cha wanawake kupenda vya dezo na vizuri tu nyuma ya migongo ya teuzi na viti maalum ni nadra sana kupata Sururu Jembe kama Fatma Karume.

Watanzania tujivunie huyu Dada.Afrika Nzima hakuna kama huyu.

Afrika tunakua maskini sana kwa sababu tuna roho mbaya ya ubinafsi na kujijali kuliko kuwajali wengine.
Hakuna MTU aliyeshiba anayeweza kulala kumsemea mwenye njaa.
Wanasayansi na wengi waliotokea ulimwenguni walizijali jamii zao na hata kufa kwa ajili ya kuziletea mabadiliko. Ndio maana Hakuna nabii aliyetokea Afrika mana waliokuwepo walikua wabinafsi.
Walitumia miujiza kuwaangamiza wengine na kujikweza tu.

Ni nadra sana kumpata mtoto wa Rais ambaye hajipendekezi kwa watawala tena kwenye mfumo mgumu sana kusurvive kiuchumi ,kisiasa na kijamii ukipingana na watawala.

Fatma ni hazina kwa taifa hili kwa ustawi wa haki,demokrasia na utawala bora.

Kuna wengi Leo wanajiita wapambanaji na kujinanga kuwa wao ndio wanye kukomesha maovu kwenye taifa hili yaliyokuwepo kwa muda mrefu lakini ukweli ulioko wazi ni kwamba watu hao hao walishiriki kupiga makofi na kuinamisha vichwa wakati wote nchi ilipokuwa inadhulumiwa na hawakuthubutu kujitoa kusema ukweli wa kile wanachokiamini ili kusimamia haki. Kwao maslahi yao kwanza na baada ya kushiba wataangalia namna ya kuendelea kutawala kwa kutangaza kuwa wao ni wapya wanaopaswa kuheshimiwa na kutukuzwa huku wakiziba midomo ya wengine isiseme kile wanachona hakipo sawa.

Hatuwezi kuendelea kwa kuendelea kuwakosoa waliopita tu bila kutoa fursa na sisi kukosolewa.
Wanaopaswa kukosolewa ni waliopo ili warekebishe.

Fatma Karume hajasema kuwa hajasomeshwa na baba yake ambaye ni mtumishi wa serikali ya CCM Bali amekanusha kuwa amesomeshwa na CCM.
CCM ni chama kama vyama vingine vya siasa ndio maana serikali haichukui kodi kwa wanaCCM peke yao.
Tena kwa haraka haraka wanaCCM wengi ndio ambao hawalipi kodi ukianzia na wenye madaraka kwenye serikali ambao wote ni wanaCCM. Kwa hiyo kama ni kodi basi wale ambao sio wanachama wa CCM ndio wanatoa kodi zaidi na kwa wingi kuliko Wale wa CCM.

Logically pato kubwa la nchi linatoka kwa wale wasio wanaCCM. Kwa hiyo ni vyema tukaweka Katiba mpya ili kila mtu achangie Kodi kwenye pato la serikali na sio kujisifu tu kuwa Sisi ndio tumekusomesha wakati hata kodi hukatwi kwenye mshahara.
Kila mtu akatwe kodi kwa kila senti anayoipokea.

Mwisho CCM ikubali pia kuambiwa kuwa imeshindwa kwa miaka 5O kuwasomesha watanzania wengi kwa kiwango cha Fatma Karume kama ukweli wao ndio waliomsomesha na sio wazazi wake. Je, ni wanachama wote wa CCM waliosoma kama Fatma.? Kwa nini CCM haikuwasomesha ? Au chama hicho kina ubaguzi wa wanachama wake?

Acheni kumtukana Malkia wetu Fatma Karume.
Tumkosoe kwa Sera na sio mambo binafsi.

Hakuna namna mjukuu naye atakuja kuukwaa urais Siku moja.
Ule ukoo unaonekana umechaguliwa na Mungu kuwaongoza watu.

Ninachompendea yule Dada hatukani MTU na kusababisha jinai.
Hamtukani Rais wetu wala waziri Mkuu wala makamu wa Rais wala Rais wa Zanzibar bali anakosoa akisimaia sheria . Huu ndio ustarabu wa kukosoana na sio kutukanana kama wengine wanavyofanya.
..Kuna wengine wanatumia Fursa za vyeo na vyama vyao kuwatukana na kuwakejeli wengine.
 
Last edited:
Huyu mama anajishushia heshima taratibu, aachane na siasa adeal na mambo yake ya sheria
 
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume amejikuta katika wakati mgumu pale alipoaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hajasomeshwa na Serikali ya CCM bali pesa za Biashara za baba yake na Mfuko ya AGHAKHAN na Mkopo wa Bank ya London,

maneno hayo yamewapandisha hasira wachangiaji huku wakihoji Biashara gani Baba yake alifinya wakati historia inaonesha baba yake maisha yake mengi ameyatumia kwenye siasa. aidha wamehoji ni Watanzania wangapi wemeweza kusoma kwa Mifuko ya Taasisi kubwa kama Aghakhan na Mikopo ya Mabenki makubwa kama London Bank kama siyo watoto wa Vigogo.
Mashambulizi hayo yamemfanya Mwanaharakati huyo mara kadhaa kuwa-block wale wote walioandika maneno yenye ukweli ndani yake na yanayomchoma.

View attachment 819312
View attachment 819313
View attachment 819314
View attachment 819315

View attachment 819317
View attachment 819318
View attachment 819319
View attachment 819320
View attachment 819321
View attachment 819322
CCM mmeshikwa pabaya na Binti Fatma Karume mmebaki mnakenua kumuwinda kama fisi.
 
Aisee!Maana kama ni unyama wa kisiasa baba yake alishawahi kuufanya wa kutisha kwa wapinzani wa eneo lile!

Ajabu leo eti anathubutu kuyakemea yaleyale yaliyo pata kufanywa na mzazi wake.
Acha upunguani wewe kwa hiyo unajustify kwamba kwa vile baba yake alifanya unyama na huyu mpuuzi afanye ?karne hii tumchekee tu ?
 
Utakuwa mpuuzi tu wewe hiyo pesa ya umma waliibia wapi? Kwetu hakuna aliyewahi kuwa mtumishi wa serikali kwa taarifa yako.
Mpuuzi ni wewe ambaye una fikra mgando ukiamini kuiba pesa ya umma ni lazima uwe mtumishi wa serikali. Lugumi alikuwa mtumishi wa Idara gani?
Pathetic!
 
Hoja kubwa na ya msingi hapa ni kuwa Fatma alishawahi kumuuliza "mshua" kuhusu wizi wa kura za Maalim Seif? Alikemea na kuhoji hilo hata kimoyo moyo?
Hizo Tweets amejibu kama muuza vitumbua kwa mtogole na sio Rais wa TLS. Kukaa kimya ni busara pia.
Shame!
je maalim aliwahi kuzikataa zile pesa alizo kuwa ana pewaaa... aliwahi kutamka waziwazi kuwa ameongwa na kukataa... watoto wa familia moja hao wanacheza segere au mdundo mmoja
 
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume amejikuta katika wakati mgumu pale alipoaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hajasomeshwa na Serikali ya CCM bali pesa za Biashara za baba yake na Mfuko ya AGHAKHAN na Mkopo wa Bank ya London,

maneno hayo yamewapandisha hasira wachangiaji huku wakihoji Biashara gani Baba yake alifinya wakati historia inaonesha baba yake maisha yake mengi ameyatumia kwenye siasa. aidha wamehoji ni Watanzania wangapi wemeweza kusoma kwa Mifuko ya Taasisi kubwa kama Aghakhan na Mikopo ya Mabenki makubwa kama London Bank kama siyo watoto wa Vigogo.
Mashambulizi hayo yamemfanya Mwanaharakati huyo mara kadhaa kuwa-block wale wote walioandika maneno yenye ukweli ndani yake na yanayomchoma.
Amesema ukweli hajasomeshwa na pesa za ccm kasomeshwa na pesa za babaake. Kama babaake alikopa alikuwa ni mfanyabishara hiyo ilikua mbinu ya baba ya kuendesha maisha yake na familia yake. CCM haimsomeshi mtu. Baadhi ya wanaccm uelewa bado Ni tabu
 
je maalim aliwahi kuzikataa zile pesa alizo kuwa ana pewaaa... aliwahi kutamka waziwazi kuwa ameongwa na kukataa... watoto wa familia moja hao wanacheza segere au mdundo mmoja
Hayo ungemuuliza Fatuma atoe majibu....
 
Lumumba njooni na hoja pevu za kuondoa ujinga, maradhi na umasikini. Walioiba kura za Maalimu ni CCM na taasisi zake shirika. Hakika mtatawala kitambo kwa mbinu hizo chafu lakini si milele. Umilele unaye mwenyewe ambaye ni Jalali, acheni kukufuru.
 
Back
Top Bottom