Fatma Karume Yamkuta Twitter, Ni Baada Ya Kusema Hajasomeshwa Na Serikali Ya CCM

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume amejikuta katika wakati mgumu pale alipoaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa hajasomeshwa na Serikali ya CCM bali pesa za Biashara za baba yake na Mfuko ya AGHAKHAN na Mkopo wa Bank ya London,

maneno hayo yamewapandisha hasira wachangiaji huku wakihoji Biashara gani Baba yake alifinya wakati historia inaonesha baba yake maisha yake mengi ameyatumia kwenye siasa. aidha wamehoji ni Watanzania wangapi wemeweza kusoma kwa Mifuko ya Taasisi kubwa kama Aghakhan na Mikopo ya Mabenki makubwa kama London Bank kama siyo watoto wa Vigogo.
Mashambulizi hayo yamemfanya Mwanaharakati huyo mara kadhaa kuwa-block wale wote walioandika maneno yenye ukweli ndani yake na yanayomchoma.
 
Last edited by a moderator:
yani vitu vingine bana!
SASA MLITEGEMEA MTU BABU YAKE KAWAHI KUWA RAIS!
BABAKE RAIS!
yeye asipate fursa ya kusoma!
HATA NYIE MNGEKUWA NDO KARUME BABU NA KARUME BABA!
manake msingesomesha wanenu?
naye anajieleza sana ,KWANI NINI MBAYA KUSOMESHWA NA BABAKO?
ADA UNAULIZA ALIKOITOA?
si wajibu wake kama mzazi?
si alikuwa analipwa mshahara kutokana na kazi aliyonayo ambayo ni urais!?


aaaand last time I checked.
MSHAHARA UNALIPWA KUTOKA KWENYE MFUKO WA SERIKALI AMBAYO INA PATO KUTOKANA NA RASILIMALI NA KODI ZA WANANCHI!
AU?
 
Sioni tatizo kwa Fatma kuwa mwanaharakati kwani kwa mujibu wa Katiba yetu ni haki yake lakini pia nakuwa na mashaka kwanini anaogopa kukiri kuwa alisomeshwa na serikali ya CCM, hata mtoto mdogo anajua huyu kakulia Ikulu, amesomeshwa na Serikali, asijifanye kauzu kwa kila jambo,na hata jeuri alionayo ni kwa sababu ametokea ikulu
 
Ni upuuzi kusema kasomeshwa na serikali ya CCM kwani babake hakuwa na mshahara?let alone huo mkopo na ufadhili aloupata.
kwani wewe unaelewa nini unaposema. umesomeshwa na serikali ya CCM? hata Chadema. Siku wakichukua nchi kuna watu watasima. Kipindi hicho, watakuwa wamesomeshwa na serikali ya Chadema na watakuwa wenda wazimu watakapojishebedua kuwa hawajasomeshwa na serikali
 
Hivi huyu Fatma Karume si ni rais wa TLS? Sasa iweje anajichanganya kuwa hajasomeshwa na serikali ya CCM, hivi ni chama kinachosomesha mtu au serikali?
 
kwani wewe unaelewa nini unaposema. umesomeshwa na serikali ya CCM? hata Chadema. Siku wakichukua nchi kuna watu watasima. Kipindi hicho, watakuwa wamesomeshwa na serikali ya Chadema na watakuwa wenda wazimu watakapojishebedua kuwa hawajasomeshwa na serikali
Kusema nimesoma kwa Fedha ya serikali ya CCM binafsi ni kama unanitusi. Nimesoma kwa pesa ya wazazi wangu.sijawahi kukopeshwa na ccm wala serikali ili nipate elimu.
 
Mtapata tabu sana watu wa Lumumba!
Hawa viumbe ni wa ajabu sana!!yaani ukionekana tu una mawazo tofauti na wao na unaonekana unawaamusha watu tayari limekuwa kosa?!!!wataanza kutaka kukutoa kwenye reli!!ila kwa huyo SHANGAZI wetu wataula wa chuya!!yaani sijui hawa ni viumbe wa namna gani ina maana na wao wanatuambia kuwa kwa sasa ni wanufaikaji na mfumo huu ndio maana hawapigi kelele???ndio maana wanakuwa wakali wakimuona mtu anakosoa??kwa vile muda wa kufaidi matunda ya nchi umekwisha??
 
Akili mali sana..Ukose vyote lakini pata akili.Nachowaza tu kwa mbaaaaaaaali.............V.A.T ..makato ya wafanyakazi...Makato ya wafanya biashara na biashara zao.Vyote ni serikali ya CHAMA si Serikali ya Wananchi..Reli(SGR),DreamLiner..Bomba d..yoote si ya waananchi ni ya CCM.Naanza kuelewa kwa nini tuliitwa SHITHOLE countries.Vizuri vyoote tumeletewa na CCm na Mabay yoote na mapungufu mengi tumeletewa na Wachochezi na wasio penda nchi si CCM.
 
Back
Top Bottom