Fatma Karume: Sheria inayokataza mapenzi ya jinsia moja imepitwa na wakati

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Mwanasheria Msomi Fatma Karume amepinga kitendo cha kuwaandama na kuwasaka watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja akisema kitendo hicho ni kuwanyima haki ya kuishi kwa amani.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Fatma Karume amesema sheria inayokataza ushiriki wa mapenzi ya jinsia moja ( Sodomy) imepitwa ni sheria kandamizi. Wakili msomi huyo amesema kitu ambacho watu wazima wanaamua kufanya kwa hiyari yao faragha ni haki yao hawatakiwi kutokea viongozi wa kuingilia.

Wakati hayo yakiendelea Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewataka watu wanaotumia akaunti ya Fatma Karume waache mara moja wakati Fatma Karume mwenyewe alishakiri kupitia WhatsApp kuwa hiyo akaunti ya twitter ni akaunti yake halisi.
Screenshot_2018-11-01-18-35-44.jpg
Screenshot_2018-11-01-18-36-31.jpg
Screenshot_2018-11-01-18-37-27.jpg
 
Madam namkubali ila hapa kafeli na wewe pia umefeli kwanini usifiche hiyo namba yake
Hapana hajafeli, sababu hata kwa upande wa imani naisemea biblia imesema "tuyachukie matendo yao sio wao" , uwe makini kunielewa inamaana unapoyachukia na kuyapinga matendo yao, hivyo automatically watajua kua matendo yao hayakubaliki katika jamii basi wataacha njia zao ovu au watajitenga na kuwa wapweke.
 
Ushoga, usagaji na upuuzi wote wa namna hiyo siyo vitu vya kuvivumilia wala kuvichekea nchini mwetu ni uovu wa kiwango cha juu ndiyo maana Sodoma na Gomora ilichomwa moto.

Siyo kila kitu ni cha kupinga tu mambo mengine mema kama hili la kuwafutilia hawa wanaojihusisha na huu uchafu tena wengine wanajitangaza hadharani hatua ya kula nao sahani moja ili wafikishwe mbele ya sheria ni jema ili kuukomesha huu uchafu japo kwa muda maana ni hakika huko mbeleni tutataitiwa tu turuhusu kwa sababu ya umaskini wetu ila kwa sasa acha tupambane nao

LAW. :18:22
Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
 
Naamini kila kitu kina mipaka yake.
Na kwa Binadamu privacy na maswala mengine kama ya kidini na imani hayapaswi kuingiliwa maadamu hayana madhara kwa wengine.

Namuunga huyu Dada mkono kwasababu hili jambo amelizungumzia kimuktadha wa sheria na haki za binadamu.
 
namuunga mkono by the way tutakataa sasa hivi ila mabepari wakianza tushika koo tutakubali tu tena kilaini ....mbona sheria hizo zinakataaa lakini watu wanafanya tu kwangu sipendi ndo maana sifanyi ila wanaopenda na kufanya mbona tunaishi nao mitaaani na wako wengi sana naina julikana kabisa ndoo maana ukienda jeshini lazima wakucheki.....
 
Nilisoma article moja hivi.

Kuna mtu (Ujerumani) aliweka tangazo mtandaoni anatafuta mtu ili amle nyama. Basi lile tangazo kuna mtu akalijibu, wakapanga siku ya kukutana ili kufanya walichokubaliana.

Alipofika jamaa baada ya mvinyo muda wa kufanya walichokubaliana ukaanza. Ukakatwa uume, ukapikwa wakala kwa pamoja. The whole time mtu anableed. Akaanza kukata na viungo vingine.

Mwisho akafa. Na jamaa akakamatwa na akashtakiwa akafungwa.

Kwa hoja ya Fatma kwamba eti watu kisa mmekubaliana mnafanya vitu sirini eti tuwaache hapo siyo kweli. Kwahiyo huyu jamaa angekua yeye ni hakimu angemuacha kisa alimla nyama mwenzie sirini?

Na lazima tujue haki za binadamu huwa compromised na sheria au na haki za mwingine. Wewe una haki ya hayo mapenzi ya jinsia moja lakini na mimi nina haki ya kuishi comfortably kwa maamuzi na tamaduni zangu.

Ndiyo tunasema 'Una haki ya kusikiliza muziki kwa sauti ya juu kabisa ila jirani yako asisikie kelele"

Hivyo vitu mnavyofanya sirini vibaki huko huko vikitufikia sisi wengine sheria ihusike.
 
Yupo Sahihi

Dini inakataza mapenzi ya jinsia moja, ila Tanzania haiongozwi kwa sheria za dini, ni secular country

Kama hao watu wanafanya wenyewe huko sirini kwao huko, kuwafuatilia kisha uwafunge itakua hai make sense kisheria

Sasa mtu akiwa accused anafanya mapenzi kwa njia hiyo (kama alivyotaja Dudubaya) mtaenda kumpima ili mumfunge?

Itakua kitu cha kudhalilishana sana.....as long as wanafanya kwa hiyari yao bana, hayo ni ya kwao, sisi tuadhibu wanaobaka, wanaotembea na wanafunzi, ama kulawiti watoto

Wanaotakiwa tuwadhibiti ni hao wa instagram, maana mambo mengine ni taboo hata kwa mtu usiye na dini

Japo hili kuwaingia Watanzania wengi ni ngumu sana, sababu dini imechukua nafasi kubwa sana katika maisha ya wa Tz
 
Hii nchi tokea baba wa taifa amesema haina dini na kauli hii kuendekezwa na viongozi wajao ni shida tupu, maana kuna wakati watu wanataka kutumia dini kutatua mambo ya msingi hasa viongozi wa juu lakini pa kushika hamna sasa ni mparaganyiko tu.

Kweli wengi tunachukia hiyo homosexual lakini tutumie nini kama taifa kukemea? hiyo katiba ndio imepitwa na wakati sasa ni maneno mdomoni tu. Uislamu umekataza lakini hakuna kiongozi wa nchi hata mmoja anayesubutu kusimama kwenye jukwaa akaongelea uislamu namna unavyokataza hiyo kamuluttwi.
 
Back
Top Bottom