Fatma Karume, kubali umeteleza

Fatma Karume, kubali umeteleza

-Kwanza hoja ya wanaounga mkono hili suala la kuanza kukimbizana na mashoga ni "dini" hamna reference nyingine kubwa.

Sasa swali je mbona dini imekataza kuzini? mbona dini imekataza mauaji? mbona dini imekataza wizi mbona dini inashawishi kusaidiana lakini huwa hamtumii hii nguvu kuyapinga haya?

Nadhani kama nchi tunakosa muelekeo. Hatuna dira ndiyo maana miaka rudi akija huyu rais analeta vyake...haanzii alipoishia mwenzake.

-Kwenye nchi iliyojaa maskini wa kutupwa na isiyo na huduma za kueleweka ushoga ni jambo ndogo lisingepaswa kuwa mjadala wa kitaifa. Ushoga hauathiri usafiri wa masaa mawili kutoka mbezi kwenda Ukonga,....
 
Um
Wewe ni moja ya wanawake wenye elimu nzuri. Mwanamke jasiri na mwenye uthubutu wa kuongea jambo lolote ukiliona halijakaa sawa. Elimu yako na sifa zingine lukuki ndizo zimekupa heshima kubwa kwenye jamii ya kitanzania.

Nafahamu wewe ni mwanasheria na una uelewa mpana kuhusu fani hiyo. Unajua kuwa sheria zipo kwa ajili ya kuifanya jamii iishi kwa amani bila kuvunjiana haki za watu. Lakini pia unaelewa kabisa zipo haki ambazo mtu huweza kuzidai ambazo zitauvua utu wa mtu na kudhalilisha watu wengine.

Mimi ni miongoni mwa watu ninaopendezwa na mengi uyafanyayo na uyateteayo lakini sasa naona unataka kuboronga. Naomba usimalize vibaya na kujivunjia heshima yako ambayo sisi vijana tulikuwa tunakupa. Vinginevyo tuwe tulikujua tofauti na ulivyo lakini bila shaka najua uliteleza.

Hatuwezi ruhusu kila kitu kwa kigezo cha haki na maamuzi binafsi ya mtu. Embu fikiria kama tukiruhusu mambo unayoyatetea unadhani nini kitatokea.

Embu fikiria turuhusu Mtoto wa kike alale na Baba yake mzazi unadhani utu wa mtu utakuwa wapi? Kisa tu ni mambo binafsi ya watu. Embu fikiria mtu afanye mapenzi na mnyama unadhani utu wa mtu utakuwa wapi? Embu fikiria sasa hivi hapo wewe utembee na mwanao wa kiume eti kisa tu ni haki na mambo yako binafsi unadhani utu wako utakuwa wapi?

Kujua sheria kusikufanye ukavuka mipaka ya asili. Ukavunja kanuni za asili ambazo zimewekwa na Mungu(sio kwa umuhimu).
Tunahitaji wanawake kama ninyi mpiganie mambo ya msingi. Mambo kama Haki za wanawake, haki za watoto, na mambo mengine. Lakini si kutetea ujinga na upuuzi.

Kujua sherias sio kutetea Uovu na kudhalilisha utu wa mtu. Nilitegemea Mama kama wewe ungetumia muda wako kutoa elimu za kisheria na matamko makali ya kuonya kuhusu tabia za ushoga na usagaji. Ukiwa kama Mzazi wengi wangefurahi kukuona ukiwashauri wadada wanaotupa picha za uchi mitandanoni waache kwani wanadhalilisha jinsia ya kike ukiwemo wewe.

Lakini matokeo yake umepuyanga na kuteleza katika utelezi wa kimagharibi. Sikulaumu wala sikushutumu kwa ulilolitenda kwani najua huenda uliteleza.

Nitakulaumu endapo hutafuta kauli yako. Na ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wako. Maliza vizuri kwa heshima. Wewe si binti tena mpaka uongozwe na mihemko hivyo busara ikutawale umalizapo zamu yako.

Heshima uliyonayo ni kubwa kwenye jamii ndio maana hata Ukachaguliwa na wanasheria wenzako kuwaongoza kwa mwaka huu.

Hii ilitosha kukufungua akili jinsi Watanzania wanavyokuheshimu. Sasa unapofanya mambo haya kiukweli unanipa mashaka mimi na wengine wenye akili za mfano wangu ambao bila shaka ni wengi.

Hatukusoma ili tuudhalilishe utu wetu. Hatukupata nafasi za juu ili tuifanye jamii yetu kuwa ya kinyama. Mambo ya hivyo tuwaachie mataifa mengine. Kama yupo anayependa mambo hayo tutamsaidia kumpa uhamisho aende akaishi huko ili afanye bila shida.

Hata hivyo serikali ni kama imepoa sana kiasi kwamba inaachia baadhi ya mambo yaenda kiholela. Udhalilishaji wa kina mama umekua kwa kiasi kikubwa. Sasa naona unahamia kwa wanaume.
Nilitamani kusikia wanasiasa, wanaharakati, na viongozi wa dini wakipinga mambo haya kwa nguvu zote. Ushoga na kutuma picha za uchi mitandaoni.

Lakini Mhe. Fatuma umeingia katika kundi la wanaowatetea. Haki ndio wanayo lakini si katika taifa hili. Kama unawaonea huruma basi iombe serikali ikupe ruhusa uwahamishia katika nchi zinazokubaliana na mambo hayo

Mhe. Fatuma Karume, ni matumaini yangu kuwa Andiko hili hutoshindwa kulielewa hakika. Nafahamu unahekima ambayo haitashindwa kuona mahali ulipokosea. Muungwana hukubali maonyo bila kujali anaonywa na nani. Usiwavunje moyo vijana wanaokuchukulia kama Role model wao.

Ikufikie ulipo.
View attachment 920312
Umepotea wewe ambaye, hadi leo hujajua kuna watu wanazaliwa tofauti, wengine, na vinasaba vya kike au kiume, wengine wana jinsia mbili, wengine wana hormonal imbalance, basi tufanye kama babu zetu ukizaliwa tofauti unakutana na watu wasiojulikana na unapotea, pumbav.weye
 
wakati ule picha za uchi za mteule wa rais wa mkuu wa wilaya zinapigwa stop kusambazwa huyuhuyu fatuma Karume alijitokeza kuunga mkono watu kusambaza picha hizo ila hakusema yule ni mtu mzima anatumia haki yake ila lilipotolewa tamko la kupambana na mapenzi ya jinsia moja amekurupuka haraka haraka na kutetea watu wanaofanya vitendo hivyo swali la kujiuliza ni kweli anatetea haki za binadamu au anatafuta umaarufu wake binafsi na watu wanaomtumia
 
Hapo hawezi kufuta hiyo kauli maana atakosa ruzuku toka Magharibi huko na hakuna mwanasiasa wa mlengo ule atakaekuja kukemea maana pesa wanapatia huko Magharibi na wanajua wakipina hiko kitu hadharani wanapoteza mapato.
 
Mimi Huyo Shangazi yenu Napingana nae sana katika hili.
Hatuwezi kurekodi vitu vya kijinga tu post mtandaoni, whether accidentally or intentionally, no way!
Yakifumbiwa macho kizazi hiki kitajua ndo fasheni.
Tutafika stage ya Sodoma na Gomorrah kutaka kuwajisi malaika wa Mungu, TUMPINGE huyu Mama,
Je, mwanae akitoa video ya hivyo ataendelea kusapoti?
Wafanye ufuska wao gizani huko na sio kuleta kwa umma.
Kila mtu akirekodi na kupost hii nchi tutakuwaje?
Kila mtu abebe msalaba wake.
Wewe umepotoka kama wengi wengine walivyopotoka.

Sielewi iwapo tatizo ni Ki-kristo (Kidhungu) anachokitumia hakieweki au tena wengi wetu ni wagumu wakuelewa.

Anachokisema 'Shangazi';
Ni lazima Haki,Uhuru na Maamuzi ya Kila Mtanzania kuheshimiwa na kulindwa na Sheria.

Hajasema watu waruhusiwe au Ni Halali kutuma picha 'zisizo na maadili kwenye Mtandao.

Pia, Anadhani (yeye Shangazi) kuwa adhabu ya miaka 30 ambayo inamkabili yule Dada wa Video chafu hailingani na Uzito wa kosa lake.
-Hayo ni maoni yake ambayo hakatazwi kuwa nayo na kuyasema hadharani kama tusivyokatazwa sisi kujadili.

Tuwe na utamaduni wa kusoma na kufuatilia kwa nia ya kuelewa sio kukariri hasa mabandiko ya watu makini kama auntie @fatma_karume aka Shangazi.
 
Jamaa, jifunze kuandika kitu ukizingatia Brevity. Get to the point, ngonjera ndeeeefu kumbe point iko mwisho, tena screenshot, unapoyltezea watu muda kusoma lirisala lako hilo la nn?

Halafu kulala na baba ni 'INCEST', na kwenye post yake hajataja incests, na kulala na wanyama ni 'BEASTIALITY', pia hajaitaja kwenye post yake, acha kumuwekea maneno mdomoni.

Ila na-support hoja kwamba homosexuality si kitu cha kucheka nacho, lazima kipigwe vita kwa nguvu zote

That Includes.....
 
Wewe umepotoka kama wengi wengine walivyopotoka.

Sielewi iwapo tatizo ni Ki-kristo (Kidhungu) anachokitumia hakieweki au tena wengi wenu ni wagumu wakuelewa.

Anachokisema 'Shangazi';
Ni lazima Haki,Uhuru na Maamuzi ya Kila Mtanzania kuheshimiwa na kulindwa na Sheria.

Hujawahi kusema popote kuwa aruhusiwe Mtu kutuma picha 'zisizo na maadili kwenye Mtandao.

Pia, Anadhani (yeye Shangazi) kuwa adhabu ya miaka 30 ambayo inamkabili yule Dada wa Video chafu hailingani na Uzito wa kosa lake.
-Hayo ni maoni yake ambayo hakatazwi kuwa nayo na kuyasema hadharani kama tunavyojadili.

Si pungufu ya hivyo wala si zaidi ya hivyo.
Ila watu sijui ni kusudi au kujifanyisha tu mnapotosha.

Muwe na utamaduni wa kusoma na kuifuatilia kwa la kuelewa kuelewa sio kukariri hasa mabandiko ya wasomi na watu makini kama auntie @fatma_karume aka Shangazi.
Lugha kwangu sio tatizo,
Unaposema haki za binadamu, adhabu na kosa hailingani ana maana gani? Soma kwa makini mkuu.
Wewe uliyemwelewa unadhani sheria iliyopo ya mitandao na masuala ya Kanuni ya adhabu ya homos ipo kufurahisha mtu?
Masuala haya ya kishetani lazima yapate utetezi kwa watu kama ninyi. Rejoice!
 
Kusoma sheria za kidunia ni sawa na bure,Hata wanyama hawafanyiani hivi huyu mama yaonekana hata madrasa hakupita.Ingawa Unguja kuna wanazuoni wengi.Aina ya watu kama huyu mama ni bure kabisa I wish I could be President ningefuta kabisa vyeti vyake vya sheria.
 
Kusoma sheria za kidunia ni sawa na bure,Hata wanyama hawafanyiani hivi huyu mama yaonekana hata madrasa hakupita.Ingawa Unguja kuna wanazuoni wengi.Aina ya watu kama huyu mama ni bure kabisa I wish I could be President ningefuta kabisa vyeti vyake vya sheria.
MHESHIMIWA, USIJITIE MJUVI WA WANYAMA MAANA HAUNA LOLOTE UNALOLIJUA.

HATA UKIPEWA USHAHIDI WA WANYAMA MASHOGA BADO UTAENDELEA KURUKA RUKA NA NGONJERA ZA SODOMA NA GOMORA.
 
Jamaa, jifunze kuandika kitu ukizingatia Brevity. Get to the point, ngonjera ndeeeefu kumbe point iko mwisho, tena screenshot, unapoyltezea watu muda kusoma lirisala lako hilo la nn?

Halafu kulala na baba ni 'INCEST', na kwenye post yake hajataja incests, na kulala na wanyama ni 'BEASTIALITY', pia hajaitaja kwenye post yake, acha kumuwekea maneno mdomoni.

Ila na-support hoja kwamba homosexuality si kitu cha kucheka nacho, lazima kipigwe vita kwa nguvu zote
Mm pia nimewaza hivi
 
Tatizo binadamu wa sasa tumekuwa wanafki sana,
Tunaishi na kutenda km MAFARISAYO
tunajua kunyooshea watu vidole na kujiona sisi bora,
Hebu jiulize
Mzinzi wa kawaida na huyo shoga mbele ya Mungu wanaonekanaje,
Unamlaani shoga,wakati wewe mwizi,ama mzinzi,ama muuaji,ama mchawi,mshirikina nk unadhani pepo utaiona kwa kukosoa wengine,
Siku ya kiama tutaona mengi asee
Tumekuwa wanafki kupiliza,
Huyo huyo aliyeagiza wakamatwe mashoga yy ana madha mbi kibao,lkn anawanyooshea kidole wadhambi wengine,
Kubwa tunapaswa si kubagua dhambi,kuwa hii ni bora hii ni mbaya,
Tukimbie dhambi siyo kubagua dhambi,
Tutubu na kuwaombea tunaoona wanakosea,
 
Unampa ushauri wakati asili yake muarabu kwake ni somebody business analeta upwani bara yaani ndo maana half cast ni cast spicies sehemu nyingine za ulimwengu .....kasoma sheria za ulaya analeta tanzania kama ni mwanasheria wa vyuo vyetu ataelewa sheria zetu haziruhusu ushoga ndo utamaduni wetu bana ....labda hukupita school of law ya TZ baada kurudi shule yake ya UK
Hakuna dhambi na ww unayoifanya,
Acha unafki,
Dhambi ni dhambi
 
Huyu dada anatafuta kiki kwa nguvu sana kumtetea Amba rut kama angekuwa kafanya bahati mbaya sawa lakini amba rut amepost video nyingi sana akifanya mapenzi kwenye mitandao tena akiwa na hiyo shoga walieshtakiwa Naye wakibanduliwa pamoja . Huyu karume simpendi kwa sababu amekula bata sana kwenye familia yao sasa na baada ya kukosa teuzi serikalini anajifanya mwanaharakati . Lakini kwa hili aidha fatma msagaji au anatumika kuvuruga watu.
Kiki?
Itakuwa haujui maana ya kiki,
Mtu aliyekulia ikulu kiki ipi sasa atafute,
Ile kuwa tu mtoto wa ikulu ni kiki tosha,
Umaarufu na uelewa na ujasiri alio nao ni kiki tosha
 
Oza mtoto wako wa kiume kwa dume.
Una hakika mzazi wako ama ndugu yako yyte hajawahi pitia huko,
Hajahalalisha hayo,
Anachosema nao ni binadamu na maadamu ni binadamu waheshimiwe,
Maana mbaya wa Leo ndo mwema wa kesho,
Mwema wa leo ndo mbaya kesho,
Iga mfano wa Yesu hakuwabagua wazinzi walevi watoza ushuru na wadhambi,
Tunachopaswa kufanya siyo kuwabagua ni kuwaelimisha
 
Hili swala la Ushoga ni ngumu sana kulishinda kwa vita ya Damu na nyama /kibinadamu. Hapa inatakiwa Tumuombe Mungu sana awez kutuepusha na janga hli. 2tashinda Ushoga kwa kusal na kufunga. Kilio cha wengi Mungu atajibu kwa wakati 2
Naaam mkuu
TUMUOMBE MUNGU TUTASHINDA,
siyo kuwabagua,
Ukiwabagua wanajifunzaje sasa,
Wanajirekebishaje sasa,
Tukemee kitendo kiovu lkn muovu tumsaidie atoke huko,
Afu skia bana tusiwe Mafarisayo
Ss sote wakosaji,tena wengine wabaya kuliko mashoga,
Leo hii hata wauaji,wachawi,waiba wake na waume za watu nao wanawanyoishea vidole akina Amber
 
Back
Top Bottom