- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu hii ni kweli ?
- Tunachokijua
- Humphrey Polepole ni mwanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba
Madai
Kupitia mtandao wa Facebook mtumiaji mmoja amechapisha taarifa Agosti 8, 2025 iliyoambatana na grafiki yenye utambulisho wa chombo cha habari cha ‘Mwananchi’ ikiwa na ujumbe unaosomeka;
“Fatma Karume: Polepole ni mnafki na msaliti mkubwa”
Grafiki hiyo pia imeambtana na ‘sreenshot’ na ikiwa na utambulisho wa Fatma Karume katika ukurasa wake wa X kuwa amechapisha maneno yanayosomkea kuwa;
“Polepole si mfano wa uongozi, ni kielelezo cha unafki wa kisiasa. Alitutukana wanaharakati, akashindwa kuthibitisha uwezo wake alipokuwa madarakani. Leo anarudi na maneno matupu yasio na mwelekeo. Tanzania inahitaji viongozi wenye msimamo. Si walalamishi wa mitandaoni”
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Grafiki hiyo ni ya kughushi kwani ina mapungufu kadhaa ya kiuandishi, mpangilio na mwandiko ukilinganisha na taarifa rasmi zilizowahi kuchapishw ana chanzo hicho.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Agosti 8, 2025, Mwananchi kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii hawajachapisha taarifa yoyote inayofanania na hiyo.
Aidha inayoonekna kuwa ni ‘Screenshot’ kutoka kwenye ukurasa wa Fatma Karume ni ya kughushi pia. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na Keyword search, JamiiCheck imebaini kuwa Fatma hajaandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa X.