Pole sana kwa matukio na samahani kwa nitakayoyasema.
Nilishaona kwa macho yangu, desk check ya Turkish Air ikiwa imefungwa saa moja kabla. Ila alikuwepo Mbabe mmoja akapiga simu kwa mama mmoja ndani na wakafungua ingawa wafanyakazi wa Turkish Air walishasema kuwa hadi kesho.
Naona nyie mlikosa mtu kama huyo.
Ila nashindwa kuelewa kitu kimoja, ninavyofahamu mie ni kuwa kwa sasa kwa sheria za ulinzi zilivyo uwanja wa ndege, unatakiwa ufike masaa mawili kabla yaani dakika 120 kabla. Sasa wewe nani alikuambia unafika dakika 40 kabla? Dakika 40 kabla ni kuwa ndiyo mnajiandaa kwenda kuingia kwenye ndege tayari na si kwamba ndiyo unafanya Check-In.
Naona ukaja tena kuchelewa hata Bus la kwenda KIA. Yaani hata Bus likakuacha jamani? Nalo sijui utasingizia nini?
Pole sana kwa tukio ila kumbuka kuwa uwanja wa ndege unatakiwa kufika saa MBILI kabla popote pale duniani labda kama umesha Check-In online na huna mzigo, yaani unafika tu na kuingia ndani kusubiri kupanda ndege.
Ukiacha ile arrogance Fastjet wako sahihi kabisa. Kawaida check-in inapaswa kumaliza dakika 30 kabla ya ndege kuruka ili kuwapa marubani kupitia loadsheets kujua wana abiria wangapi, mizigo ya uzito kiasi gani na mafuta kiasi. Bila kufanya hivyo ndege haiwezi kuondoka. Kama check-in imeshafungwa sio rahisi kufungua kwa ajili ya abiria wachache labda liwe jambo la kufa na kupona. Hata pale ambapo ndege imepata hitilafu kama Ground handling Agent yaani Swissport wamefunga usiku Manager wa Fastjet hana cha kufanya. Jifunze kuwahi maana ndege haisubiri mtu labda awe Rais
Ofisi nyingi bongo ongea nao kwa kiingereza na hata mawasiliano fanya kwa kizungu lazima upate huduma wanababaika sana. Kuna siku niliwapigia CRDB kuulizia sim banking.....nitatema yai, walihangaika sana kupata walau wa kuelewa na kunielewesha.....jaribu sikumoja kuwapigia CCM makao makuu ongea kiingereza uone watakavyohangaika hata kukata simu yako.
Pole sana ndugu Tiba,
Customer care ya Watanzania ni mbovu sana karibia kila mahali...
Inasikitisha ila mara nyingi najikuta nikilazimaka kutumia hata vitisho au kujivika vyeo ambavyo sina ili kuruka viunzi ambavyo hawa watoa huduma huweka bila sababu za msingi...
Kwa hiyo kuwastua watu kuwa nawapigia vijana wangu wa Ikulu sasa hivi ni moja ya mambo ambyo huwa yako kwenye amoury yangu!!
Ushauri wa Masanilo pia wa kuwabadilishia lugha baadhi ya hao wapuuzi wakati mwingine unasaidia.
Babu DC!!
Hivi kumbe umeweka mpira kwapani?
SIpigi tena tik tak, uweke tu chini tucheze wote
Pole sana ndugu Tiba,
Customer care ya Watanzania ni mbovu sana karibia kila mahali...
Inasikitisha ila mara nyingi najikuta nikilazimaka kutumia hata vitisho au kujivika vyeo ambavyo sina ili kuruka viunzi ambavyo hawa watoa huduma huweka bila sababu za msingi...
Kwa hiyo kuwastua watu kuwa nawapigia vijana wangu wa Ikulu sasa hivi ni moja ya mambo ambyo huwa yako kwenye amoury yangu!!
Ushauri wa Masanilo pia wa kuwabadilishia lugha baadhi ya hao wapuuzi wakati mwingine unasaidia.
Babu DC!!
gharama nyingi ni zakujitakia...hapakuwa na sababu ya kukodi tax mara tatu toka arusha kwenda KIA. kuna hoteli za kutosha moshi bado ungepata hifadhi. pia gharama ya hoteli ni ya kujitakia.
Dah! siku ya 26 April nikuwepo pia first jet na kweli abiria walilahi waiting longe.
Kwenye siku hiyo hiyo sikia mkasa ulionikuta!
Wengine tuna ma-karama (angels) mambo kama hayo yakitukuta huagiza The flying carpet yajakutubeba...next time just call!!Preta, wewe mkali, mbona hukunishtua na mimi nifuate mkondo jamani?
Tiba
Pole sana mkuu.....kumbe tulikuwa wote pale......ila mwenzio nilicheza ushapu nikaondoka na 5H-CCM.......
Wengine tuna ma-karama (angels) mambo kama hayo yakitukuta huagiza The flying carpet yajakutubeba...next time just call!!
Pole sana.
Lakini taabu yote ya nini, ungepanda tu Luxury Bus kutoka Arusha mpaka Dar, na ungepata faida zifuatazo:
1/Gharama Nafuu(Nauli Haidizi Tsh 30,000/=)
2/Ungepata wasaa wa kufanya utalii wa ndani.
3/Hakuna gharama za ziada zilizojificha(eg.Taxi, VAT, Lugagge Charge nk)
Nikupulizie ka upepo!! :kev:haiyaaaa.....kijukuu cha Alladin.......