Fastjet Arusha: Kauli za wakata tiketi

Fastjet Arusha: Kauli za wakata tiketi

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
3,840
Reaction score
660
wana jf majuzi nilipata hasira sana baada ya kwenda kukata tiketi ya kuja dar asubuh nika mkuta mama mmoja analalamika sana juu ya wale wadada wanao kata tiketi pale jinsi walivyo mjibu wakawa wameshindwa kumuelimisha tofauti ya kukata tiketi ambayo unatakiwa kuondoka siku hiyo hiyo ambayo bei yake ilikuwa 155,000 na wakati mama alikuwa na elfu 75 ndipo wale wadada wakawa wanamuelewesha kwa kumkalipia yani mpaka watu waliokuwa pale ndani wakasikitika sana na majibu ya yule dada kwa yule mama.. Huyo dada jina silikumbuki ila ni mnene mweupe kwa kweli afai hata kuwa kwenye ile ofisi ni janga.
 
cheap is expensive.
 
Mnene_mweupe....namfahamu...ngoja nimnange kimya kimya...lo!
 
zamlock mimi kama msemaji wa fastjet naomba radhi kwa watanzania wote kwa mfanyakazi wetu kukosa nidhamu au lugha nzuri kwa mteja... naomba msamaha sana na ningependa kujua ni ofisi ipi tukio hili lilipotokea, maana tuna ofisi nyingi na huyo dada mweupe alikaa upande upi ukinisaidia kwa hilo nita hakikisha hili swala haltokei tena.
kwa ujumla fastjet tutawaonya na kuwakumbusha wafanyakazi wetu wote juu ya umuhimu wa kuwa na lugha nzuri na yenye busara. nakuahidi measures will be taken.

ASANTE KWA KUICHAGUA FASTJET
 
Hii fastjet siyo kitu ya kupanda tena,maudhi kila kona,hayo ni maamuzi yangu binafsi...kiujumla hamfahi
 
cheap is expensive.

Nadhani hili si swala. Kama kuna kitu ambacho watanzania tunatakiwa kujifunza na kubadilika ni customer care. Wengi wetu tunatafuta kazi kwa kupiga magoti na tukishapata tunakuwa wajeuri. Waangalie baadhi ya wafanyakazi wa Shoprite, Game, Mariedo na sehemu nyingine walivyo wajeuri na kujiona! Ukienda kuulizia kitu na ukawa unashangaa bei wanakuona wa ajabu na mshamba, hebu uliza mishahara yao uone kama wana uwezo wa kununua hata pini hapo wanapofanya kazi? Kinachowaweka hapo ni wizi mdogo mdogo na kuuza sura kwa wakware!

Jamani, ndio maana mahoteli makubwa yamejaa wakenya kama managers! Ina maana vyuo vyote vya hoteli management (pamoja na vile vya utitiri hukoi mitaani) bado tunashindwa kutoa good managers? Hapana sio kweli, shida yetu ni kushindwa kuthamini kazi zetu, ndio maana wakenya wanachukua kazi zetu tunabaki kulalamika!

Jamani kuwa kuwa Fast jet ni cheap ( I am not sure if it is that cheap as they say), haina maana kwamba wafanyakazi wake wanauwezo na ni haki yako kujibu wateja kijeuri. Unachotakiwa kufanya ni kumweleza mteja kwa heshima (kama misingi ya kazi yako inavyokutaka ufanye) and not otherwise!!!

NB: Mkuu Gladdyrix kuna thread nyingine ya tabia mbaya za marubani na wahudumu wa ndege zenu umeiona?
 
tusikalie kimya hao wafanya kazi

they need to be reminded kazi yao

Ila binafsi naamini wanawake wengi wanaojibu watu hovyo huwa na mahusiano na mabosi wao

naweza kuwa nimekosea
 
Kweli amekosea sana,inatakiwa angemuelemisha kwani angepungukiwa na nini?aibu sana!
 
Chezeya mshahara!Uschezee kazi!kwani kupata kazi ndo kazi!! WAHUSIKA WABADILIKE!!
 
FastJet, na ajira ilifanyika fast vile vile kwa watu kuja na vimemo na kupewa kazi. Matokeo yake mnaajiri majanga for your future business. Rekebisha huu upuuzi!!!!

Tiba
 
sio fat jet tu Tanzania karibia yote sehemu wanapotengeneza hela kastama kero huwa ni mbovu tu. tena ukikuta siku hiyo wametengeneza hela hasa. mimi napenda wa Mwanza those people wanajua kuhudukia wateja balaa na kuna hawa wa dara kuna yule wa kwanza ukiingia tu ofisi ya karibia na IFM yule anajali wateja na anawaelewesha vizuri sana. fastjet ni kweli mko cheap lakini kutuuzia soda kwenye ndege hapo ndipo balaa afu bei dah nyie wakali hapo hatujasahau 8000 ya mizigo so kwa hesabu ya haraka haraka nauli 43000 one way hapo taxes included, baggage fees 8000, soda ndogo 3000. jumla 58000 dah mmesahidia sana watanzania ndoto za wengi za kupanda ndege zimetimia. Asanten sana
 
Kwa fast jet Nadhani team nzima imeoza... Nilikuwa nimekata ticket ya katikati ya mwezi Sa kwanza. KIA Dar KiA .baadaye nikalazimika kuhahirisha safari kwenda April. Nikaenda KIA 48 hours before the trip date.mhudumu akaniambia nimwachie atashughulikia...
Kesho yake akanipigia simu kuniambia kulikuwa na Tatizo la system ila nisiwe na wasiwasi system ikiwa ok aatsshughukia. Siku inayofuata ilikuwa jumapili jioni baada ya kumpigia sana bila kupokea simu yangu niliamua kutumia simu ya rafiki yangu ndipo aka pokea na kujipanga namba ya marketing personnel wao makao makuu kwa madai ya Kuwa flight za April hazipo kwenye system.

Nilipompigia Huyo marketing peronel ananiambia nimpigie kesho saa nne. Nikamkumbusha Kuwa kesho ndipo nilitakiwa kusafiri... Akanijibu very short ... Kwamba Hana anoloweza kunisaidia Kwani mpaka muda huo ticket yangu itakuwa no show passenger hivyo sitastahili kusogeza wala kulipwa chochote ....

Hawa fast jet ni wezi
 
wafundishwe huduma bora kwa wateja
 
yes nimeziona na ninazifanyia kazi zote asenteni sana kwa kuyaweka hayo wazi.
 
asante kwa kuipanda na tunaomba radhi sana kwa kero zozote ulizozipata, kumbuka kwamba sisi ni kampuni mpya na carrer mpya Tanzania, mwanzo mgumu ila tunaimani muda si mrefu tutakaa sawa kwani tunarekebisha makosa yetu moja baada ya moja. asante.
 
Muonamambo pole sana kwa hilo lililokukuta, tunaomba utuambie ni marketing personnel gani alokupa hayo majibu? kama unaweza pata jina lake ingesaidia sana kurekebisha kosa hilo lisitokee kwa mtanzania mwingine. ila fastjet sio wezi hata kidogo ndo maana tumeamua kurekebisha madhaifu yetu yote to grow stronger.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom