Wakuu mpoooo!!!!
Huyu inatakiwa VAR imulike bongo lake labda kuna chenga chenga 😂 😂 😂
Wanaovuruga amani ni hao wanaong'ang'ania madaraka kiuhalifu
-------------
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kulinda na kudumisha umoja, utulivu na mshikamano wa taifa, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuruhusu kwa namna yoyote ile hali ya amani iliyopo nchini kuvurugwa.
Akizungumza wilayani Muleba mkoani Kagera, Buruhani amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na wasaidizi wake, ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuleta maendeleo endelevu kwa taifa.
Ameeleza kuwa misingi ya imani na mafundisho ya dini mbalimbali nchini inahimiza utii kwa viongozi, jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa kama sehemu ya kulinda amani, mshikamano na ustawi wa jamii.
Buruhani amewahimiza wananchi wa Kagera kuendelea kuwa walinzi wa amani, akibainisha kuwa utulivu uliopo ni nguzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa taifa la Tanzania.