Farhia Midle mtangazaji wa ITV badilisha staili ya kubana nywele

Habarini wakuu,

Nimekuwa navutiwa na mwanadada huyu mtangazaji wa ITV Farhia Midle katika utangazaji wake lakini kwakweli amekuwa na staili yake moja ya kubana nywele kwa nyuma jamani mpaka inaboa.

Nilikuwa namuomba awe anabadilisha staili mbali mbali za kubana nywele zake maana anaonekana ana nywele nzuri na ndefu.

Nawasilisha
Kwani ni mkeo?Mambo hayo kampangie mkeo
 
Unajua wengine hawana mzuka wa urembo wa nywele.....Sasa hapo alipo yeye anajionea sawa tu......
 
mh! mwe watu mpo busy aisee mpaka nywele za mtangazaji mwingine aliona kola bado miguu,,,,,,
 
Kuna siku nilipata muda wa kuchezea nikaona nitumie kuangalia movie nilikua na mdada fulani wakati tunatizama ile sinema, katikati ya movie akasema mapazia ya nyumba kwenye movie mabaya. Nilishangaa na kuchoka. Wanawake huwa wanawaza nini! Ningeangalia peke yangu nisingeona kabisa yale mapazia. Mnaweza kuangali kitu kimoja ila mwanamke akaona kitu tofauti
Hiyo muvi mlikuwa mnaangalizia geto kwako? Ehee, nini kilifuata baada ya muvi kuisha (kama iliisha kweli)?
 
Mbona hao kina Sam Mapesa hawabadili mitindo ya nywele na tunaangalia news....au naye anyoe kiduku?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom