FAO LA KUJITOA: Tundu Antipas Lissu Kupigania Wafanyakazi

Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Mkuu, Hivi kweli wewe ni binadamu halisi? Maana wakati mwingine isije ikawa kuna vibwengo huku JF . Maana hata haki za watu za wazi wazi unapinga!.
 
Mimi nimepewa fedha yangu toka Nssf tawi la waterfront bila shida yeyote. Nilipeleka form zangu za kujitoa nimekaa mwezi kisha nikaambiwa nikae mwezi nilipokwenda ni kapewa cheque bila shida. Sijatimiza hiyo miaka 55 nina 51yrs. Isipokuwa nilikuwa nafanyakazi chini ya ubalozi kwa kweli ya Mungu sikutoa chochote ili nipewe hiyo fedha. Japo waliniambia hivyo kuwa nina 55 yrs nikawaambia bado but Nikamwambia ninawatoto wanasoma wamefukizwa shule kwa kukosa ada. Nikakubaliwa kujitoa. Namshukuru sana Mungu.
 
Afungue kesi halafu wahanga wa hii sheria kandamizi tuwasilishe vielelezo vya kukataliwa kupewa mafao yetu ili vimsaidie kupambana nao. Akifungua kesi tu tujuzane wakuu
 
Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Kwa hiyo tufwe kikondoo tu huku tukichekelea mafwao yetu wenyewe tukinyinwa? Mbona wanasiasa wao haliwahusu, miaka 5 ikiisha wanachota mamilioni? Je, ni akili au ujuha kupigania haki unayodhulumiwa?

Vv
 
Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Kwa hiyo wewe hujaguswa na suala la watu kuchukua chao? Mbona una ushabiki wa kivyama namna hiyo ndugu yangu!!! Hata kama wewe uko na maisha mazuri(kwa mfano) lakini yupo ndugu,jamaa na rafiki inamuathiri kwa namna moja au nyingine kwa kukosa kuchukua stahiki yake wakati akiwa na afya njema.
Maisha yenyewe ukibahatika ni 60 yrs maximum(on average) sasa hizo penshen za kulia kaburini hazina maana yoyote.
 
wale ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira hawataelewa umuhimu wa thread hii,na sidhani kama wanaelewa kuhusu fao la kujitoa.

utawagundua kwa komenti zao.
naunga mkono hoja.
Mkuu kutoelewa ni ujuha, mimi simo ktk mfumo rasmi lkn najua umuhimu wa hilo fao maana nilipoondoka kwenye mfumo rasmi lilinisaidia sana; infact nilijiondoa kazini ili nipate fao langu nifanye mambo mengine.

Vv
 
Argument ya serikali pamoja na SSRA kuhusu fao la kujitoa ni nzuri, kwamba nia ya mifuko hii ni kuwafanya wafanyakazi wawe pensionable ili waweze kuishi decent life baada ya muda wao wa utumishi kumalizika.

Waingereza wana msemo usemao " NO RULE WITHOUT EXCEPTION" or EXCEPTION CONFIRMS THE RULE" - Kuna makundi maalumu ambao ni wanachama wa mifuko hii ambao kwa nature ya ajira zao ni vigumu sana ku - attain umri huo ambao ni wa kisheria kuwa pensionable: SSRA inaweza ikabadili umri wa kuwa pensionable kwa sekta hizo ambazo zimethibitika zina ugumu wa kukithi matakwa ya sheria hii. Au, wakaruhusu makundi haya maalumu kuendelea na utaratibu uliokuwepo tangu awali wa fao la kujitoa.
Wezi tu hawana lolote. Mimi mwaka 2006 nilienda kuchukua statement ya michango yangu NSSF nikakuta nina 8m lkn riba waliyonipa mwaka huo ni elfu 9, sio wizi huo?

Baba yangu alikuwa mwabachama wa NPF tanfu 1967, hadi anastaafu 2006 balance yake laki 4 wakati akianza kuchangia alibunua nyumba mwaka 1970 kwa shilingi elfu 3, sasa leo unampa 400,000/- yaani hawatoi hata fidia ya thamani ya Pesa,WIZI MTUPU!

Vv
 
Hata akiwapigania Nyuki anajisumbua tu, hana mvuto na wala hakuna anayemjua ukiacha Waajiriwa wa Masha aka Wanasheria!
 
Niko pamoja na TL kwa hilo, maana huu ni upuuzi kuchukua hela ya mtu bila ridhaa yake.
 
Kwa mara ya kwanza nitakuwa upande wa Tundu Lisu. Haiwezekani pesa yenyewe ni million 5 unamwambia asubiri miaka 55 kweli hiyo hela itakuwa na thamani kweli. Wacha niishie hapa kwa leo
 
Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Chama dola ndio muibe jasho letu?.Unajua ni jinsi gani tunapigana kusave hizo hela?..Hebu ficha ujinga wako wewe.
 
Tundu Antipas Lissu, Kuwapigania Wafanyakazi--FAO LA KUJITOA.

Kama kuna watetezi wa wafanyakazi katika nchi hii, basi ni pamoja na Tundu Antipas Lissu. Kwa kutumia taaluma yake, kwa moyo wake wote akishirikiana na Chama cha Wanasheria nchini (TLS) ambacho yeye ndiye Rais (ama kiongozi wa juu), Tundu Lissu ameahidi kushughulikia na kupigania wafanyakazi ili waweze kupata haki yao ya fao la kujitoa mahakamani; (na kwa sasa wapo kwenye mchakato).

Itakumbukwa kwamba, tangu mwezi May mwaka 2016, mifuko ya jamii nchini (PPF/NSSF na mingineyo) ilisitisha utoaji wa fao la kujitoa kwa madai ya kutekeleza sheria ya mifuko hiyo kwamba ili mfanyakazi achukue pesa yake, basi lazima awe amefikisha umri wa miaka 55 au 60.

Yaani wewe kijana mwenzangu na umri wako huo wa miaka 25 au 30 inapotokea leo umefukuzwa kazi na mwajiri, basi kuchukua pesa zako zilizoko kule PPF/NSSF ambazo ni jasho lako, eti unatakiwa kuishi miaka 25 au 30.

Kumbuka hapo, pesa haiongezeki thamani, kumbuka, kuchukua pesa yako haupati riba, kumbuka kodi unalipa ila bado unazuiwa kuchukua haki yako. Toa neno moja kwa Tundu Lissu, wakati huo huo, wafanyakazi wote tumuombee kwa Mungu Tundu Antipas Lissu--Jembe. Kwa maana yeye ndiye anaonekana kuwa mtetezi wetu wafanyakazi.

*Zingatia: Kama Mwanasheria, na Rais wa Chama Cha Wanasheria (TLS), anayo MAMLAKA ya kuishitaki serikali kwa jambo lolote pale anapoona mambo hayako sawa. Maana wapo watakaohoji....'yeye kama nani'? Pili...wapo watakaohoji, kwa nini TUCTA wako kimya? Jibu ni kwamba, TUCTA si wenzetu wale, hawako kupigania maslahi ya wafanyakazi, in a nutshell, they (TUCTA) are opportunists.

Solidarity Forever, For The Union Makes us Strong.
Kuna hukumu ya mahakama ya rufani ya hili suala au lifananalo na hili suala
 
Na abarikiwe na Mungu kila ateteaye wanyonge.

FAO LA KUJITOA ni haki yetu ya msingi kwa kuzingatia mazingira na hali zetu za kiuchumi. Serikali dhalimu, kupitia taasisi hizi za hovyo zinatumia fedha hizi kwenye miradi ambayo haina manufaa ya moja kwa moja kwa mdau wa mfuko.

Ikiwa kweli wadhalimu hawa wana nia njema na FUTURE zetu, basi tusingeona mipango ya miradi ambayo tafsiri yake ni KEJELI kwa watu maskini. NSSF inauza nyumba 114m, kitu ambacho ni kiinimacho kwa mwanadamu Mtanzania ambaye wanamuandaa kufa siku chache baada ya kustaafu.

Kuna sisi ambao ajira zetu ni kukodishwa kama maturubai. Tunapewa mkataba wa mwaka mmoja mmoja tu na waliokutodisha kwenye makampuni ya kimataifa. Hatukopesheki na taasisi yeyote ya fedha. Siku na saa yeyote, unaambiwa kuanzia next month hatutakuwa na wewe. Nitasubiri miaka 25 ndio nipate hizo senti ambazo ungenipa leo pengine zingekuwa mtaji?

Ikiwa serikali inakopeshwa fedha zangu zilizo NSSF, mbona nisidhaminiwe na amana yangu iliyopo huko hata nipate mkopo wa nusu ya hiyo amana kutoka benki na mimi ninunue kiwanja nyie watu?

Serikali dhalimu haina muda wa kuangalia wananchi wake. Saa zote bize kukimbizana na wanaotafuta riziki zao.
Aaaaaaaaah aisee umeandika mambo yanayotia hasira na simanzi kweli!! Cha kushangaza kuna watu bado wanaleta uccm na uchadema hata kwa hili pia

Najiuliza labda watu hao ndo huwa wananufaika na fedha zetu moja kwa moja!?

Kwa sababu kama wewe sio unaenufaika na haya mafao yetu huwezi kuacha kuungana na watu wanaojitoa kwa moyo wao kutupigania sisi tunaodhurumiwa ktk hili.
 
Back
Top Bottom