FAO LA KUJITOA: Tundu Antipas Lissu Kupigania Wafanyakazi

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
tundu.jpg

Tundu Antipas Lissu, Kuwapigania Wafanyakazi--FAO LA KUJITOA.

Kama kuna watetezi wa wafanyakazi katika nchi hii, basi ni pamoja na Tundu Antipas Lissu. Kwa kutumia taaluma yake, kwa moyo wake wote akishirikiana na Chama cha Wanasheria nchini (TLS) ambacho yeye ndiye Rais (ama kiongozi wa juu), Tundu Lissu ameahidi kushughulikia na kupigania wafanyakazi ili waweze kupata haki yao ya fao la kujitoa mahakamani; (na kwa sasa wapo kwenye mchakato).

Itakumbukwa kwamba, tangu mwezi May mwaka 2016, mifuko ya jamii nchini (PPF/NSSF na mingineyo) ilisitisha utoaji wa fao la kujitoa kwa madai ya kutekeleza sheria ya mifuko hiyo kwamba ili mfanyakazi achukue pesa yake, basi lazima awe amefikisha umri wa miaka 55 au 60.

Yaani wewe kijana mwenzangu na umri wako huo wa miaka 25 au 30 inapotokea leo umefukuzwa kazi na mwajiri, basi kuchukua pesa zako zilizoko kule PPF/NSSF ambazo ni jasho lako, eti unatakiwa kuishi miaka 25 au 30.

Kumbuka hapo, pesa haiongezeki thamani, kumbuka, kuchukua pesa yako haupati riba, kumbuka kodi unalipa ila bado unazuiwa kuchukua haki yako. Toa neno moja kwa Tundu Lissu, wakati huo huo, wafanyakazi wote tumuombee kwa Mungu Tundu Antipas Lissu--Jembe. Kwa maana yeye ndiye anaonekana kuwa mtetezi wetu wafanyakazi.

*Zingatia: Kama Mwanasheria, na Rais wa Chama Cha Wanasheria (TLS), anayo MAMLAKA ya kuishitaki serikali kwa jambo lolote pale anapoona mambo hayako sawa. Maana wapo watakaohoji....'yeye kama nani'? Pili...wapo watakaohoji, kwa nini TUCTA wako kimya? Jibu ni kwamba, TUCTA si wenzetu wale, hawako kupigania maslahi ya wafanyakazi, in a nutshell, they (TUCTA) are opportunists.

Solidarity Forever, For The Union Makes us Strong.
 
Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
 
Namuunga Mkono 100% niko nyuma yake kwenye hili.. Ni heri serikali kama haitosheki na PAYE ni bora wakapendekeza kodi ingine wakiweke milele na sio kunizuia kuchukua mlungura wangu.. Kamwe sitakaa na kulichekea hili..Iliniuma saana wakati swala hili linapitishwa.
 
Back
Top Bottom