Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 17,057
- 18,406
Hii mihimili siielewi. Sheria ya FLK ilipitishwa na Bunge (Mhimili) Tundu Lissu anaenda mahakamani (Mhimili) kupinga Bunge. Hivi hii mihimili inaweza kupingana kweli?Ni mahakamani...aisee.
Hii mihimili siielewi. Sheria ya FLK ilipitishwa na Bunge (Mhimili) Tundu Lissu anaenda mahakamani (Mhimili) kupinga Bunge. Hivi hii mihimili inaweza kupingana kweli?Ni mahakamani...aisee.
Tatizo lenu vijana wa mitandaoni hampo kwenye ajira rasmi ndio maana lazima mtapinga. Mkishapokea buku saba yenu basi kesho itajitegemea.Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Huoni Mantiki ya kupinga fao la kujitoa!?Jamaa anahangaika kweli, lkn hajui masikini ya Mungu, CCM ni Chama Dola hizo kiki zote zinaishia ukingoni!
Mkuu, unatakiwa uwe serious kwenye mambo ya maana. Halafu unajiita doctor? Pambafu thana!
NSSF ni matapeli haswa.Kwakweli nitamshangaa Mtanzania atakayepinga hili, ukienda kwenye hizi Ofisi za Mifuko ya Jamii utawaonea huruma wanaodai mafao yao. Mlalahoi kafanya kazi anadai milioni 1 tu lakini anazungushwa hakuna maneno. PPF wako wazi kusema njoo ukifikisha miaka 55, NSSF wao wanakupiga kalenda kama ya miezi 4 hivi, ukienda unapigwa tena miezi 4.
Ni mahakamani...aisee.
Mungu ambariki mtani wangu,maana nilikuwa nmeshajiwekea malengo baada ya mwaka Mungu akipendezwa nngeachana na hii kazi ya mhindi nihangaike na mambo yangu , lkn hawa pumbafu wanataka tusichukue hela zetu, kazi tufanye sisi matumizi ya pesa zetu watupangie
Tundu Antipas Lissu, Kuwapigania Wafanyakazi--FAO LA KUJITOA.
Kama kuna watetezi wa wafanyakazi katika nchi hii, basi ni pamoja na Tundu Antipas Lissu. Kwa kutumia taaluma yake, kwa moyo wake wote akishirikiana na Chama cha Wanasheria nchini (TLS) ambacho yeye ndiye Rais (ama kiongozi wa juu), Tundu Lissu ameahidi kushughulikia na kupigania wafanyakazi ili waweze kupata haki yao ya fao la kujitoa mahakamani; (na kwa sasa wapo kwenye mchakato).
Itakumbukwa kwamba, tangu mwezi May mwaka 2016, mifuko ya jamii nchini (PPF/NSSF na mingineyo) ilisitisha utoaji wa fao la kujitoa kwa madai ya kutekeleza sheria ya mifuko hiyo kwamba ili mfanyakazi achukue pesa yake, basi lazima awe amefikisha umri wa miaka 55 au 60.
Yaani wewe kijana mwenzangu na umri wako huo wa miaka 25 au 30 inapotokea leo umefukuzwa kazi na mwajiri, basi kuchukua pesa zako zilizoko kule PPF/NSSF ambazo ni jasho lako, eti unatakiwa kuishi miaka 25 au 30.
Kumbuka hapo, pesa haiongezeki thamani, kumbuka, kuchukua pesa yako haupati riba, kumbuka kodi unalipa ila bado unazuiwa kuchukua haki yako. Toa neno moja kwa Tundu Lissu, wakati huo huo, wafanyakazi wote tumuombee kwa Mungu Tundu Antipas Lissu--Jembe. Kwa maana yeye ndiye anaonekana kuwa mtetezi wetu wafanyakazi.
*Zingatia: Kama Mwanasheria, na Rais wa Chama Cha Wanasheria (TLS), anayo MAMLAKA ya kuishitaki serikali kwa jambo lolote pale anapoona mambo hayako sawa. Maana wapo watakaohoji....'yeye kama nani'? Pili...wapo watakaohoji, kwa nini TUCTA wako kimya? Jibu ni kwamba, TUCTA si wenzetu wale, hawako kupigania maslahi ya wafanyakazi, in a nutshell, they (TUCTA) are opportunists.
Solidarity Forever, For The Union Makes us Strong.
NSSF ni matapeli haswa.
Ww acha tu mkuu watu hawajui changamoto tunazokutana nazo makazini na hawana huruma na sisiNimesoma kwa uchungu sana hii meseji.
Mkuu wale watu wanashida kubwa sana.Halafu wanajibu kwa dharau mnoo.
Jàman mbona watu wanachukuwa mafao yao mifiko yte inatoa mafao tena kwa fasta sana ushahidi upo kabisa