Family Tree 🌳/Chimbuko la Familia

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,501
41,914
Habari za kuamka mabibi na mabwana,

Popote pale ulipo ukiwa unasoma huu uzi, salamu za kheri zikufikie.

Kichwa cha uzi chahusu Chimbuko la familia aka Family Tree. Kwenye kitabu kimojawapo cha dini kiliandika kuhusu laana kumpatiliza mtu hadi kizazi chake cha nne. Kizazi cha nne kurudi nyuma wewe/mimi nikiwa hicho kizazi cha nne, kizazi cha kwanza ni babu wa wazazi wetu ama wazazi wa babu zetu.

Naamini ni watu/familia chache sana hubahatika kuona vizazi vya tano na sita ama mimi na wewe tukiwa vizazi vya tano na sita ni mara chache sana kukuta tumeona kizazi cha sita kurudi nyuma yaani hata sijui uwaiteje.... kwa lugha ngeni grand grand parents huko.

Labda najiuliza, nini maana ya kujua chimbuko la ulikotoka ama kizazi cha nne, tano au sita kurudi nyuma.

1. Kujua haswa magonjwa ya kurithi
2. Kuna vitu vinatembea kwenye familia kama mkono wa biashara au uongozi n.k.
3. Saa nyingine ni faida ya vizazi vijavyo hata kuhifadhi picha zao.

Binafsi natamani kufanya hii family Tree ila sijaipa kipaumbele.

Kuna mtu alinigusia, kuna nguvu za asili nyuma yake... wengi huishia njiani na wako wanaotunza huu utamaduni.

Sina mfano wowote wa familia zilizoweka hii family Tree ukiacha Royal Families....

Wasalaam,

Kasinde Mahaba Matata.
 
I love you Mama, huu Uzi ni mzuri sana, Ila Amini usiamini Kasie atatokea mfuasi wa nabii fulani very fake, atakwambia kwamba family tree ni laana na ibada za mizimu na ni ushetani wa kupigwa vita.

Bila kujua ulikotoka, kamwe hutojua uendako..
 
Ni bahati ya kipekee hata kuona kizazi cha nne , au cha cha kwanza kwa maana ya baba yake babu, babu , baba, Na mimi.
Katika hali ya kawaida sio rahisi kwa kuwa mitindo ya maisha yetu kwa kipicho hiki tulicho nacho kuweza kumkuta babu yupo hai na sisi wajukuu tumesha pata ufahamu.

Sasa nende mbele kidogo umkute baba babu wa babu wangu yangu ambea atakuwa wa tano na baba yake huyo babu wa babu! Ni ngumu mno na karibu kwa dunia nzima hata kama sina takwimu ni nadra mno kukuta hivyo kiasi cha kwamba hamna .

Hili somo la mti wa ukoo au familia nimelisikia sana likieleza sana habari za laaana kuvuka kizazi kwenda kizazi.
Mara chache sana wafundishaji waliweza kuzungumzia baraka,wao kwenye hili ni laana tu ndio inafanya kazi!

Kidogo nilikuja kuona ni mawazo tu ya binadamu hamna uhalisia wowote, sisi binadamu nunapo kosea hatukubali kosa bali tunatafuta wa kumsingizia na cha kusingizia, ni asili ya binadamu kukwepa kosa lake na matokeo ya kosa lake kwa kumpasia mwingine ikiwepo shetani.
 
Back
Top Bottom