Family friendship inapovuka mipaka...

Family friendship inapovuka mipaka...

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,356
Haya mambo za mapenzi hayana dalili wala hodi sometimes, hiki ni kisa cha mtaani kwetu.

Familia mbili changa zimekuwa kwenye level ya juu sana ya family friendship.Wababa wenye hizo nyumba wameoa mwaka mmoja,wake zao wote ni wabichi.

Familia hizi ambazo wote wanne ni waajiriwa wa serikali wawili sehemu moja, wengine sehemu tofauti tofauti. Katika kuendeleza urafiki wakaanza michezo ya hapa na pale jioni wakitoka kazini kwa baadhi ya siku huku foleni hamna, so wanafika mapema tu. Walianza na gym kwa pamoja, baadae pool table baa ya jirani, kisha karata, kisha michezo ya computer nk.

Ila utata umekuwa hapa kwenye karata, ambapo wamekuwa wakicheka michezo maarufu ya arba na last card. Najua zina majina tofauti lakini sisi twaita hayo. Wametengeneza timu mbili kwenye karata, na ili kuondoa ufamilia, mke wa mmoja ameteam na mme wa mwingine and vice versa. Mjuavyo karata zina maneno mengi ya utani mfano; nakulambisha, msimamishe, napeleka mchezo nyuma,narudisha mbele, n.k. Lakini ikumbukwe hapa partner wa mmoja ni mke/mume wa rafiki yake...

Sasa mmoja wa hawa wanaume ambaye ni mshikaji job, ndo anakuja kunipa stori kuwa walizoeana sana na partner wake kwenye karata ambaye ni mke wa rafiki yake. Na kuwa mchezo haukuishia hapo kwani kuna siku ilitokea wakaenda safari ya kikazi kwa siku 6 mkoa mwingine na kuanzia siku ya pili shemeji akawa anakuja room kwa mshikaji na karata akisema eti ameshakuwa addicted.

Karata zilichezwa huku wakiendeleza ule utani wa maneno. Jamaa ananiambia utani haukuishia kwenye maneno kwani mtu alipoambiwa lamba tano utani wa kulamba ulihamia mwilini na yaliyotokea hayaelezeki hapa MMU.

Ndugu wanajumuiya wenzangu wa jumuiya hii ya ndoa, hebu tuweni makini na mipaka ya family friendship, unless tumeamua kuuishi ule usemi wa kizuri kula na nduguyo.
 
nakuunga mkono jamaa yangu kila kitu kinapaswa kuwa na mipaka, hao na hiyo family friendship yao ilivuka mipaka halafu na hao waliowasaliti wenzao wakatumia chance hiyo kama excuse.
 
Mh Tuko kwa urafiki huo mimi sina kabisa....sitaki ata kufikiria
 
Last edited by a moderator:
Urafiki wa kifamilia unapoingia mpaka kwa watoto wanaishia kumenyana kama pipi tu.
 
Hao waume ni wangese, wameoa fasheni tu. Kila familia lazima iwe na privacy yake. Wanaishi maisha ya bf/gf au kigheto wakati washaoa?

Wote na wanawake zao hamnazo kabisa.
Mie ningekuwa mke ningepiga marufuku haraka sana.
 
Hii ni kwa upande mmoja.
Huenda upande mwingine mchezo ni huo huo...
Cha msingi wakubaliane waanze kufanya Foursome ili kudumisha Muungano wao..
 
utafiti hii kitu hairuhusiwi kabisa wala kukaribisha urafiki wa aina hiyo na nikikumbuka kuwa hakuna rafiki mbele ya mke wako hapo ndo kabisa
 
Last edited by a moderator:
Mie kucheza Karata na dada tu na kidume kingine siwezi..sembuse mke
 
mhhhhhhh wote majanga hao wameoa na kuolewa wakiwa bado hawajui jinsi ya kusimama kwenye nafasi zao
 
Kila jambo au kitu katika maisha kinahitaji mipaka, zaidi ya hapo ni kutafutiana lawama za kujitakia
 
Kwangu rafiki mwisho kituo cha basi!! ........................... nashukuru Mungu watu wote nawaona sawa hakuna cha rafiki wala adui. Watu wote wameharibika, wote kabisa.
 
Back
Top Bottom