bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 701
- 1,643
Unaogopa Kuchitiwa Wakati Wewe Ndiye Bingwa wa Michezo!
Dunia ya sasa imekuwa ya ajabu sana, hasa hapa mjini ambapo kila mtu anajifanya mjanja. Lakini kuna ile hali moja inayovunja mbavu na kuacha maswali mengi: unakuta mtu ndio kinara wa "kuchepuka," yaani ana 'substitutes' hadi benchini zimejaa, lakini huyo huyo ndio anakuwa na wivu wa kijinga na uoga uliopitiliza kuibiwa. Ni kama mwizi anayeogopa kuibiwa redio.
Moyoni najua kabisa nachokifanya siyo poa. Hivyo, kila saa nakuwa na hofu kwamba malipo ni hapa hapa duniani. Naogopa kuwa mhanga wa mchezo ambao mimi ndio kocha mkuu..
Kuchiti ni kama mchezo wa karata. Unajihisi mjanja unapokuwa na turufu, lakini ukihisi mwenzako naye ana karata ya dume, unachanganyikiwa.
"Siku hizi mapenzi yamekuwa kama kuishi kwenye nyumba ya vioo huku unarusha mawe. Unarusha jiwe kwa jirani unachiti, lakini muda wote unajikinga usivunjiwe kioo chako.
Inachosha sana kuishi kwa mashaka. Unajikuta unatumia nguvu nyingi kulinda "mali" yako huku wewe mwenyewe ukiwa ni mwizi wa mali za watu. Tunajifanya maprofesa wa uaminifu mbele za watu, kumbe mioyoni mwetu sisi ndio matapeli namba moja wa hisia.
Inasikitisha lakini ndio ukweli wa mtaa; tunapendana kwa 'remote' huku kila mtu akiwa na betri zake mfukoni tayari kubadilisha channel muda wowote..