Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
Kuna swali ambalo huwa ninajiuliza kila mara tochi inapoangaza yaliyokuwa mahusiano ya Mwl. Nyerere na Mandela.
Kwa nini Mandela hakuhudhuria mazishi au kwenye memorial service ya Mwl. Nyerere?.
Tumeona viongozi wengi wa mataifa mbali mbali, makubwa na madogo wakibadilisha ratiba zao ili kuhudhuria memorial service yake, lakini yeye ambaye viongozi wetu walikuwa wanatuaminisha na wameendelea kutuaminisha kuwa walikuwa karibu sana katika majukumu ya kiutendaji wa jamii na kifamilia, lakini hakuweza kurekebisha ratiba yake ili ahudhurie.
Kuhudhuria kwa Mama Graca ukiangalia kwa undani hukukufanyika kwa sababu alikuwa mke wa Mandela, bali kulifanyika kwa sababu aliyekuwa Mme wake Mama Graca (Samora Machel) alikuwa karibu sana na Mwl. Nyerere.
Samora Machel hakuwahi kukutana na Mandela na kwa maana hiyo, hata mahusiano aliyokuwa nayo na Mwl. Nyerere hawezi kuyafahamu kwa undani zaidi ya kuelezwa na Mama Graca.
Mzee Mandela baada ya kutoka Jela, alijikuta akikumbatiwa bila kufurukuta na watu wa nchi za Magharibi ambao walikuwa na maslahi makubwa South Africa kiasi kwamba akaanza hata kuwasahau wapigania uhuru wengine kama Mwl. Nyerere. Siyo ajabu hata wakati wa memorial service na mazishi vilimkuta akiwa kwenye nchi hizo na akaendelea kuwepo huko!.
Hata kitabu chake kinachoenda kwa jina la Long Walk to Freedom by Nelson Mandela (1994) pia kimewasahau na kuishia kudodosa dodosa tu.
Ama kweli, tenda wema uende zako.......
Mwl. Nyerere alitenda wema kwa walalahoi wa Afrika kusini na akaenda zake lakini makovu ya kiuchumi na kisiasa tuliyoyapata kwa kuisaidia Afrika Kusini bado tunayauguza mpaka leo.
Ndugu zangu watanzania, wale mliofuatilia hotuba ya viongozi wakuu wa South Africa kwenye mazishi ya Nelson Mandela, kwenye hotuba hizo kuna nchi zilitajwa km ndizo zilizotoa mchango mkuu wa upatikaniji au ufanikishaji wa South Africa kupata uhuru!
JAMBO LA KUSHANGAZA HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA WA SOUTH AFRICA KATI YA WALE WALIOTOA HOTUBA ALIYEITAJA TANZANIA KAMA NCHI MUHIMU ILIYOJITOLEA KILA HALI KUISADIA SOUTH AFRICA NA CHAMA CHA ANC KUPATA UHURU, NI KWANINI?
Kuna swali ambalo huwa ninajiuliza kila mara tochi inapoangaza yaliyokuwa mahusiano ya Mwl. Nyerere na Mandela.
Kwa nini Mandela hakuhudhuria mazishi au kwenye memorial service ya Mwl. Nyerere?.
Tumeona viongozi wengi wa mataifa mbali mbali, makubwa na madogo wakibadilisha ratiba zao ili kuhudhuria memorial service yake, lakini yeye ambaye viongozi wetu walikuwa wanatuaminisha na wameendelea kutuaminisha kuwa walikuwa karibu sana katika majukumu ya kiutendaji wa jamii na kifamilia, lakini hakuweza kurekebisha ratiba yake ili ahudhurie.
Kuhudhuria kwa Mama Graca ukiangalia kwa undani hukukufanyika kwa sababu alikuwa mke wa Mandela, bali kulifanyika kwa sababu aliyekuwa Mme wake Mama Graca (Samora Machel) alikuwa karibu sana na Mwl. Nyerere.
Samora Machel hakuwahi kukutana na Mandela na kwa maana hiyo, hata mahusiano aliyokuwa nayo na Mwl. Nyerere hawezi kuyafahamu kwa undani zaidi ya kuelezwa na Mama Graca.
Mzee Mandela baada ya kutoka Jela, alijikuta akikumbatiwa bila kufurukuta na watu wa nchi za Magharibi ambao walikuwa na maslahi makubwa South Africa kiasi kwamba akaanza hata kuwasahau wapigania uhuru wengine kama Mwl. Nyerere. Siyo ajabu hata wakati wa memorial service na mazishi vilimkuta akiwa kwenye nchi hizo na akaendelea kuwepo huko!.
Hata kitabu chake kinachoenda kwa jina la Long Walk to Freedom by Nelson Mandela (1994) pia kimewasahau na kuishia kudodosa dodosa tu.
Ama kweli, tenda wema uende zako.......
Mwl. Nyerere alitenda wema kwa walalahoi wa Afrika kusini na akaenda zake lakini makovu ya kiuchumi na kisiasa tuliyoyapata kwa kuisaidia Afrika Kusini bado tunayauguza mpaka leo.
Mkuu, usinunue hizi ngonjera za kisiasa. Angalia wewe mwenyewe kwa macho matatu.Ni kweli Mandela hakuhudhuria mazishi ya Nyerere, nakumbuka taarifa zilisema kuwa anajisikia vibaya na atasononeka sana ukihudhuria mazishi ya Mwalimu. Hata hivyo,mara baada ya Mwalimu kuzikwa Mandela alienda Butiama (26/11/1999). Na nakumbuka uwanja wa Ndebele alipokelewa na waziri wa mambo ya nje Kipindi hicho Kikwete. Kama hivyo imejitokeza kwa mama Maria, afya yake haimruhusu kwenda kwenye pilika pilika za mazishi.
Ni kweli Mandela hakuhudhuria mazishi ya Nyerere, nakumbuka taarifa zilisema kuwa anajisikia vibaya na atasononeka sana ukihudhuria mazishi ya Mwalimu. Hata hivyo,mara baada ya Mwalimu kuzikwa Mandela alienda Butiama (26/11/1999). Na nakumbuka uwanja wa Ndebele alipokelewa na waziri wa mambo ya nje Kipindi hicho Kikwete. Kama hivyo imejitokeza kwa mama Maria, afya yake haimruhusu kwenda kwenye pilika pilika za mazishi.
Huu ni upotoshoaji. Kuonyesha wanatambua umuhimu wa Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ataongea kwenye mazishi kijijini QUNU kutokana na ukaribu wa Tanzania na ANC na South Africa kwa ujumla.
Source: City Press News Paper (City Press - The home of City Press online)
Mkuu, usinunue hizi ngonjera za kisiasa. Angalia wewe mwenyewe kwa macho matatu.
Mandela wakati akiwa jela, alifiwa na Mama yake na Mwanae. Mbona aliomba ruhusa ili akawazike?. Kwa nini hakusema siendi kwa vile nitasononeka sana!. Itakuwa Rafiki wa kukutana barabarani na kwenye majukwaa ya kisiasa?.
Mbona aliweza pia kuhudhuria kwenye msiba ya mtoto wake wakati alikuwa hajiwezi vizuri hata kutembea?.
Ndiyo maana mara nyingi siwapendi wanasiasa kwa sababu kama hizi za kutufanya sisi ni kama wajinga fulani!.