Sababu ya kujisikia vibaya ni DHAIFU mno kwa sababu zifuatazo.
1. Mandela amewahi kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Africa Kusini. Kazi hiyo inahitaji ujasiri mkubwa. Mtu aliyeimudu kazi hiyo pamoja na kuvumilia jela miaka 27 hawezi kukosa ujasiri wa kuhudhuria mazishi ya rafiki.
2. Nyerere amefariki akiwa na umri wa miaka 77. Huu sio umri mdogo wa kufanya kifo chake kiwe habari ya kusononesha kiasi cha kushindwa kuvimilia kuwepo.
3. Je, Mandela aliumizwa zaidi kuliko watoto wa Nyerere na mama yao? Mbona wao waliudhuria mazishi ya Baba yao pamoja na uchungu walio nao.
4. Je, Mandela alimpenda Nyerere zaidi kuliko ndugu zake wote? Je, mazishi ya ndugu zake hakuwa akihudhuria?
Ninachoona ni kwamba Mandela alikuwa hataki mazishi ya Nyerere yawe triumph. Alijua uwepo wake utafanya mazishi hayo kupata coverage kubwa na akajiweka kando. Lengo ni kiogopa kutonesha vidonda vya "wazungu".
Nchi za magharibi zinailaumu Tanzania kwa kuvipa mafunzo vikundi vya ANC ambavyo according to wamagharibi vikundi hivyo ni vya kigaidi.
Mandela anaonekana alihofia kukumbushia historia hiyo. Kwa watu wa magharibi kilichofanywa na Tanzania
pale Mazimbu Morogoro sio ushujaa ila ni ugaidi. Mandela anaonekana kukubaliana na wanagharibi kwenye hili. Anaona aibu kujiweka karibu na watu waliounga mkono "ugaidi" wake ili asiwaudhi "wakubwa".
Kwa kuongezea, Mandela angetambua mchango wa Tanzania, kipindi cha utawala wake angefuta visa kwa watanzania, lakini haikufanyika hivyo bali kinyume chake Wakenya wakawa na ruhusa ya kuingia Afrika Kusini bila visa! Mpaka manual alipoingia Zuma ndiyo watanzania wakaruhusiwa kuingia bila visa! Kumbuka maslahi ya wamagharibi yaliyoko Afrika Kusini ndiyo hayo hayo yaliyoko Kenya.