Familia ya Mwl. Nyerere yaalikwa kwenye mazishi ya Mandela

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Familia ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere itawakilishwa katika mazishi ya Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye atazikwa kesho katika Kijiji cha Qunu, Mthatha Jimbo la Eastern Cape.

Habari ambazo gazeti hili lilizipata jana mjini Pretoria zinasema kuwa Mama Maria Nyerere, ambaye ni mjane wa Baba wa taifa, alialikwa kuhudhuria mazishi hayo kwa kuzingatia uhusiano uliopo baina ya familia hizo mbili.

Hata hivyo, imethibitika kuwa Mama Maria hataweza kuhudhuria mazishi hayo kesho, badala yake amewatuma wawakilishi ambao ni mabinti zake wawili; Anna Nyerere ambaye ni mtoto wa pili na mtoto wake wa saba, Rosemary Nyerere.

Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa sita wa Mwalimu alithibitisha jana kwamba familia yao imealikwa kushiriki mazishi hayo, lakini akaweka wazi kwamba: "Mama hataweza kwenda kuzika, atakwenda baadaye kidogo baada ya mazishi kufanyika."

Madaraka alisema kwa jinsi afya ya mama yake ilivyo sasa, hataweza kwenda Qunu. "Kwa kawaida mazishi haya ya kitaifa huwa yana mambo na pilika nyingi, kwa hiyo mama ameona asubiri," alisema.

Kuhusu kifo cha Mandela, Madaraka alisema kwamba kama wanafamilia, wameguswa na msiba huo na kuwa kimewakumbusha uchungu walioupata wakati walipofiwa na baba yao Oktoba 14, 1999.

"Kwa kweli tumeguswa sana na msiba na tunawapa pole sana, tunakumbuka kwamba wakati baba alipofariki, Mama Graca tulikuwa naye, alikuja kabla ya mazishi na alikuwepo kwenye mazishi na baada ya mazishi aliendelea kukaa kwa siku kama saba," alisema Madaraka na kuongeza:

"Pia tunakumbuka kwamba Mzee Mandela yeye alikuja baadaye mpaka Butiama kutoa pole. Ilikuwa Novemba 26, 1999 kwa hiyo tunaguswa na msiba huu." Awali, gazeti hili lilidokezwa kwamba watoto hao wa Nyerere walikuwa wamefikia katika Hoteli ya Burgers Park, Pretoria lakini walipotafutwa katika hoteli hiyo wafanyakazi walisema kwamba tayari walikuwa wameondoka.

Kwa hisani ya Mwananchi.
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Kuna swali ambalo huwa ninajiuliza kila mara tochi inapoangaza yaliyokuwa mahusiano ya Mwl. Nyerere na Mandela.

Kwa nini Mandela hakuhudhuria mazishi au kwenye memorial service ya Mwl. Nyerere?.

Tumeona viongozi wengi wa mataifa mbali mbali, makubwa na madogo wakibadilisha ratiba zao ili kuhudhuria memorial service yake, lakini yeye ambaye viongozi wetu walikuwa wanatuaminisha na wameendelea kutuaminisha kuwa walikuwa karibu sana katika majukumu ya kiutendaji wa jamii na kifamilia, lakini hakuweza kurekebisha ratiba yake ili ahudhurie.

Kuhudhuria kwa Mama Graca ukiangalia kwa undani hukukufanyika kwa sababu alikuwa mke wa Mandela, bali kulifanyika kwa sababu aliyekuwa Mme wake Mama Graca (Samora Machel) alikuwa karibu sana na Mwl. Nyerere.

Samora Machel hakuwahi kukutana na Mandela na kwa maana hiyo, hata mahusiano aliyokuwa nayo na Mwl. Nyerere hawezi kuyafahamu kwa undani zaidi ya kuelezwa na Mama Graca.

Mzee Mandela baada ya kutoka Jela, alijikuta akikumbatiwa bila kufurukuta na watu wa nchi za Magharibi ambao walikuwa na maslahi makubwa South Africa kiasi kwamba akaanza hata kuwasahau wapigania uhuru wengine kama Mwl. Nyerere. Siyo ajabu hata wakati wa memorial service na mazishi vilimkuta akiwa kwenye nchi hizo na akaendelea kuwepo huko!.

Hata kitabu chake kinachoenda kwa jina la Long Walk to Freedom by Nelson Mandela (1994) pia kimewasahau na kuishia kudodosa dodosa tu.

Ama kweli, tenda wema uende zako.......

Mwl. Nyerere alitenda wema kwa walalahoi wa Afrika kusini na akaenda zake lakini makovu ya kiuchumi na kisiasa tuliyoyapata kwa kuisaidia Afrika Kusini bado tunayauguza mpaka leo.
 
remon

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
295
170
Ndugu zangu watanzania, wale mliofuatilia hotuba ya viongozi wakuu wa South Africa kwenye mazishi ya Nelson Mandela, kwenye hotuba hizo kuna nchi zilitajwa km ndizo zilizotoa mchango mkuu wa upatikaniji au ufanikishaji wa South Africa kupata uhuru!

JAMBO LA KUSHANGAZA HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA WA SOUTH AFRICA KATI YA WALE WALIOTOA HOTUBA ALIYEITAJA TANZANIA KAMA NCHI MUHIMU ILIYOJITOLEA KILA HALI KUISADIA SOUTH AFRICA NA CHAMA CHA ANC KUPATA UHURU, NI KWANINI?
 
Megawatt B

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
259
195

Ni kweli Mandela hakuhudhuria mazishi ya Nyerere, nakumbuka taarifa zilisema kuwa anajisikia vibaya na atasononeka sana ukihudhuria mazishi ya Mwalimu. Hata hivyo,mara baada ya Mwalimu kuzikwa Mandela alienda Butiama (26/11/1999). Na nakumbuka uwanja wa Ndebele alipokelewa na waziri wa mambo ya nje Kipindi hicho Kikwete. Kama hivyo imejitokeza kwa mama Maria, afya yake haimruhusu kwenda kwenye pilika pilika za mazishi.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,863
1,250
Ndugu zangu watanzania, wale mliofuatilia hotuba ya viongozi wakuu wa South Africa kwenye mazishi ya Nelson Mandela, kwenye hotuba hizo kuna nchi zilitajwa km ndizo zilizotoa mchango mkuu wa upatikaniji au ufanikishaji wa South Africa kupata uhuru!

JAMBO LA KUSHANGAZA HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA WA SOUTH AFRICA KATI YA WALE WALIOTOA HOTUBA ALIYEITAJA TANZANIA KAMA NCHI MUHIMU ILIYOJITOLEA KILA HALI KUISADIA SOUTH AFRICA NA CHAMA CHA ANC KUPATA UHURU, NI KWANINI?

Jambo nililiandika hapa siku ile ile .Tanzania haiutajwa katika mchango huo .Pale palikuwa sehemu muhimu sana lakini hatukutajwa sasa tunapewa hadithi za pembeni kwamba JK alikuw anamba kwenye list .Kuwa list namba moja Obama alikuwa namba ngapi na kahutubia pale ?
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Kuna swali ambalo huwa ninajiuliza kila mara tochi inapoangaza yaliyokuwa mahusiano ya Mwl. Nyerere na Mandela.

Kwa nini Mandela hakuhudhuria mazishi au kwenye memorial service ya Mwl. Nyerere?.

Tumeona viongozi wengi wa mataifa mbali mbali, makubwa na madogo wakibadilisha ratiba zao ili kuhudhuria memorial service yake, lakini yeye ambaye viongozi wetu walikuwa wanatuaminisha na wameendelea kutuaminisha kuwa walikuwa karibu sana katika majukumu ya kiutendaji wa jamii na kifamilia, lakini hakuweza kurekebisha ratiba yake ili ahudhurie.

Kuhudhuria kwa Mama Graca ukiangalia kwa undani hukukufanyika kwa sababu alikuwa mke wa Mandela, bali kulifanyika kwa sababu aliyekuwa Mme wake Mama Graca (Samora Machel) alikuwa karibu sana na Mwl. Nyerere.

Samora Machel hakuwahi kukutana na Mandela na kwa maana hiyo, hata mahusiano aliyokuwa nayo na Mwl. Nyerere hawezi kuyafahamu kwa undani zaidi ya kuelezwa na Mama Graca.

Mzee Mandela baada ya kutoka Jela, alijikuta akikumbatiwa bila kufurukuta na watu wa nchi za Magharibi ambao walikuwa na maslahi makubwa South Africa kiasi kwamba akaanza hata kuwasahau wapigania uhuru wengine kama Mwl. Nyerere. Siyo ajabu hata wakati wa memorial service na mazishi vilimkuta akiwa kwenye nchi hizo na akaendelea kuwepo huko!.

Hata kitabu chake kinachoenda kwa jina la Long Walk to Freedom by Nelson Mandela (1994) pia kimewasahau na kuishia kudodosa dodosa tu.

Ama kweli, tenda wema uende zako.......

Mwl. Nyerere alitenda wema kwa walalahoi wa Afrika kusini na akaenda zake lakini makovu ya kiuchumi na kisiasa tuliyoyapata kwa kuisaidia Afrika Kusini bado tunayauguza mpaka leo.

Tunatofautiana mambo mengi sana na kukubaliana mambo machache lakini pia kwa hili la leo kwa kiasi kikubwa tunakubaliana

Graca aliwahi kuwa Mwalimu wa Shule za FRELIMO nchini Tanzania na ndipo alipokutana na Samora wakati akiwa kwenye harakati

Mandela aliyetoka Jela hakua Mandela aliyeshawishi kusaini Freedom Charter ya mwaka 1955.

Juju ameegemea katika mapungufu ya ANC kusimamia maslahi ya kiuchumi na kijamii katika kutunga ilani ya EFF.

Ndiyo maana hata majibu ya Gwede Matanshe (ANC Secretary General) ni ya kipuuzi.

Mandela hakufikia matarajio ya wengi pamoja na kubebwa na legacy ya upambanaji,sacrifice binafsi yeye na familia yake na pia reconciliation legacy.
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Sasa naomba katika Mjadala huu nishiriki kwa kucheza nafasi ya wakili wa Shetani.Nisihukumiwe baada ya mchezo huu!
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Ni kweli Mandela hakuhudhuria mazishi ya Nyerere, nakumbuka taarifa zilisema kuwa anajisikia vibaya na atasononeka sana ukihudhuria mazishi ya Mwalimu. Hata hivyo,mara baada ya Mwalimu kuzikwa Mandela alienda Butiama (26/11/1999). Na nakumbuka uwanja wa Ndebele alipokelewa na waziri wa mambo ya nje Kipindi hicho Kikwete. Kama hivyo imejitokeza kwa mama Maria, afya yake haimruhusu kwenda kwenye pilika pilika za mazishi.
Mkuu, usinunue hizi ngonjera za kisiasa. Angalia wewe mwenyewe kwa macho matatu.

Mandela wakati akiwa jela, alifiwa na Mama yake na Mwanae. Mbona aliomba ruhusa ili akawazike?. Kwa nini hakusema siendi kwa vile nitasononeka sana!. Itakuwa Rafiki wa kukutana barabarani na kwenye majukwaa ya kisiasa?.

Mbona aliweza pia kuhudhuria kwenye msiba ya mtoto wake wakati alikuwa hajiwezi vizuri hata kutembea?.

Ndiyo maana mara nyingi siwapendi wanasiasa kwa sababu kama hizi za kutufanya sisi ni kama wajinga fulani!.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013

Sababu ya kujisikia vibaya ni DHAIFU mno kwa sababu zifuatazo.

1. Mandela amewahi kuwa amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Africa Kusini. Kazi hiyo inahitaji ujasiri mkubwa. Mtu aliyeimudu kazi hiyo pamoja na kuvumilia jela miaka 27 hawezi kukosa ujasiri wa kuhudhuria mazishi ya rafiki.

2. Nyerere amefariki akiwa na umri wa miaka 77. Huu sio umri mdogo wa kufanya kifo chake kiwe habari ya kusononesha kiasi cha kushindwa kuvimilia kuwepo.

3. Je, Mandela aliumizwa zaidi kuliko watoto wa Nyerere na mama yao? Mbona wao waliudhuria mazishi ya Baba yao pamoja na uchungu walio nao.

4. Je, Mandela alimpenda Nyerere zaidi kuliko ndugu zake wote? Je, mazishi ya ndugu zake hakuwa akihudhuria?

Ninachoona ni kwamba Mandela alikuwa hataki mazishi ya Nyerere yawe triumph. Alijua uwepo wake utafanya mazishi hayo kupata coverage kubwa na akajiweka kando. Lengo ni kiogopa kutonesha vidonda vya "wazungu".

Nchi za magharibi zinailaumu Tanzania kwa kuvipa mafunzo vikundi vya ANC ambavyo according to wamagharibi vikundi hivyo ni vya kigaidi.
Mandela anaonekana alihofia kukumbushia historia hiyo. Kwa watu wa magharibi kilichofanywa na Tanzania pale Mazimbu Morogoro sio ushujaa ila ni ugaidi. Mandela anaonekana kukubaliana na wamagharibi kwenye hili. Anaona aibu kujiweka karibu na watu waliounga mkono "ugaidi" wake ili asiwaudhi "wakubwa".
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Huu ni upotoshoaji. Kuonyesha wanatambua umuhimu wa Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ataongea kwenye mazishi kijijini QUNU kutokana na ukaribu wa Tanzania na ANC na South Africa kwa ujumla.

Source: City Press News Paper (City Press - The home of City Press online)

Kuongea sio hoja. Marekani ilikuwa mshirika mkubwa wa makaburu lakini Rais wao Obama alipata fursa ya kuongea kwenye memorial.
 
Ben Saanane

Verified Member
Jan 18, 2007
14,594
2,000
Mkuu, usinunue hizi ngonjera za kisiasa. Angalia wewe mwenyewe kwa macho matatu.

Mandela wakati akiwa jela, alifiwa na Mama yake na Mwanae. Mbona aliomba ruhusa ili akawazike?. Kwa nini hakusema siendi kwa vile nitasononeka sana!. Itakuwa Rafiki wa kukutana barabarani na kwenye majukwaa ya kisiasa?.

Mbona aliweza pia kuhudhuria kwenye msiba ya mtoto wake wakati alikuwa hajiwezi vizuri hata kutembea?.

Ndiyo maana mara nyingi siwapendi wanasiasa kwa sababu kama hizi za kutufanya sisi ni kama wajinga fulani!.

Statement ya "Nitasononeka sana" ni rhetoric za kidiplomasia tu.Ni kiwango cha juu cha kubobea katika matamshi ya kidiplomasia yanayolenga pia kuwasaidia nchi wenyeji'Wafiwa' katika kurahisisha propaganda za kisiasa kwa mwelekeo wa kuaminisha umuhimu wa mhanga wa mauti na kuweka uwiano sahihi wa kulinda haiba ya mkosaji bila kuacha mashaka ya "kuwa na dhamira" au "kutokua na dhamira" ya dhati katika jambo mahsusi.
 
zinc

JF-Expert Member
May 24, 2013
1,388
2,000
Mandela alisema kwamba "nitazimia au kupoteza fahamu kabisa kama nitauona mwili wa marehemu mwalimu Nyerere kwenye jeneza", ambaye hapo awali alikuwa rafiki yake kipenzi nje ya SA. Hayo ndiyo niliyowahi kusikia kutoka kwa Marehemu Mandela akiwa hai
 
Bigaraone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
723
195
Mkuu, usinunue hizi ngonjera za kisiasa. Angalia wewe mwenyewe kwa macho matatu.

Mandela wakati akiwa jela, alifiwa na Mama yake na Mwanae. Mbona aliomba ruhusa ili akawazike?. Kwa nini hakusema siendi kwa vile nitasononeka sana!. Itakuwa Rafiki wa kukutana barabarani na kwenye majukwaa ya kisiasa?.

Mbona aliweza pia kuhudhuria kwenye msiba ya mtoto wake wakati alikuwa hajiwezi vizuri hata kutembea?.

Ndiyo maana mara nyingi siwapendi wanasiasa kwa sababu kama hizi za kutufanya sisi ni kama wajinga fulani!.Your inputs are indeed touchy. Kwenye siasa kuna mambo ya ajabu kwelikweli.Kuna upotoshaji wa hali ya juu. Yumkini Tanzania ya Mwalimu Nyerere ilifanya what can be called sacrificial martyrdom pale tulipotoa kile kidogo tulichokuwa nacho pamoja roho za wenzetu wa mipakakani waliokuwa wanauawa na mabomu ya makaburu na Wareno wa Msumbiji na Angola achilia mbali wanajeshi wetu waliokwenda kusaidia. Sasa kama ilivyokuwa huruka ya binadamu yawezekana South Africa are not rational na wanaangalia quantity kuliko quality. Inahitaji unyenyekevu kama aliofundisha Yesy Kristu alipochungulia katika sanduku la sadaka na kuwaona matajiri na nmafarisayo wakitoa sadaka kubwa lakini bibi kizee mjane akatoa senti ndogo. Huyu alionekana ametoa kubwa kwa maaana she offered the last she had in her possession. Wa South wakikosa shukrani iwe changamoto lakini tusife moyo katika kusaidia wavyonge kokote walipo katika uso wa dunia
 
kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,174
0
Unapozungumzia LEGACY Mw. Nyerere anayokuwa KUBWA mno, ililinganishwa na Mandela (Kwa mfano wa haraka nimeishi Malawi, Angola, Namibia, Botswana Lesotho na Msumbiji na hata kupita South Afrika, katika nchi hizo kujulikana tu kwangu kuwa ni Mtanzania nilikuwa napata ushirikiano mkubwa mno sababu kubwa wanalitaja jina la Nyerere ukiacha South).

Kilichopo ni kwamba Mandela baada ya kusaini ile dili na Frederik Willem de Klerk aliisahau kabisa Tanzania, cause tayari ilikuwa imeonekana kwa wakubwa kwamba inafundisha magaidi ambao ndio walikuwa wakimsaidia Mandela. Na ndio maana wakaamua kuwazawadia wote wawili tuzo ya Nobel.

All in all to me Mandela in nothing and I take him as a traitor compared to Nyerere na Kwame Nkurumah.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom