hakuna mzee amelipa price kubwa ndani ya ccm kama mzee SAMWEL CYGEYAMWISI LUSINDE MALECELA ....mtakumbuka amekatwa urais mara mbili ,mara ya kwanza akiwa na nguvu kubwa kabisa ndani ya chama karibu sawa na aliyokuwa nayo Lowassa ......2005
Mwaka 1995 pia alikatwa akiwa pia na ushawishi .
Kuna wakati alipatwa na mikasa ya kufiwa na watoto wake wa kiume na mmoja wa kike aliyekunywa sumu,akafiwa na mkewe etc .......Kati ya msiba uliowauma hata vijana wengi waliokuwapo mjini enzi hizo ni msiba wa IPYANA MALECELA ambaye alikuwa anaelekea kuwa mwenyekiti wa uvccm Taifa ....na wakora wakizuia asiingie kwa kuhofia kumpangia baba yake safu ya 2005.
Huyu ni malecela ambaye ...kuelekea 2005 mkutano mkuu ,mkewe mpya Anna Kilango alitekwa na maharamia kina HUSSEIN GOGO na kundi lake la vijana wakihuni kutoka Bagamoyo ...na kumfanya ukatili wa kila aina na kumpora mamilioni ya pesa ambayo walikuwa wanazuia zisifike dodoma kwenye mkutano mkuu ....jambo ambalo walifanikiwa na mgombea waliemtaka kupita
kimsingi naona hakuna mwanasiasa mmoja ndani ya ccm ambaye amelipa GHARAMA kubwa kama malecela ...anastahili tuzo ...kiasi sioni tena jambo la kumfanya ahame ...haya ya sasa ni madogo sana eti ya mkewe kufukuzwa kazi kwa aibu tena bila kosa la moja kwa moja ...na bintiye mpendwa kufukuzwa kazi kwa fedheha huku wasiokuwa na fani ya utafiti ndio wakiongoza propaganda hizo ..........nadhani huyu mzee ni mbuyu na hawezi kuyumba ...ni AYUBU wa ccm .