Familia ya Lissu yagoma ombi la Serikali, yasema hawataomba msaada huo wenye masharti

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,981
2,000
Ikija kwenye suala la PR Lissu anaigaragaza vibaya sana serikali.

Na si kwa sababu ya umahiri wake kwenye mambo hayo bali ni kwa sababu ya unforced errors za serikali.

Mystique ya Lissu imeongezeka sana baada ya jaribio kubuma na ataporudi nadhani nchi nzima itasimama!

Pia, sasa hivi hata 'street cred' imeongezeka. Mtu kutandikwa marisasi yote hayo na ukanusurika kifo...si jambo dogo hilo.

Na kwa sababu hiyo kwa watu wengi atakuwa ni a larger than life hero.

Sasa sijui mkulu kajiandaaje kwa hilo maana kuna kila kiashiria kwamba sasa Lissu atam - upstage mheshimiwa rais kwenye umaarufu.

Only time will tell...so we shall see.
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,372
2,000
Naona serikali ilitupa last card kujisafisha kwa kuipata imani ya familia ya Lissu na kuwapiku CHADEMA kisiasa.

Nadhani wangeamua kumtibu kwa moyo mmoja bila masharti wala bla bla nyingi wangeipata imani hiyo na kufanya wengi watilie shaka hoja za CHADEMA kuihusisha serikali na tuhuma za kutaka kumfisha Lissu. Serikali inahitaji wanamikakati bora zaidi kuliko ilio nao sasa.
Nimependa changamoto waliyopewa serikali (siri-kali) na familia ya Lissu kupitia Mwanasheria wa serikali ya kutaka wachunguzi (huru) wa nje wasaidie uchunguzi wa kuwasaka "watu wasiojulikana" ili mlolongo wa wahusika wa jinai ile wajulikane.

Serikali imewekwa kwenye kitimoto.
 

titimunda

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
7,588
2,000
Naona serikali ilitupa last card kujisafisha kwa kuipata imani ya familia ya Lissu na kuwapiku CHADEMA kisiasa.

Nadhani wangeamua kumtibu kwa moyo mmoja bila masharti wala bla bla nyingi wangeipata imani hiyo na kufanya wengi watilie shaka hoja za CHADEMA kuihusisha serikali na tuhuma za kutaka kumfisha Lissu. Serikali inahitaji wanamikakati bora zaidi kuliko ilio nao sasa.
Nchi inaongozwa na washamba wa siasa hii,wanshindwa hata kucheza karata zao vizuri.angekuwa mkwere saizi lisu yuko ulaya kwa pesa za serikali tena with no strings atached.tatizo umbumbu unawasumbua
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,224
2,000
Vipi kuhusu yule jamaa aliepigwa risasi tano na majambazi harafu kesho yake tu anaongea kama DJ wa redio uhuru! Yeye hazikuingia vizuri tumboni ?
Ndugu yangu, tumbo limeshamiri viungo (organs) nyingi mbali mbali zenye kazi tofauti tofauti katika uhai wa binadamu. Hoja si risasi kuingia vizuri tumboni bali hoja ni kiungo gani tumboni kimefumuliwa na hizo risasi. Mtu ambaye figo zake zote mbili zimefumuliwa kwa risasi hawezi kuwa sawa na yule ambaye bandama lake limefumuliwa kwa risasi au yule ambaye ni abdominal wall tu ndiyo imefumuliwa.
 

elitee

JF-Expert Member
May 15, 2017
328
500
I truly admire this man! "He is a true son of his father" Our heaven father will favor & heal him. Amen.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,120
2,000
Tunaomba baadae isilete shida, kama kweli lisu na familia yake wamekataa msaada basi Watanzania, tumewaelewa. Tunaiweka kwenye kumbukumbu.
Tuweke kwenye kumbukumbu pia kuwa

Kiongozi yeyote wa nchi hii kutoka bungeni Mahakamani au serikalini akiugua lazima aombe pesa kwa ya matibabu kwa waziri wa afya ..

Iwekwe hivyo maana Lissu si wa mwisho kuugua tutataka kuona barua zao.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,224
2,000
Mwenyekiti ameshasema taarifa zote kuhusiana na lissu atatoa yeye na wala si vinginevyo!
Huyu Return of Undertaker na wenziwe sijui kwa nini hawataki kufuata maagizo ya mwenyekiti wao? Au ni yale aliyoyaona Mzee Duni kuwa chama kile ni cha makambale, kila mmoja ana masharubu.

Leo gazeti la mwananchi limedai kumhoji mke wa Lissu kuhusu msaada wa serikali kugharimia tiba ya mme wake. Mrs Lissu akajibu hana comments kwa sasa. Undertaker anasema Tundu mwenyewe akiwa ICU amempigia simu mdogo wake akiwa kwenye kikao cha TLS Arusha kuwa hataki msaada huo wa kinafiki kutoka serikali.
 

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Jul 21, 2017
5,668
2,000
Aisee Lissu ni mtu strong sana. Nafkiri haijawahi kutokea. Lakin pia familia yake ipo kimkakati zaid kias kwamba pamoja jamaa ni mahututi (ICU) lkn joto lake lipo juu kama siku zote
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,743
2,000
*************************
ENGLISH:
Breaking news*

Tundu Lissu has phoned his brother Advocate Alute Mughwai and told him he will get back to the struggle for a free and democratic Tanzania.

He also instructed him to respond to Minister Ummy Mwalimu on behalf of the family that, the family will not request for treatment aid from the government for the same is an afterthought
and an entitlement that the patient deserves.

Alute has briefed the press in Arusha. More news to come.

*************************
KISWAHILI:

Habari mpya

Tundu Lissu amempigia simu kaka yake Alute Mughwai na kumwambia atarejea kupigani kupata Tanzania yenye demokrasia huru .

Pia amemuelekeza kwamba amjibu Waziri Ummy Mwalimu kwa niaba ya familia kwamba, familia haitaomba msaada wa matibabu kutoka serikalimi kwa sababu hilo ni wazo si tu "halina tija kwa sababu limeshatanguliwa na matukio halali mengine" bali hiyo ilikuwa ni huduma anayostahili kupewa mgonjwa.

Alute ametaarifu wanahabari mjini Arusha. Habari zaidi kufuata baadaye


NB:

Nimepata kigugumizi na neno "afterthought" ingawa ninalijua vizuri katika english najihisi kutotoa tafsiri nzuri naomba mmoja anisaidia kama nimelikosea.

MY TAKE:

Binafsi ninaamini hii english ni ya kisheria na inaweza kweli kutoka kwa Tundu Lissu. Ni mara chache sana usipokuwa mwanasheria ukatumia neno "the same" kama lilivyotumika kwenye hii message.

Hongera mliouliza tafsiri maana kwa kadiri maneno yalivyotumika hata ordinary english ungeweza usielewe mantiki kwa baadhi ya statements kama mimi ninavyojihisi kwamba sijatafsiri vizuri neno "afterthought"

Cc:

delako Ngoda95 minji Wervemarcel, Mwifwa
si jambo la KUFIKIRIA bali ni haki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom