Familia ya Lissu yagoma ombi la Serikali, yasema hawataomba msaada huo wenye masharti

Wapo watu wachache wenye mashetani na uzm wa watanzania kwao ni Msiba. Poleni sanaaaaa !!! Kwa TL Tutachanga tuuuu nyie vp ???
 
nitauza bata wangu wawili nichangie matibabu.kulamba miguu ya watu ni laana na aibu. get well soon Hon TAL
 
Mtu ambaye yuko kwenye critical condition (= edge of life) in ICU hawezi kuwaza mambo ya dunia hii. Jana tu mwenyekiti wa chadema alitutahadharisha kuwa tusisikilize taarifa zo zote isipokuwa zile atakazotoa yeye. Zingine zote si rasimu na ni za uwongo/ uzushi tu. Mtu ukiwa ICU huruhusiwi kuwa na simu wala kupokea au kupiga simu. Hivyo hayo maongezi ni ya kutunga, ni hewa. Mwacheni Lissu ampumzike ili aweze kupata quick recovery.
Vipi kuhusu yule jamaa aliepigwa risasi tano na majambazi harafu kesho yake tu anaongea kama DJ wa redio uhuru! Yeye hazikuingia vizuri tumboni ?
 

Heshima kwenu wakuu,

Familia ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, imesema haitaandika barua Serikalini ya Kuomba Tundu Lissu atibiwe na Serikali.

Kaka wa Tundu Lissu ambaye ni Msemaji wa Familia Alute Mghwai, amesema aliongea na Tundu Lissu. Kasema Tundu Lissu aliamwambia asiandike barua ya Kuomba Tundu Lissu atibiwe na Serikali baadala yake Lissu kasema atalizungumzia mwenyewe siku za hivi karibuni.

Lissu alimwambia Kaka yake kwamba kwa yeye kuwa mbunge anapaswa atibiwe na Serikali pale anapopata maladhi au tatizo la kiafya bila ya kuandika barua wala familia kuandika barua. Ni wajibu wa Serikali kumtibu na ni haki yake kutibiwa.

Kaka wa Lissu ameongeza kuwa, Wamemuandikia Barua mwanasheria mkuu wa Serikali tarehe 16/09/2017 kumueleza katika swala la Uchunguzi wa Lissu, hawana imani na vyombo husika, hivyo wameomba Waruhusu kutumia vyombo vya nje ili kufanikisha Uchunguzi wa kuwatambua watu waliohusika. Tunataka Uchunguzi huru kutoka nje ya nchi.

Vilevile ameongeza kuwa, Tundu Lissu anaendelea Vizuri.
 
Naona serikali ilitupa last card kujisafisha kwa kuipata imani ya familia ya Lissu na kuwapiku CHADEMA kisiasa.

Nadhani wangeamua kumtibu kwa moyo mmoja bila masharti wala bla bla nyingi wangeipata imani hiyo na kufanya wengi watilie shaka hoja za CHADEMA kuihusisha serikali na tuhuma za kutaka kumfisha Lissu. Serikali inahitaji wanamikakati bora zaidi kuliko ilio nao sasa.
 
Issue ya kutaka familia iandike barua ni manyanyaso. Huenda hata wangeandika, wangeishia kujibiwa tu kwa kupewa mlolongo mreeefu wa taratibu na kanuni "mrudisheni Muhimbili then doctors wetu bingwa wamchunguze na kumpa rufaa kama wataona kuna ulazima huo".

Yaani Mbunge anataka kuwa treated kama wale kinamama hohehahe wanaojifungua watoto watano kwa mkupuo then wanaambiwa warushe maombi huku na kule. Kamati husika ya Bunge ijitafakari na ikibidi ifanye mchakato wa kureview procedures za kutoa msaada wa matibabu kwa dharura kama hizi ili huko mbele ya safari tusijikute kwa sintofahamu kama hii tena.
 
Back
Top Bottom