Familia ya Gwajima imemkosea Waziri wa Afya, kiungwana wamtafute wamuombe radhi

Mbona mnaleta double standard inawasaidia Nini mbona issue ya Gwaji girl kuleta masuala ya mkono wa baunsa hambwabwaji hivyo
 
That's personal..!😄😄 When you outside to fight don't wear your best trousers 😄😄
Waziri mwenye dhamana hakua na sababu ya kutumia mipasho kwenye kuhamasisha hiyo chanjo yeye angetumia wataalamu wake tu kumjibu gwajiboi
 
Kama hunipendi mimi utapata tabu sana mwaka huu! Tandu watakuwa wanatembea usoni mwako wakati unapofumba macho kutaka kulala, na utakosa usingizi mwaka mzima! Afadhali ubadilishe mtazamo uwe mtu positive ambaye haendeshwi na hisia.
So mkuu ni lazima kukupenda?
 
Kwa taratibu za kisukuma, Mwanamke yeyote aliyeolewa kwenye familia "NG'WINGA = mtu wa kuondoka wakati wowote (mpitaji)" hawezi kuombwa msamaha hadharani na mwanafamilia yeyote mwenye umri au hadhi kubwa kuliko ya mmewe katika familia husika kwa kosa lolote. Ukiolewa usukumani hiyo 50-50 sahau.
 
Wazee wa zamani walisema upumbavu/wapumbavu usipewe/wasipewe nafasi ya kuzungumziwa/kuzungumza katika jamii.
 
Apana, chanzo Cha tatizo Ni waziri mwenyewe kwa kuleta personal issues kwenye mambo ya korona, alitakiwa amjibu askofu kwa mambo ya korona na si kuleta mambo ya mkono wa baunsa. Nk.
Mm niko upande wako nayaona haya malumbano ya Gwajima waziri na Askofu kwa mtazamo tofauti ya kwamba kila mmoja ana haki kwa upande wake ,Askofu ana haki ya kuchambua mambo ya chanjo na kujiridhisha kabla kutokana na Imani yake, achilia mbali the other side of him km political figure na Waziri ana haki ya kutetea kazi yake km waziri mwenye dhamana na muhusika mkuu wa kusimamia zoezi zima la chanjo!
Sasa tuje kwenye mapungufu ya wote wawili kwa maono na mtazamo wangu
1.Askofu akijua kabisa kwamba ni Mbunge tena wa chama hicho chenye serikali iliyoleta hiyo chanjo anasimama na kuipinga hadhalani kinyume na kiapo chake cha kutetea maslahi ya chama na Serikali yake!
2.Askofu akijua kuwa si mwana sayansi amekuwa akiichambua hii chanjo na kuwaaminisha wauumini na jamii kwa ujumla kwamba chanjo haifai bila kuwa proof za kisayansi
3.Askofu kwa kujua au kutokujua kwamba yeye ni maarufu na ana wafuasi wengi ametumia platform ya kanisa lake kutoa ya1nayoonekana kuwa maoni yake binafsi kuhusu chanjo huku yakiathiri maamuzi ya Umati mkubwa wa umma wa Watanzania.

Kwa upande wa Waziri
1.Tofauti ya misimamo yake miezi 6 iliyopita na sasa inafanya kazi yake kuwa ngumu na kuonekana kwamba hana msimamo thabiti ktk maamuzi yake
2.Kuingiza mambo ya Familia au personal issues ktk mamno ya siasa kunamharibia hakupaswa kum attack Askofu kwenye mambo yake private katika issue ya chanjo itapelekea kuonekana kuwa ana chuki na yeye sio kikazi.
3.Kuweka Jokes nyingi (kutest mitambo)kwenye mambo serious kunafanya Maadui zake kumtoa kwenye Reli na kumfanya asionekane kuwa makini though ni mmoja kati ya watendaji makini sana.
All in all ni ngumu sana kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja yaani kwa Askofu kuwa pia Mwanasiasa Bible always don't lie iliposema ya Kaisari apewe Kaisari na ya Mungu apewe Mungu hii ndio Challenge Askofu anayo face hapa ,inshort siasa is all about lies na Dini ni Truth kwa kwenda mbele!
 
Umesahau kuwa ni ASKOFU GWAJIMA ndiye aliyeanza UBAYA wa kuwaombea LAANA YA KUFA MADAKTARI WOTE WATAKAOHIMIZA CHANJO ?!!!!

Mh.Waziri D.Gwajima naye ni DAKTARI.....
 
Umesahau kuwa ni ASKOFU GWAJIMA ndiye aliyeanza UBAYA wa kuwaombea LAANA YA KUFA MADAKTARI WOTE WATAKAOHIMIZA CHANJO ?!!!!

Mh.Waziri D.Gwajima naye ni DAKTARI.....
Ukivuliwa nguo na kichaa na wewe ukaanza kumkimbiza, watu timamu watakushangaa wewe.

Msimtetee Dorothy na acha tu waendelee kuparurana
 
Ukivuliwa nguo na kichaa na wewe ukaanza kumkimbiza, watu timamu watakushangaa wewe.

Msimtetee Dorothy na acha tu waendelee kuparurana
Simtetei mtu....

Naongelea mambo yalivyoanza....kwa hiyo mchungaji Gwajima hakuuanza mjadala na kupinga chanjo na KUWALAANI madaktari watakaohimiza chanjo?!!!
 
sasa kwa nini unichukie basi?
Kukupenda/kukubaliana na mitazamo yako ni hiyari yangu na pia naweza nisikupende/kutokubaliana na wewe na bado nikawa sahihi, mimi nimeamua kutokubalia na wewe, sidhani kama nimekosea
 
Umejalibu kumuuliza huyo shemejie kama alitumia busara badala ya kuzungumzia upingaji wa chanjo wa askofu yeye akaingilia mambo ambayo yanaleta udhalilishaji kwa kusema askof kakutwa na mlembo na mambo ya kutaka ubunge pia kuhusu amina chifupa?
Je yeye hapo kama mwanafamilia alitumia busara?

Je hayo yalikuwa yanahusu chanjo au yalilenga kumdhalilisha gwajima?

Sifulahii tabia hizo za gwajiboy kama mnavyomuita ila waziri kama mke wa mdogo wake angetumia maneno ya hekima kupingana na shemejie ukizingatia baada ya uwazili na ubunge bado watatakiwa kuishi kama familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…