Familia ya CDF Mwamunyange: Yupo nje ya nchi kwa majukumu ya Kitaifa

Huyu ni kaka tu, kwanini mwandishi hakuenda kumhoji mke wa Mwamnyange Monica Lyanda? Inashangaza kidogo!! Mbona Mwmnyange yuko kimya sana huko aliko? Hajapata habari kuwa kuna habari mkanganyiko huku na watanzania wanataka kujua ukweli wa mambo? Anyway time will tell and the truth will be unveiled soon.
View attachment 298881

Familia ya Mkuu wa Majeshi General Davis Mwamunyange imetoa kauli mara baada ya sintofahamu inayoendelea Mitandaoni Kuhusu Mkuu huyo wa Majeshi, Familia ya CDF Mwamunyange:

Yupo nje ya nchi kwa majukumu ya Kitaifa. Akizungumza kwa Niaba ya Familia Kaka Yake Davis Mwamunyange amethibitisha Mdogo wake anaendelea na Majukumu yake yupo Nje ya Nchi na anatarajiwa Kurudi Nchini siku za Karibuni.

Ni baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni juu ya kulishwa sumu kwa mkuu huyo.

Familia imesema anaendelea vizuri na yupo nje ya nchi kwa majukumu ya kitaifa.
 
Tungeamini kama wangesema kutoka nyumbani kwake yaani mke na watoto,pili wangesema kaenda nchi gani na anarudi lini.Pia akangeweza kukanusha ata kwa video call.Wameongeza maswali hawa.
 
Hamuiamini serikali, sasa Familia yake imesema General yuko salama na bado yupo nje ya nchi kikazi.
Kaka yake Kapteni Aden Mwamunyange na Dada yake wamesema huo uzushi unawaumiza kama family .

Source: ITV
Mmh, Kampteni Polisi,?
 
View attachment 298881

Familia ya Mkuu wa Majeshi General Davis Mwamunyange imetoa kauli mara baada ya sintofahamu inayoendelea Mitandaoni Kuhusu Mkuu huyo wa Majeshi, Familia ya CDF Mwamunyange:

Yupo nje ya nchi kwa majukumu ya Kitaifa. Akizungumza kwa Niaba ya Familia Kaka Yake Davis Mwamunyange amethibitisha Mdogo wake anaendelea na Majukumu yake yupo Nje ya Nchi na anatarajiwa Kurudi Nchini siku za Karibuni.

Ni baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni juu ya kulishwa sumu kwa mkuu huyo.

Familia imesema anaendelea vizuri na yupo nje ya nchi kwa majukumu ya kitaifa.

Anaendelea vizuri na nini? Yawezekana tumewekewa picha ya zamani ya kaka MTU! Kwa nini asijitokeze mwenyewe live!!! Kwa nini hili linaonekana ni gumu? Hatukatai yeye kuwa nje ya nchi, tunataka tumwone live akiisemea afya yake mwenyewe!
 
Yule mama akiwa anahojiwa kajibu kwa hasira na ghadhabu eti anaetaka kumuona mwamunyange huyo ni nani maana hawajibiki kwake anawajibika kwa rais.

Huyo mama sijuo ndio dada yake ana uwezo na uelewa mdogo sana, anashindwa kuelewa mwamunyange ni public citizen,anawajibika kwa watanzania maana ndio wanamlipa mshahara,anachukulia ukaka yake na sio ukuu wa jeshi.

Cdf ni public citizen, watanzania wana haki wa kujua yuko wapi na anafanya nini, watu hawaulizii mwamunyange kaka yake, ukaka ni nyumbani, hapa wanaulizia mwamunyange kama cdf.

ww ndio huna uelewa. Unaambiwa lakn bado huelewi unataka umuone. Ww umuone kama nan?
Kwan ziara zote anazofanya sku zote mmewahi kuhoji?

Msilete mambo ya kisiasa kwenye jeshi. Kwahyo kama ameenda kwa mambo ya siri ya kijeshi nayo mnataka mjue nyie vimbweka tu.

Achen wanaume wafanye kazi nyie kaendeleen kukata viuno huko
 
Sintofahamu bado inaendelea kuhusu mkuu huyu wa majeshi najiuliza swali sipati jibu nikwanini siyo mke wake au watoto wake ndo waliokanusha taarifa hiyo?waliokanusha habari hiyo ni kaka yake mwamunyange na dada yao??bado hawajazima kiu za watanzania wanaotaka kujuwa alipo mkuu wetu wa majeshi
Huyo kaka yao ndiye wamemchagua kuwa msemaji wa familia. Sasa wewe unataka kuwabadilishia utaratibu wao wa familia? Wewe ni nani?

Inawezekana yupo kwenye shughuli nyeti confidential za kijeshi. Tuvute subira!
 
sijui na wala sina uhakika kama yupo hai au hayupo hai, am stick CLUELESS!
 
Nimepewa na Mungu sio Mungi.
Kweli mimi ni mtu mzima na ni ukawa.
Bado hujanijibu, anayekuwa in charge CDF asipokuwepo ni nani?

Mbowe asipokuwepo chadema in-charge anakuwa nani? Nadhani jamii forums imeingiliwa kuna watu humu ndani nadhani umri wao pengine ni chini ya miaka 12. Maswali gani haya wanauliza?Upo wakati nilitaka kujitoa JF kwa upuuzoi kama huu wa hoja na maswali yasiyo na kichwa wala mguu. Hivi ni swali gani hili la kuuliza kuwa eti asipokuwepo CDF ni nani anakuwa in-charge. Hivi asipokuwepo rais wa nchi ni nani in-charge. Asipokuwepo mkuu wa taasisi ni nani in-charge. Ni maswali ya ajabu kabisa. Hawa UKAWA wanaleta utamaduni mpya katika nchi hii. Ni vema wadhibitiwe mapema. Hawajui hata taasisi zinaendeshwaje. Hawasomi vitabu wala journals. kazi yao ni kupinga each and everything. Wao kutoheshimu mamlaka ndiyo itikadi na sera. Rubbish. Hatuwezi kuwa na nchi ya aina hii, ya watu wasiofikiri. Kwao kufagia barabara ili apite LOWASSA ndiyo mtaji. Kujikusanya uwanjani kwa mamia na maelfu eti ndio mafuriko na ndio ushindi. Umati ule wa magufuli eti ni wa kupikwa na ule wa LOWASSA ndio uhalisia. Hatuwezi kuwa na taifa la watu wasiofikiri. Kuzomea barabarani msafara wa magufuli au samia eti ndio watanzania wameamua kukataa CCM. Yaani wahuni 300 wamekusanywa wajipange barabarani kumzomea magufuli eti kwao ndi watanzania hawaitaki CCM. Wamefunikwa na illussions na emotions. Niliwahi kumuuliza kijana mmoja aliyeahi kutumia madawa na sasa ameacha kutumia madawa hayo ya kulevya kwamba wakati anatumia madawa hayo alikuwa anajisikiaje. Jibu lake lilikuwa ni kuwa alikuwa anajiona kuwa yuko pamoja na Rais George Bush wa Marekani (wakati huo) wakipanga mipango ya namna ya kuongoza dunia. ILLUSIONS.Hao ndio UKAWA, wana ndoto a ajabu.
 
Ni sahihi kabisa kabisa,Jeshi haliongozwi na mambo ya kuzua zua hovyo,hajitokezi ataendelea na ratiba zake kama kawaida,afanyapo kazi zake haweki gari la matangazo kuzunguka mitaani kualika watu,kama hutaki hakuna atakayekulazimisha kwani hupunguzi chochote.

Watu wanavopenda kuonyeshwa kwenye tv wakiwa nje..hatari..!Mim nakubali kama tu he went for holday kabla ya kustaafu .
 
Sitashangaa kama mkuu atajitokeza na raia wakasema "sio mwenyewe ni DUPLICATE"..Kwani kusubiri kuna athari gani?.Tushaambiwa yupo nje ya nchi kwenye ziara ya kikazi na atarudi baada ya siku kadhaa,Tuwe na subira.
 
sijui na wala sina uhakika kama yupo hai au hayupo hai, am stick CLUELESS!

hutojua na utaendelea kutojua tu. Kwasababu yule sio mamaako wala babaako. Na nafasi yako ndan ya nchi hii ni sawa na chawa tu. Sasa chawa anaumuhimu gani wa kujua mstakabali wa taifa hili?
 
View attachment 298881

Familia ya Mkuu wa Majeshi General Davis Mwamunyange imetoa kauli mara baada ya sintofahamu inayoendelea Mitandaoni Kuhusu Mkuu huyo wa Majeshi, Familia ya CDF Mwamunyange:

Yupo nje ya nchi kwa majukumu ya Kitaifa. Akizungumza kwa Niaba ya Familia Kaka Yake Davis Mwamunyange amethibitisha Mdogo wake anaendelea na Majukumu yake yupo Nje ya Nchi na anatarajiwa Kurudi Nchini siku za Karibuni.

Ni baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni juu ya kulishwa sumu kwa mkuu huyo.

Familia imesema anaendelea vizuri na yupo nje ya nchi kwa majukumu ya kitaifa.
sawa.akirudi mtujulishe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom