Familia Wanavunja Chungu

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Arusha sasa hivi ukitembea mjini kwenye kuta utakuta matangazo yanasema kuanzia tarehe 4/5/2011 siku ya tangazo hilo lilipowekwa hadi kufikia siku 60 mtu au watu au vikundi vilivyojihusisha kwa njia moja au nyingine kumsingizia au kumtuhumu kijana wao kwa ile kesi iliyokua inamkabili mfanyabiashara maarufu wa mawe aina ya Tanzanite jijini Arusha mwenye asili ya Kimeru ambaye alituhumiwa kwa kesi ya kutmia silaha na unyang'anyi na akakaa jela kwa muda kama wa miaka 5 hivi lakini mahakama ikamuachia baada ya kukata rufaa na akashinda kesi hiyo. Sasa familia ya mfanyabiashara huyo imejiandaa kuvunja chungu kwa yeyote aliyejihusisha kwa kumsingizia kijana wao! jamani hizi ndizo habari nyepesinyepesi na mseto kutoka jijini Arusha nawatakia jumapili njema.
 
khaaa hivi totolako dokozi af unavunja vyungu!?wampeleke aombewe jamani!hayo madudu nasikiaga yanaanzia na wewe mwenyewe
kama mwizi kweli!:tonguez:
 
Hiyo familia inaamini uchawi kuliko kitu kingine chochote, mtu amesha achiwa si walitakiwa kumshukuru mungu tu, sasa hayo mengine ya nini!!
 
Wacha wavunje kama kweli Jungu lipo na alionewa,Matajiri hapo wanawaonea sana maskini,wengi wamefungwa bila sababu.
 
Sasa ndio napata picha halisi ya kabila la Wameru!
 
Hiyo familia inaamini uchawi kuliko kitu kingine chochote, mtu amesha achiwa si walitakiwa kumshukuru mungu tu, sasa hayo mengine ya nini!!

Huyu jamaa nakumbuka alihojiwa na gazeti moja akaulizwa atachukua hatua gani kwa wale waliomsingizia akasema yote anamuachia Mungu na sadaka kubwa kanisani akatoa yeye na familia yake sasa sijui hiki chungu ni cha nini!
 
chungu ni tamaduni ya waarusha wameru wanaiga tu ila chungu na yenyewe ni two way traffic ka hakusingiziwa ni kweli chungu itarudi kwao na itawamaliza. Hilo tangazo lina muhuri wa serikali ya mtaa? Sababu lazima lipitishwe na serikali ya mtaa au kijiji bila hivo chngu haivunjwi, ila kwa utafiti wangu nimekuja gundua kuwa wengi huishia matangazo tu ili kutishia na wengine hupata mali zao, kupasua chungu si mchezo ka ni wizi na kuna mtu au watu ktk ukoo unaopasua chungu waliconspire ktk wizi chungu hurudi ktk ukoo huo tena na kuadhibu vibaya. Nafkiri na wao wanapiga biti kwa malengo fulani si unajua na maneno yako yanavyokuwa. Alioona, aliosikia hakusema, alioshiriki kwa namna yeyote ile, aliomsaidia ktk kutunga na kupanga uongo afu wanamalizia chungu impate. Sa katika woote hao utasema hamna mtu wa ukoo huo aliehusika kivyovyote? hao hawavunji hawawezi thubutu kujiadhibu wanatishia hesabu hizo siku afu fuatilia uone ka wamevunja chungu utaniambia, kwa sasa hicho kitu ni vigumu sababu hatujuani saana ktk ukoo na ikiwarudi ktk ukoo inaua mbaya kabisa
 
Hivi haya mamabo bado yapo?? hala fu mikoa ya kaskazini yameshamiri sana na watu wanaamini kuwa ukivunjiwa chungu wewe na familia yako wote mnaperish kwa vifo vya ajabu ajabu. Kazi iko kukomboa kizazi kijacho na ushirikina.
 
Hivi haya mamabo bado yapo?? hala fu mikoa ya kaskazini yameshamiri sana na watu wanaamini kuwa ukivunjiwa chungu wewe na familia yako wote mnaperish kwa vifo vya ajabu ajabu. Kazi iko kukomboa kizazi kijacho na ushirikina.

Yapo na yana impact vibaya sana yani ka mkisikia chungu kinavunjwa na unajua kuna ndugu yako anhusika ni bora mkareconcile mapema na ikishavunjwa kuipoza ni gharama sana though inaweza kupozwa na si lazima mfe mnaweza mkawa katika ukoo wenu hamfanikiwi, hamzai au wanazaliwa watoto wanakufa au ndoa hazidumu, au watoto wanazaliwa afu wanakufa wakiwa ktk certain age au mnakufa kwa ajali za ajabuajabu yaani chaos na uharibifu ndani ya ukoo afu victim anakuwa wa mwisho ili apate muda wa kutafakari na kureconcile
 
Back
Top Bottom