kati ya vitu ambavyo wanasiasa mnakosea ila nyinyi hamujui ni suala la bodaboda,
yaani kwa kuwa wahanga wa matendo ya bodaboda hawana sehemu ya kukutania na kupaza sauti, basi nyinyi mnakomalia hapo hapo. ukweli ni kwamba watu wanachukizwa sana sana na mwenendo wa bodaboda na bajaji barabarni, lakini kwa kuwa wao wana vijiwe na ni rahisi kukusanyika na kupiga kelele mnadhani maumivu wanayo wao tu. sio siri kati ya vitu ambavyo sisi wananchi vinatuonyesha ubinafsi wa mwansiasa mbele ya kura, ni kutetea bodaboda na bajaji.
watu wanalia, watu wanakufa , watu wanpoteza viungo, watu wanharibiwa magari yao, lakini hawa watu hawana jukwaa la pamoja la kutoa vilio vyao. sasa nyinyi wanasiasa bila aibu mnadhani watu wanawafurahia kutetea bodaboda , kumbe watu rohoni wanumia sana , hasa wahanga.
sisi hatusemi zitungwe sheri mahsusi ya bodaboda pekee,, la hasha, sheria zipo , ziiipo !!! zisimamiwe tu !! tatizo ni nyinyi wansiasa, MAADHALI bodaboda wao wana vijiwe na wahanga wa bodaboda HAWANA VIJIWE, basi mnaegemea kwa bodaboda.
mkuu wa mkoa wa mbeya aligongwa na bajaji kweye kivuko cha waenda kwa miguu, yote haya hamuoni.
si jambo la kushangaza kuona bodaboda anatoka sehemu moja anakwenda sehemu nyingine mita 150, lakini spidi atakayokwenda nayo, akikutana na mtu anamuua, lakini hawajali.
kuna mfano alitoa mhe. Spika , kwamba huko ASIA , akari wamepewa viboko ili kudhibiti bodaboda , akapendekeza na hapa iwe hivyo, sijui iliishia wapi.