chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,747
- 26,004
Ikiwa leo ni fainali ya mashindano haya. Washiriki wapo 6, anahitajika mshindi mmoja atakayeibuka na kitita cha shilingi milioni 50 Usiku huu.
==============
Mchuano umeanza, ushindani mkali sana .
Wapo washiriki sita, wanahitajika watano waweze kuingia top 5.
Kila mshiriki ataimba wimbo mmoja ili mchujo upite wabakie watano.
=================
- Waimbaji wote sita mpaka sasa wameshaimba nyimbo mojamoja. Majaji wanachuja majina sita yapatikane matano.
- Kampuni ya Huawei kupitia wawakilishi wake wanagawa zawadi ya simu kwa washiriki wote sita.
TOP 5:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia 5 bora;
1.Kayumba Juma
2.Angel Marry Kato
3.Nasib Fenabo
4.Frida Amani
5.Kevin Gerson
- Mshiriki aliyeshindwa kufuzu ni Jackline, anatoka katika mashindano.
==================
MC wa BSS, Ceasar Daniel azua gumzo!
===========Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mtangazaji muongozaji wa Bongo Star Search Caesar Daniel amekuja na Msemo wa #HapaKaziTu.
Hali imebadilika ghafla ukumbi ukalipuka mabadiliko, huku wahdhuriaji wakionesha vidole viwili kuashiria alama ya chama cha siasa na wengine wakizungusha mikono kuonesha Mabadilikoooooo..
Kazi kweli kweli!
TOP 3:
- Wafuatao wamechaguliwa kuingia kwenye 3 bora;
1. Nasib Fenabo
2. Frida Amani
3. Kayumba Juma
- Walioshindwa kuingia kwenye awamu hii ni Kevin Gerson na Angel Marry Kato.
===============
TOP 2:
- Waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia kwenye 2 bora ni;
1. Kayumba Juma
2. Nasib Fenabo..
- Burudani zinaendelea kabla ya kuingia kwenye awamu ya mwisho kumpata Bongo Super Star - 2015
- Jukwaani anapanda Christian Bella na Malaika Band.
- Si mchezo! Show anayoifanya Bella inamfanya kutuzwa pesa nyingi mno.. Amekonga nyoyo za waliohudhuria hapa!
===========
- Na sasa ni wakati wa msanii Runtown kutoka Nigeria kutumbuiza. Anapanda na dancers wake jukwaani.
Kumbuka: Huyu ndiye msanii wa mwisho 'kupafomu' kabla ya kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho kumpata mshindi wa BSS 2015.
===========================
Naam, na sasa ule muda uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu umewadia!
- Chief Judge, Madam Rittah amepanda jukwaani kuungana na washereheshaji Caesar Daniel na Penny kumtangaza Mshindi. Je, ni Kayumba au Fonabo?
Madam Rittah: Kwa kweli najisikia faraja sana kufikia hatua hii. Napenda kutoa shukrani kwa tulioshirikiana kulifanikisha hili (anataja timu ya BSS, Majaji wenza, Wadhamini na wadau mbalimbali).
- Na Mshindi wa BSS 2015 (Season 8) ni.....
MWISHO!