ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 15,774
- 35,994
CAF wamewakubalia Simba ombi lao na Sasa Finali itapigwa Kwa Mkapa tarehe 25 May, 2025
JamiiCheck imefuatilia Taarifa hii na kubaini kuwa si ya Kweli. Soma hapa
JamiiCheck imefuatilia Taarifa hii na kubaini kuwa si ya Kweli. Soma hapa
Uhalisia wa madai haya
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebainisha nakala hiyo ya barua haijachapishwa na chanzo chochote cha kuaminika ama CAF wenyewe.
Aidha klabu ya Simba ambayo ndiyo inayoonekana kuandikiwa barua hiyo haijaandika chochote wala kuchapisha barua hiyo katika kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii. Aidha kurasa za mitandao ya mashindano ya Total energies shirikisho na klabu bingwa barani Afrika imekanusha kuhusika na barua hiyo.