Faida za kutosheka na kuridhika katika maisha

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,921
Reaction score
3,249
Moja kati ya ushauri ambao walimu wengi wa kiimani wamekuwa wakituhamasisha ni kuwa "Kutosheka - ni utajiri mkubwa kuliko aina yoyote ya utajiri".​

​

​

​

gratitudes.jpg
​

​

​

​
Mtu yoyote anaweza kuidumisha hali ya kutosheka. Kama mtu akiuliza kwa nini hatuna furaha katika maisha yetu ingawa vitu tulivyonavyo ni zaidi ya mahitaji yetu, ni njia gani sahihi ya kumjibu? Jibu sahihi ni kwa sababu hatutosheki. Kama tungetosheka, tusingesema kwamba hiki au kile ni pungufu. Hatuwezi kutosheka kwa ajili kuna upinzania kati ya hamu zetu za kibinafsi ambazo hazina kikomo na sheria ya kutodumu kwa vitu (kukubali ukweli kuwa hakuna kinachodumu duniani).

Mtu tajiri haina maana kwamba anacho kila kitu, mtu tajiri naye pia kila wakati anahofia usalama wake. Bado naye ana majukumu ya kulinda woga wake. Bado naye atatawaliwa na fikra za woga na wasiwasi, akifikiria kwamba watu wanamsubiri kumdhulumu. Tajiri hawezi kutoka nje bila usalama, hawezi hata kulala mlango wazi na uhuru mwingine hana. Utaona wote masikini na tajiri bado wanatafuta na kutorishika na walichonacho. Masikini anategemea tajiri ana raha na akiwa tajiri anaanza kuwa na kazi ya kulinda alichokipata na mwishowe maisha yake yanaisha mwisho wake unafika na anaacha kila kitu cha kifizikia alichokuwa anakimiliki.

Mtu aliyetosheka na hali yake ndiye tajiri wa kweli. Mwingine anasema ametosheka na kiwango alichopata kwake na kwa familia yake, na kinachozidi anamsaidia mwanadamu mwingine naye aweze kuishi salama. Hebu pata picha ya maisha hayo ulimwengu ungekuwaje. Watu wasipoamua kuzidi tamaa za misingi na kujiwekea tamaa zao wenyewe zisizo za msingi.

Maisha ya kuridhika yanampa mtu matumaini na kumpa uwezo wa kushukuru kwa kila jambo. Unaposhukuru kwa kila jambo unakaribisha mambo ambayo utashukuru zaidi. The universe inapenda shukrani. Unaposhukuru zaidi unazidi kupata vya kushukuru zaidi. Hivyo wewe kazi yako ni kuhsukuru na kupata kila cha kushukuru.

​

Gratitude21.jpg
​

​
 
Ni kazi kweli kupata mtu wa kutosheka ulimwengu wa saivi, binadanu hata umpe bonde la dhahabu ataanza kutaka na jingine!

Hebu tumuangalie Tajiri wetu Bahresa mpaka leo utaamini kuwa bado hajatoka kimaisha?

Anahangaika huku na kule anatamani hata wauza vitumbua ile biashara wamuachie yeye.

Huu ni mfano upo wazi sana.
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu. Lakini mwisho wa yote kifo kinatufundisha kuwa all material things are not belong to us. Ila matendo yetu ndiyo ya muhimu na nafsi zetu. Watu wanaangaika kuitafuta furaha lakini hawajajua furaha ni nini bali wanajitengenezea furaha yao na kuiamini. Lakini furaha yao haidumu milele.

Kauli hii haimaanishi kuwa na vingi sio muhimu, bali namaanisha kuwa na ambacho umeridhika nacho ni muhimu.
 
Kuna vitu viwili muhimu sana kwenye maisha ya binadamu ambavyo ndio huleta furaha au mgandamizo wa mawazo, hizi elimu zote za utambuzi, tafakuri jadidi nk ni kwasababu ya hivi vitu viwili ego/tamaa, kutamani na craving/ hamu ya kumiliki iliyopiliza(uchoyo)
Kila mtu anatamani kumiliki vitu vingi vizuri pamoja na pesa nyingi(ego), akishamiliki hataki vimtoke na atataka zaidi na zaidi (craving) huku wakati wote akiwa na wasiwasi wa hiki kikipotea/kikiharibika itakuwaje (mateso)
Lakini ukiangalia kiuhalisia hakuna tunachomiliki milele tunaishi katika dunia ya mapito(impermanence) hakuna kidumucho milele, ukishaielewa na kuikubali hii phenomenon basi utaishi maisha ya raha na na yasiyo na stress kwakuwa tayari utakuwa umevuka na kuvunja ile mipaka ya kutamani na kumiliki
 
'The universe inapenda shukrani', sikuwahi jua juu ya hili au lugha ndio imenitatiza! hapa universe inatendaje kazi kurejesha shukrani? Apollo
 
Kuna vitu viwili muhimu sana kwenye maisha ya binadamu ambavyo ndio huleta furaha au mgandamizo wa mawazo, hizi elimu zote za utambuzi, tafakuri jadidi nk ni kwasababu ya hivi vitu viwili ego/tamaa, kutamani na craving/ hamu ya kumiliki iliyopiliza(uchoyo)
Kila mtu anatamani kumiliki vitu vingi vizuri pamoja na pesa nyingi(ego), akishamiliki hataki vimtoke na atataka zaidi na zaidi (craving) huku wakati wote akiwa na wasiwasi wa hiki kikipotea/kikiharibika itakuwaje (mateso)
Lakini ukiangalia kiuhalisia hakuna tunachomiliki milele tunaishi katika dunia ya mapito(impermanence) hakuna kidumucho milele, ukishaielewa na kuikubali hii phenomenon basi utaishi maisha ya raha na na yasiyo na stress kwakuwa tayari utakuwa umevuka na kuvunja ile mipaka ya kutamani na kumiliki

dawa mojawapo ya tamaa ni kukinai kitu kile unajua huwezi kukipata hii ni bonge ya kulipiza kisasi cha tamaa,,haha haha haha ishu sasa ni nani yupo tayari kukinai mabilioni ya fedha (justasking)!!
 
Yeah ni kukinzana na kanuni za kawaida za maisha kwakuwa kwa upande mwingine unaambiwa don't stop till you get enough..! Na sky is the limit...!
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu. Lakini mwisho wa yote kifo kinatufundisha kuwa all material things are not belong to us. Ila matendo yetu ndiyo ya muhimu na nafsi zetu. Watu wanaangaika kuitafuta furaha lakini hawajajua furaha ni nini bali wanajitengenezea furaha yao na kuiamini. Lakini furaha yao haidumu milele.

Kauli hii haimaanishi kuwa na vingi sio muhimu, bali namaanisha kuwa na ambacho umeridhika nacho ni muhimu.

ujue umeongea kitu kikubwa sana wewe mtu ambcho sidhani kma wewe unakielewa
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu. Lakini mwisho wa yote kifo kinatufundisha kuwa all material things are not belong to us. Ila matendo yetu ndiyo ya muhimu na nafsi zetu. Watu wanaangaika kuitafuta furaha lakini hawajajua furaha ni nini bali wanajitengenezea furaha yao na kuiamini. Lakini furaha yao haidumu milele.

Kauli hii haimaanishi kuwa na vingi sio muhimu, bali namaanisha kuwa na ambacho umeridhika nacho ni muhimu.
The law of impermanence...!
 
The law of impermanence...!

Mambo vipi mkuu.

Hii law mara ya kwanza naisoma kwenye Chinese Poem ya Lao Tsu sikuielewa. Baada ya muda kupita nikawa naitafakari. Hivi sasa ninaikubali 100%.

Wewe unaionaje mkuu?
 
Niliisoma mara ya kwanza mwaka 1995 na nimeishi nayo!imenisaidia mengi na mimi ni muumini waje kwakuwa hata imani yangu inaitaja
 
Hiki kitu kimeishi ndani yangu kabla ya kukikuta hapa; nimefurahi kugundua ya kwamba tunawaza kwa kuelekeana
Ingawa mimi nimekuwa nikiwaza katika mkabala wa mahusiano zaidi:Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia watu ili ufanikiwe katika mahusiano ni lazima ujue mwenza wako hawezi wala wewe huwezi kumridhisha au kumpatia mahitaji yake yote, mfano michepuko ni mfano tu wa kutafuta Yale tunayoyakosa kwa wenzi wetu.lakini ikiwa wenzi watajua ya kwamba pamoja na kupendana lakini hawatoweza kuja kupatiana mahitaji Yao kwa asilimia Mia , ni wazi hakuna ambae angehangaika na michepuko.
michepuko nayo Ina vitu ambavyo haitaweza kutimiza ila mkeo
So maisha siku zote yana gap ambalo haliwezi zibika kamwe ila kwa sisi tu kufikia muafaka kwamba baadhi ya vitu hatutoweza kuvipata mpaka tunaingia kaburini. Kiuchumi , kijamii na hata kisiasa! Ni lazma tusijenge tabia ya ni lazima kupata kila kitu, hapa ndipo tunapopotea wengi
 
Sahihi kabisa
 
Niliisoma mara ya kwanza mwaka 1995 na nimeishi nayo!imenisaidia mengi na mimi ni muumini waje kwakuwa hata imani yangu inaitaja

Okay.

Unaitazama vipi hii law? Maana sio law ya kiimani tu, ni law ya kisayansi pia. Kimaisha na kiulimwengu unaionaje hii law?
 
Back
Top Bottom