Guy Black
Member
- Mar 30, 2020
- 67
- 65
Mtu anaejifunza karate au sanaa nyingine yoyote ile ya mapigano, hupata faida nyingi sana, ikiwemo kwanza anapata uwezo wa kujihami dhidi ya wanyang'anyi, wabakaji, watekaji na wauaji. Pia, anakuwa na afya njema , na hawezi kupata magonjwa yasioambukiza kirahisi na hata kama akipata hawezi kuhathirika kirahisi. Kwasababu kinga zake za mwili zinakuwa zipo imara sana kutokana na mazoezi ambayo anayafanya kila siku . Vilevile anakuwa jasiri sana, mvumilivu, mwadilifu, mnyenyekevu, mchamungu na mwisho anapata ujuzi wa kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya sio ambukiza kwa njia ya kufanya mazoezi ya viungo na kula vyakula vya asili.