Faida ya maharage ya soya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya maharage ya soya

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 29, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Soya ina vitamin A,B,C,D,E na K. hakuna chakula duniani chenye vitamini nyingi kama hiki, soya ina protini ya ajabu na mafuta pia ambayo huifanya kuwa chakula pekee na safi. Uboreshaji wake wa afya ulifanya watu wa zamani kuitambua kama chakula cha pekee kwao ikawa chakula kizuri cha mbadalaambacho walikitumia badala ya nyama, maziwa na mafuta (butter) pamoja na mayai.walitumia watu wa rika zote, na wagonjwa pia, ilitumiwa pia kulisha ndama, ng’ombe, na kwa kufanya hivyo 90% ya ugonjwa wa kifua kikuu ulipungua kwa ndama. Soya ina mambo mengi na misaada katika miili ya wanadamu.
  KAZI YA SOYA MWILINI


  Soya ina glycerine na fatty acid ambayo inasaidia kazi nzuri ya ufanyaji kazi wa ubongo na maini. Pia ina chakula kizuri kwa neva ya ufahamu iliyochoka maana ina licitini, hii huifanya kuwa chakula kizuri sana kwa wazee.
  PROTINI YAKE


  Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika mayai sabini.
  Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika nyama kilo 3
  Kilogram 1 ni sawa na protein inayopatikana katika maziwa lita 2.
  MATUMIZI


  Soya hutengenezwa karanga za kutafunwa
  Soya hutengenezwa chakula cha nyama.
  Soya hutengenezwa maziwa mazuri sana
  Unga wa soya hutumiwa kwa:-
  Kukaangia chakula
  Kupikia ugali
  Kupikia chapati na mikate.
  MATAYARISHO


  Weka maharage ya soya kwenye maji, kwa masaa 24. kisha yaanikwe na kusagwa ili kupata unga .


  SOYA HUTIBU YAFUATAYO


  Hutibu vidonda vya tumbo
  Kisukari
  Saratani
  Tumbo
  Figo
  Ini n.k


  MAELEZO ZAIDI KUHUSU MATAYARISHO NA MATUMIZI YA MAHARAGE YA SOYA


  Ikumbukwe, kama tulivyoona hapo juu kwamba, maharage ya soya ni chanzo kizuri sana cha protein ifaayo kwa ukuzi na ustawi wa binadamu. Hata hivyo ni vyema izingatiwe kuwa, ndani ya maharage hayo vimo viini ambavyo visipodhibitiwa huudhuru mwili wa mlaji, viini hivyo vinajulikana kama “Anti Nutritional Factor” mojawapo na maarufu ni vile viitwavyo “Trypsin initiator” ambavyo vinapotumiwa huzuia protein isitumike mwilini mwa mlaji. Salama ni kuhakikisha kuwa hizo “Anti – Nutritional Factors” zimeangamizwa, nazo huweza kuangamizwa kwa njia ya joto kwa kuchemsha au kukaanga. Kwa matokeo mazuri, kabla ya kuchemshwa au kukaanga ni vyema kuyaloweka majini – kikombe kimoja cha soya katika vikombe 5 vya maji kwa muda wa masaa 6, kisha chemsha kwa dakika 30, yakaushe barabara ndipo yasagwe
  ZINGATIA UWIANO UFUATAO


  1:5 kwa kuyaloweka (soya : maji)
  1:9 kwa ajili ya uji (unga wa soya : unga mwingine)
  1:3 kwa wjili ya maziwa (unga wa soya : maziwa)


  KWA MAZIWA


  Baada ya kukoroga mchanganyiko huo, chujavyema na kitaambaa safi. Kimiminika kinachopatikana ndiyo maziwa ya soya. Ni vyema maji yatumiwe yaliyo salama baada ya kuchujakiasi.


  Kukaanga maharageya soya yaliyolowekwa kwa masaa 6 hadi yanapo kuwa na rangi kama ya majani makavu (brown) kuangamiza trypsin initiators. Ikiwa maharage ya soya yasiyolowekwa yamekaangwa hadi kuwa na rangi kama ya majani makavu (brown) trypsin initiators huwa imeangamizwalakini protini huwa pia imedhurika. Hivyo salama na uloweke kwa masaa 6 kabla ya kukaanga, tumia moto kidogo ili usiyaunguze.


  MUHIMU


  Ili kuandaa unga wa soya wenye mwonjo wa lishe unaokubalika, tumia maharage ya soya mazima kabisa.
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,755
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu,u have made my day!!!!!
   
 3. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  leo naenda kununua kilo moja ya soya na nitayachemsha kama maharagwe then nitayaunga kwa nyanya, hoho, kitunguu, nyanya chungu. nadhani itakuwa mboga safi...... mnaonaje hapo wakuu?? karibuni
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mboga ya kutosha na mimi nitakuwa mgeni wako unifungulie mlango.
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hautaweza kula. Ni mabaya haina mfano ukiamua kuyapika kwa namna ulivyoeleza. Ili ujifunze vizuri na usinione muongo pia usipate hasara, pika kikombe kidogo kimoja. Matokeo tujuze.
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  MZIZIMKAVU; AHSANTE SANA KWA POSTS ZAKO AMBAZO ZIMELENGA KUTUSAIDIA NA KUTUEPUSHA NA MATATIZO MBALIMBALI YA MAGONJWA.

  USIKUTE KUNA MTU ATATOKEA HAPA NA SOURCE UNAFIKIRI TUNAANDIKA THESIS, WEWE USIKATISHWE TAMAA NA WALE WANAOPENDA KUKOSOA HATA JAMBO ZURI. KWANI HAO LAZIMA WAWEPO KTK JAMII YOYOTE ILE. WEWE ENDELEA KUTUPA MAMBO KAMA NI MAZURI TUTACHUKUA NA KAMA NI MABAYA TUTAYAACHA. KWANI UKIWA WEWE SOURCE KUNA TATIZO? AU SOURCE MPAKA IWE MZUNGU? EBU TUACHE KUWAKATISHA TAMAA WENZETU WENYE MOYO WA KUSAIDIA JAMII KAMA MZIZIMKAVU ANAVYOFANYA. Hongera sana na Mungu azidi kukutia nguvu hata mwakani uzidi kutushushia mambo ya maana hapa.
   
 7. D

  Denis j kabende Member

  #7
  Feb 14, 2013
  Joined: Dec 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Nimejifunza mengi,asante xana mkuu
   
 8. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2017
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  kaka mzizi je yatosha kuyaloweka maharage ya soya kilo 1 kwa lita 9 za.maji kwa masaa 6 kisha kuyaanika na kuyasaga bila kuyatoa maganda?
   
Loading...