Faida ya kutumia juisi ya miwa

Faida ya kutumia juisi ya miwa

Juisi ya miwa ina uwezo mkubwa wa kuipatia miili yetu nguvu kwa haraka na kukata kiu, na hii inasababishwa na sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini.

Kwa hiyo wakati mwingine ukiwa na uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa itakufaa zaidi.Juisi ya miwa ni tamu lakini pia ni nzuri kwa wagonjwa wa kisukari, kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic Index". Kutokana na hilo juisi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani.

Lakini ni muhimu kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa Daktari.Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma na manganese.

Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser".Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.

Juisi ya miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono na kidney stones.Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi na Madaktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano.

Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula.Juisi ya miwa husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo.

Juisi ya miwa husaidia kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa "constipation".Juisi ya miwa husaidia kuzuia meno kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini.Juisi ya miwa husaidia kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha ngozi.Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na kuiimarisha uso ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Btw, hiyo kukata kiu ni kiu gani hasa Mkuu?, maana humu pia kuna zile "products" za Chuo Kikuu cha Mzumbe wanaweza wasikuelewe!
 
Juice ya miwa na juice nyinginezo sio salama kwa mgonjwa wa kisukari, ukweli ni kwamba mwili hauna uwezo wa kutofautisha sukari ya kiwandani na sukari asili, juice za viwandani na za nyumbani zote zina sukari ya glucose na fructose, ukitaka kuamini maneno yangu jipime sukari halafu kunywa juice ya miwa, baada ya Saa moja jipime utakuta sukari imepanda ni salama kula matunda kuliko juice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia inaongeza hamu ya kufanya mapenzi na huwa inafanya ujiaikie raha wakati wa tendo that is what I experience nikila miwa.
 
Mkuu, hapo uliposema juice ya miwa inafaa kutumiwa na watu wenye ugonjwa wa kisukari nadhani umepotoka/sha/shwa.

Mgonjwa wa sulari akinywa juice ya miwa lazima lazima lazima sukari itapanda. Tufanye utafiti kabda ya kushauri watu kuhusiana na matumizi ya vyakula hasa wenye matatizo ya kiafya
 
attachment.php


View attachment 139930 View attachment 139930

Uzuri wa juisi ya miwa.

Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.

Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi jijini Dar es Salaam wanaouza juisi ya miwa.

Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina

virutubisho na madini kwa wingi.

Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya glucose' iliyopo.

Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.

Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.

Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.

Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.

Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni halisia.
MIWA SIO ALKALINE NI ACIDITY
 
While the juice is packed with nutrients, there are certain side effects. Policosanol present in sugarcane can cause insomnia, upset stomach, dizziness, headaches and weight loss (if consumed excessively). It can also cause blood thinning and can affect cholesterol levels in the blood.
 
Back
Top Bottom