Faida ya kutumia juisi ya miwa

Faida ya kutumia juisi ya miwa

Mkuu MziziMkavu juice ya miwa sijawahi kunywa kutokana na mazingira inavyotengenezwa. Nyingi mtaani inzi wengi sana na usafi hakuna kabisa. Ila mimi ni fundi mkubwa sana wa kula miwa. Shemeji yako huwa ana kibarua cha kununua miwa sana kwa ajili yangu. Ni tangu utoto niseme niliipenda miwa sana na iliendelea hadi ukubwani. Hakika nikila miwa huwa najiona na nguvu Fulani hivi mwilini. Ninajua kuwa ina glucose nzuri sema sifa nyingine ndiyo siluwa nafuatilia. Bravo dr. wangu.
 
Ukitaka juice nzuri waambie wakuuzie ile ambayo haijachanganywa na mabarafu, hila bei yake imesimama.
Ila mi naipenda iww bardiii kwa siku nakunywa lita moja,wapo wanaochanganya na Tangawiz na ndimu
 
Hayo mabarafu ukitaka juice freshy mimi nanunua lita moja kwa sh. elfu 5000 freshy nikifika ananitengenezea bila kuchanganya na maji. Ni nzuri kwa afya na ni dawa kubwa ya Ugonjwa wa Ini (Manjano) ukinywa unapona na nilikuwa na nunua hiyo almost 1 year kwa mgonjwa na sasa kapona kabisa.
Mdau juis lita moja freeesh mwananyamala hapa buku,ww ulikua ukinunua wapi au huko kuna uhaba wa miwa?
 
................ pia inarudisha heshima katika ndoa! Jamani miwa! Miwa jamani!

Naona unataka kufanya miwa iadimike na kupanda bei sasa. Acha minenno yako aisee

[emoji16]
 
Okei, thanks!! Mi huwa nikiona inavyotengenezwa tu nachoka ila kuna jamaa mmoja pale mawasiliano kituo cha daladala dar kwa nje katengeneza sehemu safi kabisa ya kutengenezea juisi, nitakuwa mteja wake.
 
Back
Top Bottom