Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Bustani ya Edeni ni hadithi iliyoelezwa katika dini ya Abrahamaiki, ikiwa ni pamoja na Uyahudi, Ukristo, na Uislamu. Katika hadithi hiyo, Bustani ya Edeni inaelezwa kama mahali pa kipekee ambapo Mungu aliweka wanadamu wa kwanza, Adam na Hawa (Eva), na ilikuwa ni paradiso kamili ya uzuri na neema.

Ni muhimu kutambua kwamba hadithi ya Bustani ya Edeni haielezi tukio la kihistoria ambalo linaweza kufikiwa kwa njia ya uchunguzi wa kisayansi au ramani. Badala yake, hadithi hiyo ina nia ya kutoa mafundisho ya kiroho na maadili kwa wafuasi wa dini hizo.

Inafaa kutambua pia kwamba kuna tofauti ndogo katika maelezo ya Bustani ya Edeni kati ya dini hizo tatu. Katika Biblia ya Kiebrania, ambayo inatumika katika Uyahudi na Ukristo, hakuna ufafanuzi wa kijiografia wa mahali ambapo Bustani ya Edeni ilikuwa. Katika Uislamu, kuna maelezo kidogo yanayotaja kwamba Bustani ya Edeni iko ardhini, lakini tena, hakuna habari ya kijiografia ya mahali hasa.

Katika mtazamo wa kisayansi, hakuna ushahidi wa kihistoria au kijiolojia unaounga mkono uwepo wa Bustani ya Edeni kama mahali halisi duniani. Hadithi hiyo inachukuliwa zaidi kama hadithi ya kidini yenye maana ya kiroho.

Kuhusu hadithi ya Adam na Eva kula tunda la mti wa katikati, ni sehemu ya hadithi ya Biblia inayojulikana kama Kitabu cha Mwanzo. Hadithi hiyo inafundisha kuhusu uasi wa kwanza wa binadamu dhidi ya amri ya Mungu. Kimsingi, inaelezea jinsi Adam na Eva walivunja agizo la Mungu la kutokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hadithi hiyo inachukuliwa kama mfano wa jinsi dhambi iliingia ulimwenguni na kuleta matokeo yake kwa binadamu.

Ni muhimu kutambua kwamba hadithi hii inachukuliwa kwa njia ya kiroho na isiyokuwa ya kihistoria na wengi wa wafuasi wa dini hizo. Inasisitiza umuhimu wa kumtii Mungu na athari za kutotii amri zake.
Okay sawa so roho ni nini
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
Kwa nini tunda walikula wengine ila adhabu ikatuhusu wote?
 
Tafuta biblia zilizo halali utajua maana ya Tunda, achana na hizo nakala za kihuni walizotafsiri VATICAN kwa kuficha ficha mambo kwa maslahi yao.

Mtu wa kwanza hakuitwa Adam wala mkewe hakuitwa eve maana hawakuwa na asili ya Uzungu, pili hawakuishi huko walikotuaminisha hawa wachungaji na wanasayansi uchwara.

Tatu Tunda maana yake ilikuwa ni maarifa/Neno la ujuzi wa kutambua mambo fulani hapa dunian, na Mti ulito toa hayo matunda ni Malaika ambao waliishi dunian na walikuwa na mission zao hapa hapa dunian.

Mtu wa kwanza alipewa ONYO asiwasiliane na hao malaika wala kuwaomba wampe/wamwambie Habari za maarifa waliyonayo ambayo walukatazwa kuyajua maana yalikuwa nje ya uelewa wao(Tunda).

Baada ya kuumbwa kwa mwanamke ambaye biblia za uongo zinamuita eva/hawa huyu hakuumbwa kwa udongo kama Adam bali aliumbwa kutokana na Imagination+mawazo ya Adamu kuhusu uwepo wa kiumbe kitakachofanana nayeye kitakachomtoa upweke hivyo eva aliumbwa kwa staili hii.

Kwakuwa Eva hakuwa na Uelewa sawa ama nguvu sawa na adamu bali alishawishika na kiumbe ambacho biblia zenu zinasema ni nyoka(Dragon) ambaye ndiye alimshawishi eva na eva ndiye wa kwanza kuyasikiliza maarifa ya wale malaika walioambiwa wasiyasikie na baadae akamueleza Adam, hapa ndipo chanzo cha maovu kilipoanza.

Adam hakufa kama tunavyodanganywa bali alipewa laana kwa wazawa wake na hata eva hakufa tafuta ktk biblia yako hutoona maala wanaeleza hili jambo zaid ya kudanganya kuwa adam alikufa na umri wa miaka fulan which is nonsense.

Unatakiwa ujuwe kuwa Adam mission yake aliyoletwa dunian ilikuwa ni kuongeza idadi ya malaika waliosaliti ambao idadi yao ilitakiwa kuwa replaced na wana wa adam atakao wazaa na mkewe maana Adamu nae kabla ya kuumbiwa mwili alikuwa ni sehemu ya malaika, baada ya anguko la shetan na wenzie ndipo ikaja sababu ya adamu kushushwa dunian na akafanyiwa mwili ili aweze kuendeleza uumbaji wa malaika wapya(wanadamu).

Idadi inayotakiwa kwa wana wa adamu kureplace idadi ya malaika waliosaliti mbingu inajulikana na huenda ikatimia muda ukifika.

Shida za dunia hazitokwisha na hizo raha mnazotamani hazitopatikana maana huyo kiumbe anaeitwa shetan hataki idadi ya wana wa adamu itimie maana ikitimia na ule mwisho utafika na hukumu kwa shetan na wafuasi wake itafika.

Shetan si mjinga kuwapotosha watu na kuwafanya wamsaliti Muumba ili tu idadi isifikie na malengo ya shetani kuutawala ulimwengu yaendelee uku idadi ya wana wa adamu ikiendelea kudhorota na anguko la wengi liwepo.

Tutafute elimu nje ya box, Hilo kanisa la kizungu la Katolic wakishirikiana na madhehebu yote na dini zote hawa ndio wahuni nambari moja waliopotosha Biblia ya kweli kwa kufuta baadhi ya vitabu na vingine kuvipotosha kwa kuedit na kuweka uongo mwingi maana hawa wote wako chini ya shetan kuhakikisha wana wa Adamu hatuijui kweli na hatuifikii ile idadi inayotakiwa kureplace jeshi la shetani.

Tuendeleeni kushabikia mamipira, maushenzi ya kubishiana dini ya nani ndio sahihi, kuuwana sisi kwa sisi, kujadiri uwepo wa Mungu na ujinga mwingne tunajichelewesha sisi wenyewe
Du...
 
Mangi haya mambo, hayajawahi kupata majibu maridhawa toka kwa wateule na washirika waishio humu ndani..!
Sasa swali kama.."Je mungu muumbaji wa vyote..mwenye kujua yote yaliyopita, yote yaliyopo, na yote yatakayokuja, hakujua kama Adamu atakula tunda?Mjuzi wa YOTE Alishtukia tu Adamu kashakula bila Yeye (MJUZI)kujua?
Mangi, labda humu jamvini yupo aliyewahi kujibu maswali hayo pasipo kuacha shaka, lakini niliowahi kuwasoma humu sijamwona.
KIUKWELI NI MASWALI YANAYOWANGISHA VICHWA VYA WATEULE HUMU.
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea

Kama kesi ni tunda

Inamaana Mungu naye Kuna tunda lake la mema na mabaya hajakula ndio maana hafi/anaishi milele mkuu?
 
Hatukuzaliwa ili TUFE. Bali dhambi ndio ilibadili uhai mrefu kuwa majuto ya kifo.
Hizi dini zimeundwa na binadamu ili kutoa majibu mepesi mepesi kama haya, dini ni imani tuu unaweza kuamini chochote, life is mysterious binadamu hatujui tumetoka wapi na tunaelekea wapi, labda ukijibu umetokea wapi kabla hujazaliwa unaweza kujua unaelekea wapi kitu ambacho ni impossible
 
🤣🤣🤣Mbn wachungaji hutufanyia mmbo sio kuwa kama hatusali ktk madhehebu au ktk majumuiya nivigumu siku umepatwa na tatizo la msiba wao kuja hii imekaaje
 
Mangi haya mambo, hayajawahi kupata majibu maridhawa toka kwa wateule na washirika waishio humu ndani..!
Sasa swali kama.."Je mungu muumbaji wa vyote..mwenye kujua yote yaliyopita, yote yaliyopo, na yote yatakayokuja, hakujua kama Adamu atakula tunda?Mjuzi wa YOTE Alishtukia tu Adamu kashakula bila Yeye (MJUZI)kujua?
Mangi, labda humu jamvini yupo aliyewahi kujibu maswali hayo pasipo kuacha shaka, lakini niliowahi kuwasoma humu sijamwona.
KIUKWELI NI MASWALI YANAYOWANGISHA VICHWA VYA WATEULE HUMU.
Ni story tu ya kutungwa na mababu wa zamani wakijaribu kuelewa mwanzo wa kila kitu..na imekopiwa na kupestiwa jamii mbalimbali mpaka imefika kwenye Bible na Quran. Story hii haina ukweli wowote wa kihistoria
 
Hizi dini zimeundwa na binadamu ili kutoa majibu mepesi mepesi kama haya, dini ni imani tuu unaweza kuamini chochote, life is mysterious binadamu hatujui tumetoka wapi na tunaelekea wapi, labda ukijibu umetokea wapi kabla hujazaliwa unaweza kujua unaelekea wapi kitu ambacho ni impossible
😂Si ulikuwa tumboni ama
 
Ni story tu ya kutungwa na mababu wa zamani wakijaribu kuelewa mwanzo wa kila kitu..na imekopiwa na kupestiwa jamii mbalimbali mpaka imefika kwenye Bible na Quran. Story hii haina ukweli wowote wa kihistoria
Mkuu, unaweza kuwa sahihi kabisa...Wako humu wanachungulia-chungulia tu, Maana hawana cha kujibu "
 
Back
Top Bottom