Faida ya kuandika malengo

Nov 2, 2020
68
90
Wakuu Habari,

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi ya Uhai na salama .

Leo niandike jambo kuhusu kuandika Malengo

Mwanzo niliamini ni maneno tu kama yalivyo mengine hasa yale yanayosemwa na Inspirational na motovational Speakers, ambao hivi karibuni wamekuwa wakidhihakiwa kama ilivyo dasturi ya baadhi yetu Watanzania.

Lakini tangu nimeyaandika malengo yangu ambayo ninapaswa kufanya kwa mwaka 2020, niyafanye vipi na mwisho uwe ni lini, Namshukuru Mungu mwisho huu mwaka nimepata faida nyingi.

Miongoni mwazo ni kuwa, Nimejua mambo gani nimefanikiwa na nimeyafanya lini na kwa vipi.

Imenisaidia kujua yale ambayo sijayafanya, kwa nini sijayafanya na nifanyeje ili kuyafikia.

Nimekuwa si mtu wa kupoteza muda kwa mambo ambayo yako nje ya malengo yangu hasa yanayoletwa na watu wa karibu na hata wa mbali.

Kwenye bajeti kama sehemu ya ukamilifu mkubwa wa malengo yangu, nimejua jinsi gani nipangilie matumizi ya fedha kwa kupunguza matumizi yasiyo na lazima na pia kujibana kadiri ya uwezo ili kujikimu.

Imenisaidia kujua kuwa, nifanye nifanyavyo lakini mimi ndie ninayekamilisha malengo yangu kwa asilimia mia moja hivyo sipaswi kumuachia yeyote.

Pamoja na yote changamoto hazikosekani ila zimeniimarisha kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na Corona kama moja ya changamoto iliyoikumba dunia nzima.

Si mbaya kuandika mambo yako ikiwa ni pamoja na malengo yako kimaisha sehemu ambayo utayaona kila saa, siku au muda wowote utakayoyahitajia.

Youth Worker

Hardness, Teaches
 
Back
Top Bottom