Faida na Hasara za Tamko la JPM kwenye jamii.

Faida na Hasara za Tamko la JPM kwenye jamii.

Huko ndiko kutetea mimba mashuleni.unajificha nyuma ya madhara.mr eli7 hakuna haki bira wajibu.hatuwezi kuruhusu mimba kw kisingizio cha madhara.hebu fikilia ndg angu Eli7 una watoto 7 nyumbani kwako wa kike woote.na woote wako shule.mkubwa yupo kdto cha 2 wengne wako msingi mkubwa anarudishwa shule na mimba.unaitisha kikao cha familia unamfariji mwanao na kumwambia HAKUNA SHIDA MWANGU.UKIJIFUNGUA UTARUDI SHULE.jee unajenga taswira gn kw hawa mabinti zako wengne.UNAFUNDISHA NINI?

Mkuu mimba zinasababishwa na mambo mengi buda.

Halafu hatuna
Bira=bila
Fikilia =fikiria
 
Uhalisia ni kwamba katazo la kutokuwasomesha hawa watoto halitafanya mimba ziishe mashuleni. Mimba zitaendelea kuwepo tu kama kawaida labda idadi ipungue japo sijui.

Kikubwa tutegemee..
1. Utoaji wa mimba mwingi
2. Watoto wa kike kutokusoma maana akishapata mimba na akagoma kutoa wazazi hawana uwezo kilichobaki atabaki nyumbani tu.
3. Tutegemee watoto wasio na future. Mtoto atakayezaliwa na mama aliyenyimwa elimu usitegemee ataandaliwa maisha ya baadae.
Kila uamuzi una faida na hasara.haiwezekani uwe na faida tuu %100.lkn lazima tujitizame km jamii km taifa.Maadili yetu yako wapi!! Watoto wetu wanaridhi nn kimaadili.ninyi ndio mnaotetea ndoa za jinsia moja kwa kisingizio cha haki.
 
Acha utetezi wa mambo ya hovyo.hili lifanye kwako wewe na familia yako.wakusanye watoto wako uwaambie kwako mimba ni RUKSA !!mila zetu zibatuzuia.na dini zetu pia zinatuzuia wewe unatushawishi kw kigezo gn??!! Ni upumbavu mkubwa sn.vijana woote wako shule wapigane mimba.wakiume afungwe miaka 30 na shule marufuku.lkn wakike yeye asome.HII HAIWEZEKANI. Kwanza nashauri wafungwe woote kw kuliaibisha taifa na kuitia hasara nchi.
Mkuu umenena vyema sana jinsia pendwa imekua ikipewa favouritism kubwa sana, wote wawajibishwe wakipeana mimba na c mmoja wapo tu ndo abebeshwe lawama.
 
Kila uamuzi una faida na hasara.haiwezekani uwe na faida tuu %100.lkn lazima tujitizame km jamii km taifa.Maadili yetu yako wapi!! Watoto wetu wanaridhi nn kimaadili.ninyi ndio mnaotetea ndoa za jinsia moja kwa kisingizio cha haki.
Uamuzi unatakiwa uwe na njia za kupunguza hasara mkuu.

Mkuu kulikoni mimi na wenzangu gani tulikuwa tunatetea ushoga?? Umenifananisha bwana
 
Tusimjadili yeye, lengo la uzi sio kumjadili mheshimiwa. Tunataka kujua impact ya hili katazo kwa vizazi vyetu.
Kadai wasichana wenye ujauzito kuna options nyingi, kuanzia kufanya mitihani kama private candidates, kuingia kwenye ujasiriliamala, kilimo na shughuli zingine kem kem za uwezo wao..
Bro, nina jamaa US na UK, wanadai (kama kweli), hakuna msichana mwenye mimba anaendelea na shule, sasa kwetu mbona issue?! Maana hata mifumo yetu ya elimu kama yao..Ila wanadai hao wasichana bado ya uzazi wanarudi kuifanya kama private candidates, kama wakitaka...Swala turahisishe hawa wasichana wafanye hiyo mitihani (form 4 & 6) kwa urahisi kama wakitaka..
 
Wewe unafikiri watoto wanaopata mimba wameombwa mchezo tu wakatoa kwa ridhaa yao tu?

Je wanaobakwa?
Je waliokatika dhiki watu wanatumia nafasi kuwarubuni kwa karo au sababu zingine?

Je taratibu za kimila? Halafu unaniita kipofu?
Daby Mbona Unatetea Sana Hili Swala La Mimba Kwa Wanafunzi Je huoni Ni Sawa na Kusaport Dhambi ya Uzinzi Na Hauoni wanaume katika Hili wanakandamizwa Yani Mmoja Afungwe Mwingine Asome Real?!!!
 
Huko ndiko kutetea mimba mashuleni.unajificha nyuma ya madhara.mr eli7 hakuna haki bira wajibu.hatuwezi kuruhusu mimba kw kisingizio cha madhara.hebu fikilia ndg angu Eli7 una watoto 7 nyumbani kwako wa kike woote.na woote wako shule.mkubwa yupo kdto cha 2 wengne wako msingi mkubwa anarudishwa shule na mimba.unaitisha kikao cha familia unamfariji mwanao na kumwambia HAKUNA SHIDA MWANGU.UKIJIFUNGUA UTARUDI SHULE.jee unajenga taswira gn kw hawa mabinti zako wengne.UNAFUNDISHA NINI?
Sijaetetea popote, tunaangalia faida na hasara za uamuzi huo, hakuna kingine. Hakuna faida 100% ndio maana nikalileta hapa ili tuone hasara zake pia.

Kumbuka wanaoumia ni wale masikini, wenye uwezo watapeleka watoto wao huko private wakamalize masomo yao.

Lakini pia tuangalie ongezeko la utoaji mimba, inasemekana 30% wamewahi kutoa mimba, leo tunawaambia wakishika ujauzito hawana tena ruhusa ya kurudi shuleni, huoni utoaji mimba utaongezeka mkuu?
 
Uhalisia ni kwamba katazo la kutokuwasomesha hawa watoto halitafanya mimba ziishe mashuleni. Mimba zitaendelea kuwepo tu kama kawaida labda idadi ipungue japo sijui.

Kikubwa tutegemee..
1. Utoaji wa mimba mwingi
2. Watoto wa kike kutokusoma maana akishapata mimba na akagoma kutoa wazazi hawana uwezo kilichobaki atabaki nyumbani tu.
3. Tutegemee watoto wasio na future. Mtoto atakayezaliwa na mama aliyenyimwa elimu usitegemee ataandaliwa maisha ya baadae.
Asante Daby kwa maoni yako, hilo limenifikirisha pia.

Imagine mzazi ana mtoto huko gov't school, bahati mbaya kashika ujauzito, mzazi anajua hawezi kumpeleka st. Mary international school, unadhani atachukua uamuzi gani??
 
Mkuu umenena vyema sana jinsia pendwa imekua ikipewa favouritism kubwa sana, wote wawajibishwe wakipeana mimba na c mmoja wapo tu ndo abebeshwe lawama.
Wamepewa favour coz wamekuwa wakikandamizwa na mfumo dume tangu zama za nabii Issa(Yesu), je tuache kuwapa favour??
 
Kadai wasichana wenye ujauzito kuna options nyingi, kuanzia kufanya mitihani kama private candidates, kuingia kwenye ujasiriliamala, kilimo na shughuli zingine kem kem za uwezo wao..
Bro, nina jamaa US na UK, wanadai (kama kweli), hakuna msichana mwenye mimba anaendelea na shule, sasa kwetu mbona issue?! Maana hata mifumo yetu ya elimu kama yao..Ila wanadai hao wasichana bado ya uzazi wanarudi kuifanya kama private candidates, kama wakitaka...Swala turahisishe hawa wasichana wafanye hiyo mitihani (form 4 & 6) kwa urahisi kama wakitaka..
Kiongozi, wanaume wanaowajaza mimba, je sheria inawabana kiasi gani? Najua utasema 30yrs imprisonment lakini ni kwa asilimia ngapi Hilo linatekelezwa?
 
Hapo kwenye ongezeko la utoaji mimba kuongezeka na kweli...
Kama zamani walikuwa wanafanya hao watoto wenyewe kwa siri wazazi wasijue... Sasa hivi inawezekana hata wazazi wakashiriki...

Ila ni sawa tu... Wakipata mimba hakuna kurudi...


Cc: mahondaw

Cc: mahondaw
 
Kiongozi, wanaume wanaowajaza mimba, je sheria inawabana kiasi gani? Najua utasema 30yrs imprisonment lakini ni kwa asilimia ngapi Hilo linatekelezwa?
Hilo sasa mkuu ndilo la kushughulikia, harakati zako na mke wako kuhakikisha mwapata haki yenu. Binafisi ntaliangalia kwa wigo na weledi mzuri kivyangu vyangu, nina watoto 2 wa kike 20 na 17, ntalishughulikia kitofauti, maana nitamhitaji mweshimiwa aliyesababisha hilo ashirikiane na mwenye mimba, ila kuna wazazi wengine wa mtoto wa kike watataka njemba iende ndani 30...Kila mzazi ataamuwa kivyake mkuu..
 
Wasubiri wamalize shule ,mbona sisi tumeweza kwanini wao wasiweze au achague moja kuzaa au shule acheni kuendekeza ngono zembe bana khaaa
 
Asante Daby kwa maoni yako, hilo limenifikirisha pia.

Imagine mzazi ana mtoto huko gov't school, bahati mbaya kashika ujauzito, mzazi anajua hawezi kumpeleka st. Mary international school, unadhani atachukua uamuzi gani??
Veta.akishindwa akauze bar.kw sbbu ndicho alichochgua.
 
Nilichogundua katika hii mada au hili suala ni kwamba kuna watu wanaunga mkono hili katazo kwa msukumo wa kiimani za kidini wao wanaona ni sawa kwa kuwachukulia hao wanafunzi ni wazinifu tu,ila wengine wanadhani wanaopinga hili suala ni wapinzani wa serikali.
 
Nimeleta uzi huu MMU kwa sababu unaihusu jamii, hasa wanawake ambao kwa hili ni wahanga wakubwa.

Wiki iliyopita wote tulimsikia mheshimiwa kabisa akitoa tamko kuwa mtoto wa kike aliyeko shule akifanya kosa la kujibebesha mimba, hatorudishwa shuleni. Kwa maana kwamba mheshimiwa hataki kusomesha "wazazi".

Tamko hili limepokelewa kwa hisia tofauti, wapo wenye kumuunga mkono lakini pia wapo wanaopinga tamko la mheshimiwa, zikiwemo NGOs zinazotetea jinsia hii pendwa.

Kuna mambo ya kuangalia hapa, swala la utoaji mimba kwa dada/shangazi/wake/watoto wetu limeshamiri sana, hata kipindi ambacho hakukuwa na pingamizi la watoto kutorudi shuleni baada ya kujifungua. Kuna tafuti tofauti zimefanyika ndani na nje ya nchi, zikionyesha kuwa kati ya wanawake 10, watatu wamewahi kutoa mimba angalau mara moja. 30% sio kidogo ni idadi kubwa.

Katika hizi groups ambazo wengi wamekuwa hawapendi wake/dada zao wajihusishe nazo, kuna wanawake wanaofunguka kuwa wameshindwa kupata watoto kisa walijaribu kutoa mimba wakati fulani, wapo wanaokiri kutoa hadi mimba nne kabla ya kuolewa (staggering amount, four abortions?...God forgive us).

Sasa najiuliza, mheshimiwa kapiga pini kurudisha waliozaa mashuleni, manake uwezekano wa kuchoropoa mimba utaongezeka tu. Nini faida/hasara za hii pini/katazo? Tutegemee kuona kizazi cha namna gani baada ya miaka kumi-ishirini ijayo??
c630ac19effdf84564a4c73959a95fca.jpg
Ulishasema wapo waliotoa mimba hadi 4 sasa sijui wametoa baada ya tamko la raisi au? Na je kama nikabla raisi hajasema nini kimewafanya watoe? Tatu nikwamba mambo yamwanafunzi kupewa mimba niujinga na tabia mbaya ya mwanafunzi hivyo anastahili adhabu kali ambayo ndo hiyo..

Nakumbuka watu walikua wanajiuliza kua wakati mwanaume anahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwakumpa mwanafunzi mimba jee na huyu mwanafunzi kwanini asipewe adhabu maana hata yeye katenda kosa, sasa leo hukumu imetajwa rasimi ambayo kwa lugha nyepesi nikwamba mwanafunzi akipewa mimba akiwa shuleni adhabu yake ni kufukuzwa shule na huyo mwanaume anafungwa miaka 30 sasa hapa ubaya uko wapi au angetakiwa afungwe nayeye kama mwanaume? Au ndo arudi shuleni apewe mimba tena mwingine afungwe? Sasa itafikia hatua wanaume sita wanafungwa miaka 30 jela kwakosa lakumpa mimba mwanafunzi mmoja
 
Back
Top Bottom