MarianaTrench
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 1,212
- 942
Hasara na faida za kukaa kimya.
Ndugu wanajamvi habari za wakati?
Poleni na hongereni kwa pilika pilika za uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 25 na 26.
Pongezi nazitoa kwako Mtanzania mwenzangu uliejitambua ukatumia haki yako kumchagua kiongozi anaefaa akutumikie.
Ndugu zangu leo nilitaka nizungumzie swala moja hivi. Kukaa kimya.
Natumia lugha yetu naamini kila mmoja anaielewa na haihitaji maelezo Zaidi. Katika maisha yangu nimeona faida nyingi za kukaa kimya. Sipeleki suala hili katika mlengo wa kisiasa ila katika jamii yetu kwa mfano maisha ya mke na mume....kaka na dada..wafanyakazi wenzako...majirani...ndugu na kadhalika hasa panapotokea mapishano katika kauli baina yenu.
Binafsi mimi sio mpole ila ni mkimya. Nimeona Napata faida kubwa sana kwa ukimya huu nimeona vema niwashikirikishe na nyie. Unapokaa kimya unaruhusu Mungu akutetee kwa lolote unalokumbana nalo. Pia utajifunza mengi kutoka kwa wale wanaozungumza. Wewe ukiongea unarudia rudia tu kile unachojua ila unaposikiliza wengine waweza pata jambo jipya linaloweza kukusaidia maishani.
Unapokaa kimya unajijengea heshima kama ulikuwa na wazo la kipumbavu au kijinga unalificha na hapo heshima yako inaongezeka kati kati ya wanaokuzunguka. Pia kukaa kimya kiafya kuna renew afya ya akili ya mtu amabyo itakusaidia kuziongoza hisia zako vema kabisa. Ndio maana kuna wagonjwa wanaambiwa wakae kimya wasiongee tena Zaidi wakae sehemu yenye utulivu.
Hayo ni machache tu..lakini yapo mengi tu ya kunufaisha katika hili. Ukikaa kimya hata ugomvi unaweza ukajisolve automatically mbeleni yakaisha kiulaini kuliko vile itakuwa ukilianzisha wewe mwenyewe.
Mfano mzuri ni humu humu jamvini kuna watu wanapenda kutia neno kwenye kila jambo tunaona na pumba zao ila wangekaa kimya wangejijengea heshima tu.Hasara zipo pia za kukaa kimya kutojulikana, watakuona domo zege pengine haki inaweza porwa na yanayofanana na hayo. Pia mdomo kunuka bila kusahau kuumwa vinyongo na magonjwa ya moyo.
Nawatakia mchana mwema nimechoka kuandika wakuu. Ukitaka kujua Zaidi ya haya nenda google
MarianaTrench