A
Anonymous
Guest
Habari.
Watumishi tuliojiendeleza kielimu tukiwa kwenye halmashauri tunakumbana na changamoto kubwa katika kufanyiwa re-categorization (recate) kutoka kada moja kwenda nyingine.
Maafisa Rasilimali Watu (HR) mara nyingi hutoa sababu mbalimbali, zikiwemo ukosefu wa kutokuwepo kwa ruhusa ya kusoma kozi husika, ilhali waraka wa utumishi unaruhusu, pamoja na madai ya kukosekana kwa kibali cha promotion na recategorization.
Aidha, maelekezo ya mwaka huu yanaelekeza kuwa hata watumishi ambao hawakujumuishwa kwenye bajeti ya awali wafanyiwe recategorization. Pamoja na hilo, utekelezaji bado ni changamoto kubwa katika halmashauri nyingi.
Tunatambua na kuthamini jitihada za Katibu Mkuu, Waziri na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuendelea kutoa maelekezo kwamba watumishi wote wanaostahili promotion na recategorization wafanyiwe kwa wakati. Hata hivyo, katika ngazi ya halmashauri, baadhi ya Maafisa Rasilimali Watu wameendelea kukaa kimya na kuchelewesha utekelezaji.
Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili, kwani inaonekana kuna mbinu za ucheleweshaji (delaying tactics) zinazotumika, hali inayowakosesha haki watumishi wanaostahili recategorization na promotion.