Faida kuu tatu za udongo maalum wa kupandia miche uitwao Peat Moss

Mar 3, 2018
64
53
PEAT MOSS NI NINI?

Peat moss ni udongo maalumu unaotumika kwa ajili ya kuandaa miche hasa kwenye upande wa miche ya mboga mboga na matunda kama vile nyanya,hoho,papai n.k Udongo huu huzalishwa katika nchi za ulaya kama vile Norway,Finland na husambazwa duniani kote ili utumike katika shughuli za uoteshaji wa miche kwani umetengenezwa kuwa na sifa zote maalum zinazohitajika katika uotaji wa mbegu ukilinganisha na udongo huu wa kawaida tunaoutumia kupandia mazao yetu mashambani.Peat moss huenda sambamba na matumizi ya seedling trays,tray maalumu ambazo hutumika kupandia mbegu na kukuzia miche kitaluni.​

peat-moss-lead2_1170x600.jpg

Fig 1 Udongo wa peat moss unaotumika kupandi mbegu kwa maandalizi ya miche​

michehoho.jpg

Fig 2 Miche iliyotayari ikiwa imepandwa ndani ya tray kwa kutumia Udongo wa Peat moss​

KWANINI WAKULIMA WENGI HUPENDELEA KUTUMIA UDONGO WA PEAT MOSS?

Wakulima wengi hapa nchini kwetu wameanza kupenda kuzalisha miche kwa kutumia udongo huu maalum wa peat moss kwasababu mbegu za kisasa za hybrid huuzwa ghali kidogo ukilinganisha na hizi mbegu za kawaida za OPV na mara nyingi mbegu hizi huuzwa kwa punje na gharama ya punje za zao kama nyanya hufikia mpaka 150/= Tsh kwa punje moja hasa kwa mbegu za hybrid za ndani ya greenhouse.​
Mkulima anapoamua kulima kwa kutumia punje hizi ni lazima ahakikishe punje hizi zinaota zote ili kuepusha hasara anayoweza kuipata pindi punje hizi za mbegu zisipo ota kama zinavyotakiwa kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na Udongo.Udongo wetu huu wa kawaida unaweza kutumika lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo magonjwa,rotuba na sifa mbali mbali za udongo si mbegu zote zinaweza zikaota kama inavyotakiwa kitu ambacho kinaweza kuleta hasara kubwa sana kwa mkulima.Ili kuweza kutatua changamoto hii wakulima wamekuwa wakipenda kutumia udongo huu kwani umetengenezwa ukiwa na sifa zote muhimu zinazotakiwa kwa uotaji na ukuaji wa mbegu.​

b.jpg

Fig.3 Udongo wa peatmoss ukiwa katika package ya Kilo 50

FAIDA KUU TATU ZIPATIKANAZO PINDI MKULIMA ANAPO TUMIA UDONGO MAALUM WA KUPANDIA WA PEAT MOS​

(i)Udongo wa peatmoss unauwezo mkubwa wa kuhifadhi maji pamoja na hewa ya kutosha.

Moja ya sifa kuu ya udongo huu maalum wa peatmoss ni uwezo wake mkubwa wa kutunza maji na hewa ya kutosha kwa shuguli mbalimbali za mmea ikiwemo utengenezaji wa chakula.Udongo huu huweza kuhifadhi maji mara 20 ya uzito wake wenyewe na kuyaachia maji haya pindi yanapohitajika na mmea.Udongo huu pia huhifadhi hewa ya kutosha kwani hewa ya oxygen huhitajika sana na mmea hasa kwenye mizizi ili mmea kukua vizuri.

(ii)Udongo huu hauna magonjwa wala magugu

Udongo huu maalum huwa hauna kabisa magojwa yeyote yanatoambatana na udongo ambayo huweza kuleta changamoto katika germination ya mbegu pamoja na ukuaji wa miche pindi iwapo kitaluni.Tunapotumia udongo wetu huu wa kawaida changamoto kubwa tunayokuwa nayo ni kutokua na uhakika juu ya afya ya udongo kwani udongo unapokuwa na vimelea vya magojwa mbegu kuota huwa ni ngumu.Udongo huu unapotumika husaidia pia kupunguza uwepo wa magugu ambayo hushindania mbolea na miche pindi tunapotumia udongo wa kawaida wa kupandia

(iii)Udongo huu hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote pindi unapotumika

Pindi Udongo wa peatmoss unapotumika kupandia miche,hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote wala mbolea yeyote kwani umetengenezwa ukiwa na kila sifa zote zinazohitajika kwa uotaji wa mbegu pamoja na ukuaji wa mche.Hauhitaji kuchangwanywa na chochote mbali ya dawa zinazotumika kupiga miche pindi miche inapokua.Kilo moja ya udongo huu hutosha kujaza Tray Mbili wakati wa kupanda.

Kwa mahitaji ya udongo huu wa kupandia wa PEAT MOSS usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255752022108 | 0654357571.Tunauza 3500/= Tsh kwa kilo na pia upo kwa package ya kilo 50 ambao tuna uuza 170,000/=Tsh. SEEDLING TRAYS pia tunazo zenye idadi ya matundu tofauti tofauti kwa gharama ya 5000/=Tsh kwa tray. KARIBU KWA SWALI LOLOTE.
 
PEAT MOSS NI NINI?

Peat moss ni udongo maalumu unaotumika kwa ajili ya kuandaa miche hasa kwenye upande wa miche ya mboga mboga na matunda kama vile nyanya,hoho,papai n.k Udongo huu huzalishwa katika nchi za ulaya kama vile Norway,Finland na husambazwa duniani kote ili utumike katika shughuli za uoteshaji wa miche kwani umetengenezwa kuwa na sifa zote maalum zinazohitajika katika uotaji wa mbegu ukilinganisha na udongo huu wa kawaida tunaoutumia kupandia mazao yetu mashambani.Peat moss huenda sambamba na matumizi ya seedling trays,tray maalumu ambazo hutumika kupandia mbegu na kukuzia miche kitaluni.​

View attachment 1488464
Fig 1 Udongo wa peat moss unaotumika kupandi mbegu kwa maandalizi ya miche​

View attachment 1488478
Fig 2 Miche iliyotayari ikiwa imepandwa ndani ya tray kwa kutumia Udongo wa Peat moss​

KWANINI WAKULIMA WENGI HUPENDELEA KUTUMIA UDONGO WA PEAT MOSS?

Wakulima wengi hapa nchini kwetu wameanza kupenda kuzalisha miche kwa kutumia udongo huu maalum wa peat moss kwasababu mbegu za kisasa za hybrid huuzwa ghali kidogo ukilinganisha na hizi mbegu za kawaida za OPV na mara nyingi mbegu hizi huuzwa kwa punje na gharama ya punje za zao kama nyanya hufikia mpaka 150/= Tsh kwa punje moja hasa kwa mbegu za hybrid za ndani ya greenhouse.​
Mkulima anapoamua kulima kwa kutumia punje hizi ni lazima ahakikishe punje hizi zinaota zote ili kuepusha hasara anayoweza kuipata pindi punje hizi za mbegu zisipo ota kama zinavyotakiwa kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na Udongo.Udongo wetu huu wa kawaida unaweza kutumika lakini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo magonjwa,rotuba na sifa mbali mbali za udongo si mbegu zote zinaweza zikaota kama inavyotakiwa kitu ambacho kinaweza kuleta hasara kubwa sana kwa mkulima.Ili kuweza kutatua changamoto hii wakulima wamekuwa wakipenda kutumia udongo huu kwani umetengenezwa ukiwa na sifa zote muhimu zinazotakiwa kwa uotaji na ukuaji wa mbegu.​

View attachment 1488503
Fig.3 Udongo wa peatmoss ukiwa katika package ya Kilo 50

FAIDA KUU TATU ZIPATIKANAZO PINDI MKULIMA ANAPO TUMIA UDONGO MAALUM WA KUPANDIA WA PEAT MOS​

(i)Udongo wa peatmoss unauwezo mkubwa wa kuhifadhi maji pamoja na hewa ya kutosha.

Moja ya sifa kuu ya udongo huu maalum wa peatmoss ni uwezo wake mkubwa wa kutunza maji na hewa ya kutosha kwa shuguli mbalimbali za mmea ikiwemo utengenezaji wa chakula.Udongo huu huweza kuhifadhi maji mara 20 ya uzito wake wenyewe na kuyaachia maji haya pindi yanapohitajika na mmea.Udongo huu pia huhifadhi hewa ya kutosha kwani hewa ya oxygen huhitajika sana na mmea hasa kwenye mizizi ili mmea kukua vizuri.

(ii)Udongo huu hauna magonjwa wala magugu

Udongo huu maalum huwa hauna kabisa magojwa yeyote yanatoambatana na udongo ambayo huweza kuleta changamoto katika germination ya mbegu pamoja na ukuaji wa miche pindi iwapo kitaluni.Tunapotumia udongo wetu huu wa kawaida changamoto kubwa tunayokuwa nayo ni kutokua na uhakika juu ya afya ya udongo kwani udongo unapokuwa na vimelea vya magojwa mbegu kuota huwa ni ngumu.Udongo huu unapotumika husaidia pia kupunguza uwepo wa magugu ambayo hushindania mbolea na miche pindi tunapotumia udongo wa kawaida wa kupandia

(iii)Udongo huu hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote pindi unapotumika

Pindi Udongo wa peatmoss unapotumika kupandia miche,hauhitaji kuchanganywa na kitu chochote wala mbolea yeyote kwani umetengenezwa ukiwa na kila sifa zote zinazohitajika kwa uotaji wa mbegu pamoja na ukuaji wa mche.Hauhitaji kuchangwanywa na chochote mbali ya dawa zinazotumika kupiga miche pindi miche inapokua.Kilo moja ya udongo huu hutosha kujaza Tray Mbili wakati wa kupanda.

Kwa mahitaji ya udongo huu wa kupandia wa PEAT MOSS usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba +255752022108 | 0654357571.Tunauza 3500/= Tsh kwa kilo na pia upo kwa package ya kilo 50 ambao tuna uuza 1,70,000/=Tsh. SEEDLING TRAYS pia tunazo zenye idadi ya matundu tofauti tofauti kwa gharama ya 5000/=Tsh kwa tray. KARIBU KWA SWALI LOLOTE.
Kilo moja bei gani?shs 3,500/= au 35,000/= rekebisha tangazo lako
 
Mboji yote Tanzania,samadi bado tunaagiza udongo.Mboji ya porini ina wadudu? Tuache tabia ya kukurupuka na kila wanachoanzisha wazungu.Mwafrika yupo kwa ajili ya kumtajirisha mzungu.Watanzania ni watu wa kupigwapigwa tu.Wapige tu mkuuu.
 
Imefikia mahali mpaka udongo unafanyiwa biashara?

Hivi hatuwezi kurutubisha udongo wetu, wako wapi wataalamu wetu wa Kilimo waliosomeshwa na serikali kwa kodi zetu?...mifugo ipo na mbolea ipo nyingi tu mbona.
 
Iko hivi boss tunaposema 3500 kwa kilo hiyo ni bei ya reja reja ila ukinunua kwa jumla yaani begi zima la kilo 50 unapata punguzo la sh.5000 badala ya 175000/= Tsh unanunua kwa 170000/= Tsh.
Mkuu unazilisha mini ambachi kitakulipa m 1.75
 
Imefikia mahali mpaka udongo unafanyiwa biashara?

Hivi hatuwezi kurutubisha udongo wetu, wako wapi wataalamu wetu wa Kilimo waliosomeshwa na serikali kwa kodi zetu?...mifugo ipo na mbolea ipo nyingi tu.
Unajua hiki kizazi kinajifanya kina jua fursa.Mboji tulifundishwa kuandaa shule ya msingi.Kama ni wadudu unaipitisha ktk joto tu basi.Udongo utoke Ulaya wakati misitu ya asili ipo Afrika.
 
Ni declare interest ni mkulima na ninaotesha mbegu za hybrid, kwenye seedling trays, kutumia udongo huu huu, sijawahi kupata shida...

Ninajiuliza hii kitu wizara ya kilimo na taasisi zake zote, imeruhusu udongo kutoka nje kuuzwa nchini??

Magonjwa mengi ya mimea tunayoyaona yanakuja kwa njia nyingi...kuna uwezekano KANTANGAZE aliletwa hivi..na wakulima wote wa mboga na mahindi tunahaha!

Nimefadhaika samahani mleta mada...sikusudii kuharibu biashara yako.
Ila kama TPRI, TBS, wizara zimeruhusu, mimi nani??

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Hakuna kitu chochote kinachoruhusiwa kutumika hapa nchini kwenye kilimo bila kufanyiwa kwanza utafiti.Kifupi udongo huu sio kwamba ni kama udongo wa kawaida useme wanachota tuu huko ulaya kisha wanatuletea.Swala ni kwamba kama wewe una muda wa kuandaa udongo wako wa kupandia ni sawa ila kuna wakulima hawana muda wa kuanza kuandaa udongo na hawa ndio wanao penda kununua udongo huu.Wapo watafiti wanaoandaa udongo wao wa kupanda ila wote wana appreciate performance nzuri inayotokana na udongo huu ukilinganisha na udongo huu wa kwetu wa kawaida.
 
Unajua hiki kizazi kinajifanya kina
jua fursa.Mboji tulifundishwa kuandaa shule ya msingi.Kama ni wadudu unaipitisha ktk joto tu basi.Udongo utoke ulaya
wakati misitu ya asili ipo Afrika

Udongo huu sio kwamba ni kama udongo wa kawaida useme wanachota tuu huko ulaya wanatuletea.Sio kila mkulima ana muda wa kutosha kuandaa udongo huu wa kawaida ili kuwa na sifa zote za udongo zinazohitajika ili kuota na kukua kwa miche.
 
Hata hapa Dar mbona udongo huo upo, ukienda hapo Balton Mwenge karibu na majembe Auction Mart (zamani) wanauza udongo na trays pia.

Kimsingi ni udongo mzuri (seed planting medium) Kama eneo lako hukiamini Kama udongo wake upo poa.

Pamoja na ukweli huo Kuna haja ya kufahamu Kama wizara na mamlaka zake zinajua uwepo wa udongo huo na usalama wake.

Kimsingi mahonjwa mengi tunaletewa kwa style ya mbegu, mbolea na hata vimelea (Vita za kiuchumi). Tunaomba serikali iwe makini Sana na kuwe na ufuatikiaji wa karibu.
 
Back
Top Bottom