Unapaswa kuwa na uelewa wa mambo haya kabla hujaanza Kilimo cha Matunda

Godfrey Sway

Member
Apr 13, 2018
37
34
Vitu vitano (5) Vya Kuzingatia Wakati unapoingia kwenye Kilimo cha Matunda.

1. Eneo
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufahamu vizur jografia ya eneo, Hali ya hewa, kiwango Cha mvua n.k. Hii itakusaidia kufahamu ni wapi upande aina Fulani ya matunda na pia ni wapi usipande. Mfano parachichi inafanya vizur sana ukanda wa baridi kuliko ukanda wa joto Ambao Embe inafanya vizuri zaidi.

2. Maji
Kwa zaidi ya Asilimia 90 Ya mahitaji ya mmea ni maji. Unapokuwa na maji ya uhakika tayari upo kwenye nafasi kubwa sana ya kufanikiwa kwenye Kilimo. Tutumie vizur Mvua Za Vuli Kupanda Miche ya matunda ambazo zitatupeleka karibuni na Mvua za masika.

3. Mbegu Bora./ Miche Bora
Miche / Mbegu Bora ni Ile Iliyoandaliwa kwa ustadi na utaalamu mkubwa Kwa kuzingatia ustahimilivu, muda wa kuzaa, kiwango Cha mazao pamoja na Ubora. Hapa Tumekuandalia Miche Mizur kwaajili Yako wewe Mkulima Wetu.

4. Matunzo ya Shamba
Usafi wa Shamba, mpangilio wa Shamba, Muda sahihi wa mbolea na viwatilifu, Kuvuna pamoja na njia Bora za kuhifadhi vyote hivi ni vichocheo Vikubwa vya Mafanikio Yako kwenye Kilimo.

5. Soko
Hapa Tunaangalia jamii inayotuzunguka inahitaji Nini zaidi. Masoko yapo ya namna mbili soko la ndani na soko la nje. Soko la ndani kwa mazao ya matunda Bado ni kubwa sana.

Unakaribishwa tukuhudumie Miche ya Matunda Muda Mfupi, Ambayo Utaipata kwa Bei Ile Ile ya Tsh 2500 Tu.

Tupigie Leo.
Mr. Sway 0752799673
Glory Farm 0746850361

Tupo SUA Morogoro. Ulipo Unatumiwa Miche kwa usafir wa Bus.

IMG-20231104-WA0032.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom