Fahari amekuwa mama wetu wa ujinga?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Kuna ule wimbo wa kimanyema wa GERE MAMA una ujumbe murua sana ule wimbo, katikati ya beti zake kuna maneno yanasema fahari eeh. Ndio mama wa ujinga.

Wanawake wa uswazi wana hii hulka... Fahari na kujionesha kuwa mambo safi kabisa..Kumbe ni fukara wa kutupwa huku watoto wakiwa na utapiamlo na makazi duni. Chukulia mfano wanawake hao ukiwakuta kwenye sherehe au starehe. Vitu alivyopigilia.

Dhahabu
Make up
Mavazi
Manukato nk

Ukiachana na vya kukodi na kuazima vingine kajikamua kweli kanunua cash money! Yote hayo ni kujionesha mambo safi kabisa na hana shida ndogondogo. UFAHARI!

Akitoka hapo mfuate uone surprise
Atadandia usafiri hana hata nauli
Nyumbani ni chumba kimoja kibovu
Watoto ni kwashiorkor na utapiamlo
Watoto hawana huduma za msingi
Madeni kila kona nknk

Nina tatizo na waandishi wetu Tanzania. HAWAHOJI ama hawako tayari kuhoji ama pengine hawajui au hawataki KUHOJI.

Wamealikwa kwenye uzinduzi wa Ujenzi wa Ikulu mpya Chamwino Dodoma... Wanasiasa wakawa wanaisifia kuwa ni Ikulu nzuri na yenye eneo kubwa kuliko Ikulu nyingine zote duniani huku ikilingalishwa na Ikulu za Klemlin, Beijing Uturuki nk.

Come on guys, his is stupidity at high level mnajua! Tunajigamba kuwashinda UFAHARI watu wanaojiweza kwa kila kitu huku wakitusaidia kwenye mengi.

Mmejaribu kuhoji hao wenye maikulu makubwa tunaotaka kushindana nao wako kwenye level gani kimaisha? Kiuchumi?
Huduma za kijamii kwa wananchi wao zikoje?
Lishe
Elimu
Afya
Miundombinu?

Hivi katika wote hao tunaweza kweli kufananisha miji yao yenye Ikulu zao na Dodoma yetu inayotarajiwa kuwa na Ikulu nzuri kuliko zao? 75% ya vitu vitakavyopendezesha hiyo Ikulu vitatoka kwao. Vingine vikiwa ni msaada na mkopo pengine halafu leo hii tunataka kujimwambafy. Seriously?

Tuhoji hata kwa mafumbo ili fahari asiwe mama wa ujinga kwetu sote!!!!!

Jr
 
Wanasiasa ni waongo, wanafiki na wazandiki mnooo
Ndio maana siipendagi siasa na wenye siasa yao
 
Back
Top Bottom