Kisa cha mama wa kambo kilivyofilisi ukoo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
"Pole sana wanangu, Baba yenu anavuta bangi ndiyo maana maamuzi yake ni ya kikatili sana!

Hayo yalikuwa maneno ya Bi chaurembo alipowapa pole watoto wa mmewe!
Bi chaurembo aliishi na mzee msalaba takribani miaka sita! Mzee msalaba alikuwa akifahamika kwa malezi yake ya kikakamavu! hakupenda kudekeza watoto wake!

kila mara aliwasisitiza watoto kulinda walivyochuma kwa jasho! walipokosea aliwaadhibu palepale hadharani pasipo kusubili wasahau ili kutoa fundisho kwa wengine!
Bi. Chaurembo kwa unafiki, aliwahadaa watoto kwa huruma ili kuonesha mapenzi kwao! Hakika watoto walipendezwa sana na tabia ya Bi. Chaurembo!

Baada ya miaka kadhaa kupita, Mzee Msalaba alifariki na kuacha simanzi kubwa!
watoto walifarijika wakiamini mapenzi mazito watayapata kwa Bi chaurembo!

baada ya arobaini ya baba yao! Mzee mmoja alionekana kuwa karibu sana na Bi chaurembo!

watoto walihoji huyu mzee ni nani mama? Mama yao aliwajibu ni rafiki tu!

watoto ikabidi wakaulize kwa majilani kuhusu ukaribu wa yule mzee nyumbani kwao!

majilani wakawaambia yule mzee anaitwa Mzee MBOGA! Ni mzee mwenyeji aliyewauzia eneo hilo! lakini pamoja na kuuza eneo hilo kazi yake ni udalali, Hivyo majilani waliwasihi watoto wawe makini sana na huyo mzee kwa mama yao bi Chaurembo!

Siku moja usiku Mzee MBOGA alifika nyumbani kwa bi chaurembo!

Mzee mboga alianza kwa kusema, mna bahati sana, kuna mtu mmoja anaomba kujenga hotel ya kifahari kwenye fremu katika kiwanja chenu!

Lakini kabla ya yote! kanipatia zawadi hizi niwaletee!

Mzee Mboga alifungua begi kubwa lililojaa nguo za gharama, mikufu na vidani vya dhahabu na vingine vingi!
Bi chaurembo alifurahi sana akamwambia mzee mboga hao watu wambiye waje hata kesho tu!

Siku iliyofuata wale watu walimwambia bi chaurembo abadili hati ya kiwanja isome pamoja na jina lao ili waweze kujenga hotel hiyo!

Bi chaurembo kwasabu alimwamini sana hawala yake mzee mboga hakusita kufanya hivyo!
wale watoto walikumbuka maneno ya majilani kuhusu udalali wa mzee mboga!

Siku moja mtoto wa kiume akahoji; Mama kuna ulazima gani wa kubadili hati ili huyu mtu atujengee hoteli? Yule chaurembo hakujibu chochote kwasababu tayali alikuwa kashabadili na jina la hati!

Yule mtoto akazidi kumuuliza mama kila siku mama hakujibu chochote!
Wale watu wakaanza maandalizi ya ujenzi kwa kuleta vifaa vya ujenzi!
Yule mtoto wa kiume akasema hapajengeki kitu hapa!
Mzee bonga alipofika akamahauri yule mama, akamwambia hawa watoto wakianza kubalehe ndivyo walivyo, Hizo kelele ni za balehe, hivyo kama atakusumbua sana huyo mtoto " Kuna watu watamumwagia tindikali machoni ili awe kipofu"

hata kusumbua tena! Bi chaurembo hakuwa na pingamizi kwa hawala yake mzee mboga!

Bi chaurembo akatafta watu wa kufanya kazi hiyo! Kulikuwepo kundi moja lililojulikana kama NGOME MOJA!
Kundi hilo liliaminika kwa matukio utekaji! Hivyo basi bi chaurembo akawapatia pesa ili wakatimize adhima hiyo!

Wakati mipango ikiendelea, ndani ya kundi hilo la NGOME MOJA alikuwemo mtu mmoja hatari sana aliitwa KAPYARU, alikuwa ni mtoto wa pembeni wa ujanani wa mzee MSALABA!

Alisikitishwa sana na mipango ya kumdhuru Kijana ambaye hana hatia!
Siku moja kabla ya tukio KAPYARU na wenzake wakiwa katika mipango ya mwisho ya kumteka yule kijana!
Kapyaru aliomba tarehe ibadilishwe isogezwe mbele kwa wiki moja ili wajipange vizuri zaidi ..........ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom