Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Nishajibu hilo swali la kufatilia mkuu au ubongo kichwa cha panzi? Maana maswali yako unayarudia rudia tu.
Mimi pia mtumiaji wa Twitter pia naona details za watu nisio waFollow ila sio kwa kihasi icho Boss.

Acha kubadili rangi kama kinyonga.
 
Mimi pia mtumiaji wa Twitter pia naona details za watu nisio waFollow ila sio kwa kihasi icho Boss.

Acha kubadili rangi kama kinyonga.
Una kichwa kizito sana.

Kama bado hujafunguka akili kwa hiyo mifano uliyopewa, basi unastahili kutapeliwa.
 
Wakuu msiumize vichwa ,Ontario ni Tapeli Mjanja mjanja kwa watu ambao hawana upeo lazima awaingize king,Ontario kaanzisha Shindano la kujishindia laki 1 kwa watu 10 ,mmoja wa washindi ni Dan Pol na ametaja sifa nyingi sana za Dan Pol mpaka akampa laki 1 ,ukichunguza utajua tu Dan Pol ni Ontario mwenyewe.
Teh teh teh mkuu Asante sana kwa kuliona hili..

Hawa watu ujanja wao iko siku utakuja kuwatokea puani..
 
Sikuona hii post nyumba ya nani.
Huyo tapeli Ontario aliandika kwenye mitandao kwamba hiyo nyumba kawajengea wazazi wake.

Kwa bahati tu, jamaa ambaye wazazi wake ndio wamiliki wa hiyo nyumba akaona hiyo post ya huyo tapeli, jamaa akamfata tu DM kwa ustaarabu, atoe hiyo picha. Aliambulia block tu..
 
Jamaa sijaelewa kwanini ameuliza hilo swali ,hajui Ontario anasema yeye kwamba ni tajiri anaingiza mil 100 forex ,ana mashamba kibao ya mipapai ,ana mashamba ya mkonge mengi tu , ana biashara za kuku kibao ,ana miliki mandinga ya maana ,mijengo kibao ,amewajengea wazazi nyumba ya ghorofa lakini alikuwa amepanga mikocheni usd 1000 kodi ikamshinda akaenda kupanga hostel kwa elfu 40,swali kwanini asingeenda kukaa moja ya nyumba zake wakati akijipanga? Kama ana hela nyumba zake obvoius zitakuwa prime areas!
Acha wajinga wapigwe mkuu,bila wajinga wajinga hii dunia isingekua tamu mzee baba.
 
Teh teh teh teh mchizi wangu akujibiwa kitu akaambulia block tu..

Huyu dogo mpaka Magufuli atoke madarakani atawanyoosha sana vichwa panzi..
Hahah tangu aseme alikodisha sijui tractor kwa siku 30 na akapata mil 30 kama faida nilijua tu huyu ni tapeli per se.

Ila kuna siku huyu jamaa haya mambo yatakuja kumkalia hovyo watampa kesi za utakatishaji.
 
Huyo tapeli Ontario aliandika kwenye mitandao kwamba hiyo nyumba kawajengea wazazi wake.

Kwa bahati tu, jamaa ambaye wazazi wake ndio wamiliki wa hiyo nyumba akaona hiyo post ya huyo tapeli, jamaa akamfata tu DM kwa ustaarabu, atoe hiyo picha. Aliambulia block tu..
Ni jamaa yako mwenye nyumba yao.
 
Hahah tangu aseme alikodisha sijui tractor kwa siku 30 na akapata mil 30 kama faida nilijua tu huyu ni tapeli per se.

Ila kuna siku huyu jamaa haya mambo yatakuja kumkalia hovyo watampa kesi za utakatishaji.
Kesi ya utakatishaji inakuwaje mkuu.
 
Vimoradi miradi hivi vya sungura mara sijui samaki mara kuku mara nyanya huwa siviamini, ni bora ifanye mwenyewe at your own pace na kujijengea uwezo taratibu, asije mtu akaja kukupa plan ya kuingiza hela haraka haraka, ni utapeli tu
Wasiwasi ndio akili.
Miaka ya katikati hapo walijitokeza wa kware na mayai yake wakapotea,baadae wakaja wa sungura mafundi seremala hapa nao walineemeka sana kutengeneza mabanda ya kuhamishika wakapotea,sasa hv ndio amekuja huyu mr kuku.
Huyu Mr. kuku alichofanikiwa ni ile kuwapa urahisi wateja wake yaani ukishatoa hela mara 1 wewe unalala tu nyumbani kisha tarehe zikifika muhamala unasoma.
 
Utapeli wake uko wapi?

Ana mwaka wa tatu akiendesha mradi wake kwa mfumo huohuo, je ana rekodi ya kumtapeli mtu yeyote?

Uwekezaji ni lazika uwe wa kampuni za soda, beer au na bank? Kwamba uwezekaji kwenye ufugaji sio sahihi?

Je, kampuni kubwa ambazo watu wanawekeza huwa hazifilisiki?

Huyu bwana angehukumiwa kwa matumizi ya pesa za wawekezaji na sio kuweka general comments kwamba ni tapeli bila kueleza utapeli wake. Mbona hii mifumo inafanyika hata kwenye vikundi vyetu (formal na informal). Tunachangishana pesa na kuwekeza kwenye kilimo na miradi mingine kisha tunagawana faida.

Je, pesa anayokusanya anaiwekeza kwenye miradi inayohusiana na kuku au hakuna biashara yoyote ya Kuku na anafanya PONZI SCHEME?

Huyu bwana hayuko Ulaya, yuko Kigamboni na ana ofisi plus mashamba ya kuku, YENYE KUKU. Kabla hujaharibu biashara na miradi ya watu mtandaoni uende kwaza ukajiridhishe. GNLD na FOREVER LIVING nao walitukanwa sana kwamba wanafanya utapeli lakini mpaka leo wapo wanapiga mzigo.



Sent using Jamii Forums mobile app
Habari za leo
 
Back
Top Bottom