Fahamu Mgogoro wa Taliban na Afghanistan

Hizi ni hadithi tu za uongo...Marekani wanajiona smart sana kwa sababu watu wengi wameacha ku-reason.
1: kulipua marekani si kazi rahisi na je hilo kombola Osama alikuwa nalo moja tu..mbona hajalipua sehem nyingine?
2: marekan alitoa mafunzo ya kijeshi na kulipa mishahara, yeye alipata nini?..There is no free lunch.
3: kakaa miaka 20 alaf anaondoka, kaiachaje kiuchumi au atawasingizia taleban
#chanjo kama haitibu, yanini sasa
 
Shukrani kwa majibu mazuri JF inaitaji watu kama wewe, kaswali kangu ka mwisho, nini mtazamo wako juu ya bakwata unazani inalinda na kutetea uisilamu na waisilamu kama inavyotakiwa?
Sipendi kugeneralise wapo pia wachamungu Bakwata, ila wengi wachumia Tumbo. Misaada na Miradi yote ya waisilamu wanapewa wao, Wana shule za kutosha na Miradi kibao ila usimamizi mbovu. Ni type ya watu ambao wapo tayari kuvunja Darasa watoe frame za maduka.
 
Hizi ni hadithi tu za uongo...Marekani wanajiona smart sana kwa sababu watu wengi wameacha ku-reason.
1: kulipua marekani si kazi rahisi na je hilo kombola Osama alikuwa nalo moja tu..mbona hajalipua sehem nyingine?
2: marekan alitoa mafunzo ya kijeshi na kulipa mishahara, yeye alipata nini?..There is no free lunch.
3: kakaa miaka 20 alaf anaondoka, kaiachaje kiuchumi au atawasingizia taleban
#chanjo kama haitibu, yanini sasa
Kipindi marekani mwanzoni mwa miaka ya 2000 anatafuta ushawishi wa kuvamia Afghanistan na Iraq, Ulaya ikawa mabomu yanalipuka tu, kama Bomu la Hispania la treni na kuua watu kibao.

Baada ya Kupata ushawishi na Nato kumuunga Mkono eti na mabomu yakaacha kulipuka.
 
Sipendi kugeneralise wapo pia wachamungu Bakwata, ila wengi wachumia Tumbo. Misaada na Miradi yote ya waisilamu wanapewa wao, Wana shule za kutosha na Miradi kibao ila usimamizi mbovu. Ni type ya watu ambao wapo tayari kuvunja Darasa watoe frame za maduka.

type ya watu ambao wapo tyr kuvunja darasa watoe frame za maduka
 
Upo sawa mkuu big up umetoa mguu mmoja hadi mwingine kwa usahihi kabisa maana mimi huwa nawafatilia hawa wahuni toka kitambo mno...
 
Fahamu kundi la Taliban nchini Afghanistan , Mapambano yao dhidi ya Serikali ya Afghanstan na sababu Marekani kupeleka na kutoa Majeshi yake nchini humo.

Abdul Nondo,

Watu wengi wanapata kujiuliza kuhusu hawa Taliban,ni watu gani ,ni kundi gani,waliibuka vipi ,kwanini wanapigana ,wanataka nini na kwanini Marekani ilipeleka majeshi Afghanistan kwa miaka 20 yakawa huko ,kwanini tena Marekani ameyaondoa majeshi hayo sasa,tuwe wote kwa makini kupata kujua.

Nitajiaribu kugusia kila kilicho cha msingi ili ambao tulikuwa hatuelewi jambo hili tupate kulielewa hata kidogo.

Afghanistan ni nchi ambayo imepitia katika mikono ya viongozi wengi na kupitia mikiki mikiki,mapigano,mauaji na mapinduzi ya viongozi. Hii ni orodha ya viongozi wao kadhaa waliotawala hadi Taliban kuchukua madaraka ya kuongoza Serikali 1996.

Ammanullah kiongozi wa Afghanistan alitawala 1923, Mohammed Zahir Shah 1933, Mohammed Doud Khan 1973-1978,Nur Mohammed Tariki (1978-179),Hafizillah Amin Sept.1979-Dec 1979,Babraki Karmal 1979-1986, Muhammed Najibullah 1987-1992, Abdul rahim Hatif Aprili 16, 1992-April 28,1992, Sibghatullah Mojadded April 28, 1992- Juni 28 ,1992 na Burhanuddin Rabbani 28,Juni ,1992- hadi kuondolewa na kundi la Taliban mwaka 1996.

Ukitizama hapo kuna marais na viongozi wametawala kwa muda mfupi sana , ni kiashiria kwamba Afghanistan ilikuwa katika vita na mapigano ya mara kwa mara . Kuanzia miaka ya 1973 hadi miaka ya 1980 kulikuwa na vita ndani ya Afghanstan iliyochochewa pia na vita baridi kati ya Communist ,Mrusi na Mmarekani . Serikali nyingi za Afghanistan kuanzia miaka ya 1970's hadi 1996 ilikuwa ikiungwa mkono na Soviet (Urusi ) ,huku kukiwa na makundi sio chini 40 ya wapiganaji wa kiislamu chini ya mwamvuli wa jina "Mujahedeen" ambayo yalikuwa yakiungwa mkono na Marekani /CIA,Saudi Arabia , Pakistan na Osama Bin Laden kupambana dhidi ya wanajeshi wa Mrusi (Soviet) pia dhidi ya serikali iliyo madarakani iliyopewa msaada na Mrusi.

Katika hilo kundi la Mujahedeen mmoja wa kiongozi aliyepigana dhidi ya Soviet (Urusi ) alikuwa ni Muhammed Mullah Omary rafiki mkubwa wa Osama Bin Laden na alikuwa kiongozi na muasisi wa kundi la Taliban.(Taliban ikiwa na maana wanafunzi wa Madrasa).

Mwaka 1989 ,Mikhail Gorbachev Rais wa Urusi akasaini kuondoa wanajeshi wake Afghanistan kuanzia 1990.Hivyo serikali ya Afghanstan ikabaki bila msaada wa Mrusi . Kipindi hicho cha 1989 serikali ya Afghanstan ilikuwa chini ya
Muhammed Najibullah 1987-1992, Abdul rahim Hatif Aprili 16, 1992-April 28,1992, Sibghatullah Mojadded April 28, 1992- Juni 28 ,1992 na Burhanuddin Rabbani 28,Juni ,1992 hadi alipoondolewa na Taliban 1996.

Baada ya Urusi kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan vita ikawa wao kwa wao sasa ,makundi ya Mujahedeen yakaanza kupigana wao kwa wao ,huduma za msingi zikawa hakuna ,watu wanakufa , maendeleo hakuna ,shida juu ya shida.Mullah Muhamed Omary ambaye ndiye muasisi wa kundi la Taliban ,Taliban ikiwa na maana wanafunzi wa madrasa chini ya Mullah Muhammed Omary na wanafunzi wake (Taliban) walianza kujipanga ili kuiondoa serikali iliyokuwa madarakani kwa lengo la kutambulisha utawala mpya utakaofuata sheria za dini ya kiislamu na utakao kuwa na utawala wa kiislamu.

Kiongozi wa Kundi la Taliban ,Mullah Muhamed Omary akipewa msaada na rafiki yake Osama Bin Laden , Serikali ya Pakistan na Saudi Arabia alianza kuvamia mji wa kwanza wa Kandahari mwaka 1994 akiwa na wanafunzi wake wapiganaji (Taliban ) 50 tuu, baadaye wanafunzi /wapiganaji waliongezeka zaidi kufikia 15,000 wakiamini Muhammed Mullah Omary ndiye mkombozi wa kuleta utawala wa amani na haki nchini Afghanistan.

Kufikia Septemba 1996 ,Kundi la Taliban chini ya Muhammed Mullah likawa tayari limeshika asilimia 90 ya nchi nzima pamoja na mji mkuu wa Afghanistan , Kabul .

Hatimaye Taliban chini ya Mullah Muhammed Omary ikaunda serikali yenye kufuata sheria za kiislamu. Rais wa nchi hiyo Burhanuddin Rabbani akakimbia nchi 1996.

Mullah Muhammed Omary kiongozi wa kundi /Serikali ya Taliban nchini Afghanistan akamkaribisha Osama Bin Laden kiongozi wa kundi la AlQaeda kukaa Afghanistan, hivyo makao makuu ya Alqaeda yakaw Afghanistan . Serikali ya Taliban nchini Afghanistan ilikuwa ina tambuliwa kama serikali halali na nchi tatu tuu , Pakistan, United Arab of Emirates na Saudi Arabia tuu nchi zingine hazikuwahi itambua serikali ya Taliban nchini Afghanistan kama ni serikali halali.

Ndio maana ukisoma mlolongo wa utawala nchini Afghanistan hukuti sehemu yeyote wametaja utawala wa Taliban bali utakuta wametaja utawala wa Burhanuddin Rabbani kuanzia 28-Juni 1992 hadi 2001 mbali na kwamba 1996 Rabbani alikimbia nchi, na kiongozi aliyefuata wanataja alifuata Hamid Karzai 2001 kabla ya Ashraf Ghani 2014 Septemba huyu aliyekimbia nchi juzi .Hivyo utawala wa Taliban nchini Afghanistan ulitambuliwa na nchi tatu tuu.

Ilipofika Septemba 11 ,Osama Bin Laden akaishambulia Marekani (September Eleven Attack katika jengo la World Trade Center) watu zaidi ya 3000 walifariki.

Rais wa Marekani wakati huo George W. Bush, NATO na marafiki wenza wakawaambia Afghanistan chini ya Taliban wamkabidhi Osama Bin Laden kwao ila Afghanistan chini ya Taliban wakagoma na kukataa katakata.

Marekani kwa kushirikiana na NATO na nchi zingine washirika kama Ufaransa wakaamua kuchukua maamuzi ya kuvamia Afghanistan na wakang'oa utawala wa Taliban nchini Afghanistan mwaka 2001,wakisema utawala wa Taliban ulikuwa una saidia na kuficha makundi ya Kigaidi kama Alqaeda chini ya Osama Bin Laden, AlQaeda na Taliban wakakimbilia Pakistan.

Marekani wakanui kuingiza majeshi yao (Deployment) katika nchi ya Afghanstan baada tuu ya kuondoa utawala wa Taliban ,kwa sababu za maslahi ya taifa lao (National interests ) ,kwa kutekeleza malengo makuu matatu.

1.Kukaa Afghanistan ili kusambaratisha kabisa kundi la AlQaeda .

2.Kukaa Afghanistan ili kuhakikisha kwamba ardhi ya nchi ya Afghanstan haitatumiwa tena kama sehemu ya kusaidia, kuficha na kutoa mafunzo kwa makundi ya Kigaida dhidi ya nchi Marekani.

3.Kukaa Afghanistan hadi watakapompata Osama Bin Laden.

Serikali ya muda /mpito(Interim Government ) ikawekwa ndani ya Afghanstan , Hamid Karzai akawa Rais wa Afghanistan kuanzia 2001 hadi 2014, kukawa na mfumo wa chaguzi na Demokrasia.

Majeshi ya Marekani yakiwa nchini Afghanistan wakiendelea kutekeleza missions na malengo yao makuu matatu , huku wakitoa mafunzo ya kijeshi kwa wanajeshi wa Afghanistan, wakilinda Amani ndani ya Afghanstan na kupigana vita dhidi ya makundi ya kiasi kama Taliban, huku Serikali ya Marekani ikiendelea kulipa mishahara wanajeshi wa Afghanistan, kuwapa silaha na vyenzo vyote vya kijeshi walivyohitaji kupata.

Malengo makuu ya Marekani iliyowafanya wao wapeleke majeshi Afghanistan karibu malengo yote yalitekelezwa.

1.Walifanikiwa kumuua Kiongozi wa kundi la Aqaeda Osama Bin .Mei 2 ,2011.

2.Walifanikiwa kusambaratisha kundi la AlQaeda.

3.Suala la Afghanistan kutotumiwa kama ardhi ya kuficha , kusaidia na kufunza Magaidi dhidi ya Marekani hasa AlQaeda ,hili suala utekelezaji wake ni kuhakikisha ya kwamba Afghanistan inakuwa nchi ya Amani, serikali ya Afghanstan ijadiliane na kundi la Taliban kuongoza nchi yao ya Afghanstan pamoja,ndiyo wanaweza kwa pamoja kuzuia nchi yao ya Afghanstan isiwe ardhi ya kuficha,kufunza na kusaidia makundi ya Kigaida yenye shabaha ya kuishambulia Marekani.

Malengo makuu ya Marekani kupeleka Majeshi Afghanstan takribani yote yalitimia , jambo liliobaki ni kuandaa mpango na makubaliano ya kuondoa majeshi yao kutoka Afghanistan baada ya miaka mingi majeshi yao kuwepo Afghanistan.

Mpango wa kuyaondoa Majeshi ya Marekani nchini Afghanstan alianza nao Barack Obama , yeye alinuia kufikia mwisho mwaka 2014 atatoa Majeshi ya Marekani nchini Afghanstan. Msisitizo mkubwa uliokuwa unawekwa na Marekani ni makundi ya kisiasa nchini Afghanstan yakae pamoja na kukubaliana pamoja wawe wamoja kwa maendeleo ya nchi yao.

Obama alikuwa akimsisitiza sana Hamid Karzai kukaa meza moja na kundi la Taliban ili nchi iwe na amani.Bahati mbaya hadi Obama anamaliza utawala wake hakufanikiwa kuondoa majeshi ya Marekani Afghanstan.

Katika utawala wa Rais Trump. Kuanzia mwaka 2018 Rais Trump alianza kuonesha nia ya kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Afghanstan , Afghanstan ikiwa chini ya Rais Ashrafi Ghani aliyeingia madarakani Septemba 2014 baada ya Hamid Karzai , kulianza kufanyika jitahida za mazungumzo kati ya Serikali ya Marekani chini ya Trump na kundi la Taliban ili kutafuta suluhu ya amani na Marekani iondoe majeshi yake nchini Afghanistan.Kwani taarifa zinasema tangu 2007 , takribani wanajeshi 6000 wa Marekani wamefariki , NATO wanajeshi 1100 wamefariki , Wanajeshi wa Afghanistan 73000 wamefariki, Taliban wanajeshi wamefariki . Huku Jeshi la Taliban likiendelea kupanuka ikikadiriwa kuwa na wapiganaji kati ya 60000 hadi 100,000.

Katika mchakato wa kuhakikisha Marekani inatoa majeshi yake Afghanistan na kuhakikisha Afghanistan inabaki na Amani . Tar 29 , Februari 2020 Serikali ya Marekani chini ya Donald Trump na kundi la Talibani wawakilishi wa pande zote walikutana Qatar -Doha na kuingia Makubaliano yaliyoitwa,

"Agreement for Bringing Peace to Afghanistan
between the Islamic Emirate of Afghanistan which is not recognized by the United States
as a state and is known as the Taliban and the United States of America."

Makubaliano haya yalijumuisha vifungu vifuatavyo.

1.Marekani kuondoa majeshi yake Afghanstan, miezi 14 ,baada ya Februari 2020 yaani kufikia Mei 1 2021.

2 .Kuwe na Mazungumzo ya amani kati ya Kundi la Taliban na serikali ya Afghanstan ili kuunda serikali ya pamoja (To enter into power sharing negotiations with Afghanstan Government) , pamoja na kusitisha mapigano.

3.Taliban pamoja na serikali ya Afghanstan kwa pamoja wazuie na wasiruhusu kundi lolote la Kigaidi kujificha ,kukaa na kupata mafunzo nchini Afghanistan dhidi ya Marekani au nchi yeyote.

Bahati mbaya hadi Rais Trump anaondoka madarakani hakufanikiwa kuondoa majeshi yote ya Marekani nchini Afghanstan. Ila alikuwa tayari ameanza kupunguza majeshi kutoka Afghanistan kutoka idadi ya wanajeshi 15,500 hadi 2500 .

Baada ya Rais Joe Biden kuingia madarakani , hili jambo la majeshi ya Marekani nchini Afghanstan lilikuwa na sura mbili , moja ilikuwa ni ahadi yake katika kampeni kwamba ataondoa majeshi yote ya Marekani kutoka Afghanstan lakini mbili alikuta kuna makubaliano tayari yaliyowekwa na Serikali ya Marekani chini ya Rais Donald Trump na Kundi la Taliban mnamo Februari 2020 ya kuondoa majeshi ya Marekani nchini Afghanstan kuanzia Mei 1 ,2021 .

Huku wanamgambo wa Taliban wakimkumbusha Rais Joe Biden juu ya makubaliano kati yao na Marekani ya kuondoa majeshi Mei 1 ,2021 kwamba asivunje Mkataba kabisa .

Rais Biden hakuwa na namna zaidi ya kuangalia namna ya kutekeleza makubaliano hayo , ila aliwaomba Taliban wakutane , Februari 2021 ili kujadili na kupitia tena hayo makubaliano ya Februari 2020 chini ya Trump.

Februari 2021 ,katika Mji wa Doha , Qatar. Kundi la Taliban likiwakilishwa (Mkuu wa Kamisheni ya siasa ) ,Abdul Ghan Baradar huku Marekani ikiwakilishwa na Mwanadiplomasia wa Marekani Zalmay Khalilzad , jambo kubwa lililojadiliwa ni kuongeza muda wa kuondoka Afghanstan ambapo ilikubaliwa kwamba Serikali ya Marekani chini ya Rais Biden itaondoa Majeshi yake Tar 11 Septemba 2021 badala ya Mei 1 ,2021 iliyoekwa na Trump ila Biden alipaswa kutoa Majeshi yote siku Septemba 11 (Siku ya kuenzi waliokufa katika shambulio la Septemba 11 ,2001).

Ila bila kutarajia Rais Biden aliamua kuondoa Majeshi yote ya Marekani kutoka Afghanstan Aprili 2021 ,huku kundi la Taliban likipata Mwanya wa kujipanua zaidi kuelekea mji mkuu wa Kabul na miji mingine . Hadi sasa haijulikani Rais wa nchi hiyo Ashraf Ghani aliyetorika tar 15 Agost 2021, ameenda nchi gani au mji gani aliandika kabla ya kutoroka kupitia mtandao wake wa Facebook kwamba "Nachukua maamuzi magumu ya kuondoka kupisha wanamgambo wa Taliban ambao wanataka urais , maamuzi haya yana lengo la kulinda wananchi wangu kuliko kulinda cheo changu, najua kama ningelibaki wananchi wengi wazalendo wangekufa na mji wa Kabuli ungeharibiwa sana " .Mbali na maneno haya mazito ya Rais Ashrafi Ghani bado wachambuzi wa mambo na wananchi baadhi wanamuona kama ni muoga .

Rais wa Marekani baada ya tukio hili aliidhinisha kundi la wanajeshi 6000 kwenda kusaidia kuwaondoa Rai wa Marekani, mafisa wake na wananchi wa Afghanistan ambao walijitoa miaka 20 kufanya kazi na mafisa wa Marekani kwa lengo la kuwapa VISA kuishi Marekani.Taliban walionywa katika hatua hii ya Marekani kuondoa watu wake Talib isihatarishe maisha ya Raia wa Marekani hata mmoja ,ikifanya hivyo Marekani itajibu.

Watu wengi wanatokea kumlaumu Joe Biden kwa maamuzi ya kuondoa Majeshi Afghanstan kwa uharaka , Joe Biden amejibu kwa kusema hajutii maamuzi yake kwani hakuna maslahi yeyote kwa nchi ya Marekani kwa kuendelea kuyaweka majeshi yake nchini Afghanistan ."Staying in Afghanistan is not national interest"

Akisema malengo yote ya kuweka Majeshi ya Marekani Afghanstan tayari yametimia kumuuwa Osama , kusambaratisha AlQaeda na kuhakikisha Afghanistan haitumiki kama ngome ya magaidi dhidi ya Marekani .

Rais Biden aliendelea kusema kwamba ameingia ofisini akakuta tayari kuna makubaliano yaliyowekwa kati ya Trump na Taliban tangu Februari 2020 kwamba hadi mwezi Mei 2021 Majeshi yote ya Marekani yatapaswa kuondoka ."I inherited a deal that Trump negotiated with Taliban under his agreement would be out May 1,2021.

Hakukuwa na namna ya kuacha majeshi sababu hakukuwa na makubaliano ya amani na kulinda watu wetu ikiwa majeshi hayataondoka baada ya Mei 2021 ambaye yeye aliomba iwe Septemba 2021.(He said ,No agreement to protect our forces and people after Mei 1 ,2021) "No status if Stability after May one "

Watu wanamlaumu kwamba anaiacha Afghanistan katika machafuko na watu kuendelea kufa , Rais Biden anasema Mission ya Marekani nchini Afghanstan haikuwa kujenga Taifa au kuimarisha Demokrasia bali mission ilikuwa kuzuia ugaidi dhidi ya Nchi ya Marekani. (Mission is not National building , not creating unified , centralized Democracy but to prevent a terrorist attack on American Homeland .

Rais Biden ,anaendelea kusema hakuna muda rasmi au muda mzuri wa kuondoa majeshi zaidi ya viongozi wa Serikali ya Afghanstan na Taliban kutafuta suluhu za kisiasa jambo ambalo alimshauru Rais Ashrafi Ghani walipozungumza Juni 2021 ,ila Ghani alionesha kutaka kutumia nguvu na kuinua silaha badala ya suluhu ya amani na mazungumzo.

Anasema ,"Majeshi ya Marekani hayawezi na hayapaswi kuendelea kupigana katika vita na kufa katika vita ikiwa majeshi ya Afghanstan hayapo tayari kujipigania wao wenyewe"

"American troops cannot and should not be fighting in a war and dying in a war that Afghanistan forces are not willing to fight for themselves".

Joe Biden akiendelea kusema , Marekani itaendelea kulinda sera yake ya mambo ya nje (Foreign Policy) kuheshimu haki za binadamu , kuzuia vita na mapigano kama ambavyo mara zote wanafanya Dunia nzima ila sio kwa kuendekelea kuweka Majeshi nchini Afghanistan (Not through endless military deployment).

Huku upande wa Taliban wanaendelea kutangaza kwamba nchi itakuwa ya amani , ila wananchi wanaonekana kuwa na hofu kuwa chini ya utawala wa Taliban , wakikumbuka mateso waliyopitia 1996 hadi 2001 chini ya utawala wao , utawala wa nguvu na kutumia sheria kali . Kupiga mawe wazinifu hadi kufa, kutoruhusu mziki wala kuangalia Tv , kulazimisha kuvaa hijabu kufunika nyuso kwa wanawake .

Lengo kubwa la Taliban ni kusimamisha utawala wa kiislamu na utakaofuata sheria za kiislamu.

Kiongozi na muasisi wa kundi la Taliban aliitwa Mullah Mohammed Omary ,ambaye ndiye alikuwa kiongozi mkubwa yaani Amir -Ali-Muuminin mkuu wa Rahbar Shura (Mkuu wa Baraza linalofanya maamuzi yote juu ya siasa na Jeshi ).Mullah Muhammed Omary alifariki nchini Pakistan hospital ya Karachi mwaka 2013 kwa ugonjwa wa TB lakini kifo chake kilitangazwa na Taliban mwaka 2015.

Kiongozi Mkubwa aliyefuata baada ya Mullah Muhamed Omary ni Mullah Akhtar Mohammed Mansour ambaye aliuwawa 2016 na Marekani nchini Pakistan.

Kiongozi wa sasa wa kundi la Taliban ni Mawlawi Haibutullah Akhundzada. Akisaidiwa na viongozi wengine Mullah Muhammed Yakoub , Mullah Abdallah Ghan Baradar , Sirijuddin Haqqan pia wana idara mbalimbali (Commission) zikisimama kama wizara kwa lugha ya kawaida.

Imeandaliwa kwa kukusanya taarifa mbalimbali kutoka katika vyanzo vya magazeti Washington Posts, Vyombo vya habari CNN, ALJAZEERA,BBC na vyombo vingine lakini vitabu mbalimbali juu ya Mapigano ya Taliban na Afghanistan.

Ahsante.

Imeandaliwa na,

Abdul Omary Nondo.
Thanks alot umechambua vizur sana makala hii... uwe na moyo huohuo wa kutujuza vitu
 
Hakuna malengo yaliyofikiwa.ni sawa na kwenda kumkamata mfuta bangi alafu muuzaji anaendelea kubaki.kwa akili ya kawaida tu ni lazima wavutaji wengine watapatikana maana muuzaji bado yupo
 
Kipindi marekani mwanzoni mwa miaka ya 2000 anatafuta ushawishi wa kuvamia Afghanistan na Iraq, Ulaya ikawa mabomu yanalipuka tu, kama Bomu la Hispania la treni na kuua watu kibao.

Baada ya Kupata ushawishi na Nato kumuunga Mkono eti na mabomu yakaacha kulipuka.
Wale wahuni tu, sa hv wanafanya majaribio ya chanjo kupitia sisi..ikibuma wanakuja na excuse
 
42 Reactions
Reply
Back
Top Bottom