Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kufuatia amri za Wakuu wa mikoa na wilaya mbalimbali nchini ya kuwasweka rumande watumishi wa umma, nimeona ni vyema na haki, kama Msomi wa sheria na mtanzania wa kawaida mwenye haki ya kikatiba ya kutoa na kupata habari, niandike kwa kifupi kuhusu jambo hilo. Nitaandika kwa kifupi tu na moja kwa moja kwenye hoja husika.
Nasema kabisa mwanzoni kuwa sitatamka wala kuonyesha kama Wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya haki au la. Baada ya kusoma na kukosoa andiko langu hili, utakuwa kwenye nafasi ya kuona uhalali au ubatili wa matumizi ya mamlaka hiyo kwa wahusika.
Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuagiza kukamatwa kwa mtu na kuwekwa rumande yako chini ya vifungu vya 7 (mamlaka ya mkuu wa mkoa) na 15 (mamlaka ya mkuu wa wilaya) vya Sheria ya Tawala za Mikoa, 1997. Vifungu hivyo vinafanana katika uandishi na hata mantiki isipokuwa tu maneno 'Mkuu wa Mkoa' na 'Mkuu wa Wilaya'.
Katika mtazamo huo wa kufanana kwa vifungu hivyo, nitavizungumzia kwa pamoja. Mkuu wa Mkoa/Wilaya aweza kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote ambaye mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa au Wilaya anatenda kosa au alitenda kosa ambalo linamfanya mtu huyo kuweza kukamatwa na kushtakiwa. Kiufupi, linapaswa kuwa kosa la jinai.
Pia, kama Mkuu wa Mkoa au Wilaya ana sababu za kuamini kuwa mtu yeyote aweza kuvunja amani au kuharibu utulivu uliopo au kufanya kitendo chochote ambacho kinaweza kuvunja amani au kuharibu utulivu na uvunjifu huo hauwezi kuzuiwa kwa njia yoyote nyingine isipokuwa kumsweka rumande mtu huyo, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aweza kuagiza kwa maneno au maandishi kukamatwa kwa mtu huyo.
Mtu aliyekamatwa kwa amri au maelekezo ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai. Endapo hatafikishwa Mahakamani kwa muda unaopaswa, na muda kuisha, anapaswa kuachiwa na hapaswi kukamatwa tena kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya kwa namna ile ile.
Wakati wa kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote au muda mfupi baada ya kuagiza, Mkuu wa Mkoa au Wilaya lazima aandike sababu za kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu husika na kupeleka nakala kwa Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa.
Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa, aweza kumwachia huru aliyekamatwa, kumpa dhamana au kutoa agizo la kuachiwa aliyekamatwa. Yeyote (Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya au Afisa wa Polisi) ambaye ataagizwa na Mahakama kumwachia aliyekamatwa na hatatii agizo hilo atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama chini ya kifungu 114 cha Kanuni ya Adhabu.
Mkuu wa Mkoa au Wilaya yeyote au mtu yeyote ambaye atamplekea Mkuu wa Mkoa au Wilaya kutumia vibaya mamlaka yake chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa (vifungu husika vya kukamatwa mtu) atatenda kosa la jinai na anaweza kushtakiwa chini ya kifungu cha 96 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mamlaka, matakwa na mipaka ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote. Kila mmoja awe kwenye nafasi za kuoanisha na kinachotokea na aone uhalali au ubatili wa mambo hayo.