Fahamu mamlaka, matakwa na mipaka ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusweka watu rumande

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,188
25,493
Kufuatia amri za Wakuu wa mikoa na wilaya mbalimbali nchini ya kuwasweka rumande watumishi wa umma, nimeona ni vyema na haki, kama Msomi wa sheria na mtanzania wa kawaida mwenye haki ya kikatiba ya kutoa na kupata habari, niandike kwa kifupi kuhusu jambo hilo. Nitaandika kwa kifupi tu na moja kwa moja kwenye hoja husika.

Nasema kabisa mwanzoni kuwa sitatamka wala kuonyesha kama Wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya haki au la. Baada ya kusoma na kukosoa andiko langu hili, utakuwa kwenye nafasi ya kuona uhalali au ubatili wa matumizi ya mamlaka hiyo kwa wahusika.

Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuagiza kukamatwa kwa mtu na kuwekwa rumande yako chini ya vifungu vya 7 (mamlaka ya mkuu wa mkoa) na 15 (mamlaka ya mkuu wa wilaya) vya Sheria ya Tawala za Mikoa, 1997. Vifungu hivyo vinafanana katika uandishi na hata mantiki isipokuwa tu maneno 'Mkuu wa Mkoa' na 'Mkuu wa Wilaya'.

Katika mtazamo huo wa kufanana kwa vifungu hivyo, nitavizungumzia kwa pamoja. Mkuu wa Mkoa/Wilaya aweza kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote ambaye mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa au Wilaya anatenda kosa au alitenda kosa ambalo linamfanya mtu huyo kuweza kukamatwa na kushtakiwa. Kiufupi, linapaswa kuwa kosa la jinai.

Pia, kama Mkuu wa Mkoa au Wilaya ana sababu za kuamini kuwa mtu yeyote aweza kuvunja amani au kuharibu utulivu uliopo au kufanya kitendo chochote ambacho kinaweza kuvunja amani au kuharibu utulivu na uvunjifu huo hauwezi kuzuiwa kwa njia yoyote nyingine isipokuwa kumsweka rumande mtu huyo, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aweza kuagiza kwa maneno au maandishi kukamatwa kwa mtu huyo.

Mtu aliyekamatwa kwa amri au maelekezo ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai. Endapo hatafikishwa Mahakamani kwa muda unaopaswa, na muda kuisha, anapaswa kuachiwa na hapaswi kukamatwa tena kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya kwa namna ile ile.

Wakati wa kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote au muda mfupi baada ya kuagiza, Mkuu wa Mkoa au Wilaya lazima aandike sababu za kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu husika na kupeleka nakala kwa Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa.

Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa, aweza kumwachia huru aliyekamatwa, kumpa dhamana au kutoa agizo la kuachiwa aliyekamatwa. Yeyote (Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya au Afisa wa Polisi) ambaye ataagizwa na Mahakama kumwachia aliyekamatwa na hatatii agizo hilo atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama chini ya kifungu 114 cha Kanuni ya Adhabu.

Mkuu wa Mkoa au Wilaya yeyote au mtu yeyote ambaye atamplekea Mkuu wa Mkoa au Wilaya kutumia vibaya mamlaka yake chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa (vifungu husika vya kukamatwa mtu) atatenda kosa la jinai na anaweza kushtakiwa chini ya kifungu cha 96 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania.

Kwa kifupi, hayo ndiyo mamlaka, matakwa na mipaka ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote. Kila mmoja awe kwenye nafasi za kuoanisha na kinachotokea na aone uhalali au ubatili wa mambo hayo.
 
Mpaka sasa kinachofanyika ni JINAI za wakuu wa Mkoa na Wilaya ili kumpendeza boss awaone wanafanya kazi.Ila ninachokiona ni kwamba watanzania ni waoga mno kudai haki zao za msingi.

Watanzania tunawaogopa mno watawala ambao bila kura yetu hawawezi katu kuwa watawala
 
japo sikumbuki sawasawa ni kifungu kipi,lakini lazima anayekamatwa awe anahatarisha amani katika eneo husika,naona hapo umeelezea procedures tu,lakini vigezo vinavyofanya amri itoke hukuvitaja,
 
Naona watu wengi ambao "Mungu wa Dsm"alikuwa anawasweka ndani hapa majuzi kwenye ziara yake makosa yao yalikuwa hayaeleweki na mengine yalikuwa ni makosa ya ki Madai zaidi na sio jinai.
 
japo sikumbuki sawasawa ni kifungu kipi,lakini lazima anayekamatwa awe anahatarisha amani katika eneo husika,naona hapo umeelezea procedures tu,lakini vigezo vinavyofanya amri itoke hukuvitaja,
Mkuu,soma tena aya ya nne na ya tano ya hilo bandiko langu.
 
Watanzania kuongea na kufata mkumbo hamjambo, hivi kama si Makonda haya ungeyaandika lini na ulikuwa wapi kuyaweka hapa? Mnasubiri tukio likitokea kila mtu anaanza kuongea ...matukio tu, nchi ya matukio
 
Petro, je, sheria inamruhusu mtu aliyewekwa ndani kwa amri ya hao walevi wa madaraka kuwashitaki akishatoka endapo atakuwa alikamatwa pasipo kutenda kosa la jinai?
Yaani, are there any grounds to sue them for unlawful imprisonment?
 
Maximum ya siku za kukaa Cello ni ngapi kulingana na mamlaka yao? Make naona hiyo masaa 48 ni kupelekwa Mahakamani au kuachiwa!!
 
Watanzania kuongea na kufata mkumbo hamjambo, hivi kama si Makonda haya ungeyaandika lini na ulikuwa wapi kuyaweka hapa? Mnasubiri tukio likitokea kila mtu anaanza kuongea ...matukio tu, nchi ya matukio
Na wewe unafuata mkumbo, haya yasingeandikwa leo ungecomment?
 
Watanzania kuongea na kufata mkumbo hamjambo, hivi kama si Makonda haya ungeyaandika lini na ulikuwa wapi kuyaweka hapa? Mnasubiri tukio likitokea kila mtu anaanza kuongea ...matukio tu, nchi ya matukio
Bila matukio huwezi ishi ACHA umbulula wewe
 
Petro, je, sheria inamruhusu mtu aliyewekwa ndani kwa amri ya hao walevi wa madaraka kuwashitaki akishatoka endapo atakuwa alikamatwa pasipo kutenda kosa la jinai?
Yaani, are there any grounds to sue them for unlawful imprisonment?
Hilo liko wazi. Na hata jinai kwa mkuu husika kama nilivyogusia hapo
 
Watanzania kuongea na kufata mkumbo hamjambo, hivi kama si Makonda haya ungeyaandika lini na ulikuwa wapi kuyaweka hapa? Mnasubiri tukio likitokea kila mtu anaanza kuongea ...matukio tu, nchi ya matukio
Kwani Makonda ni wa kwanza kutenda hivyo? Toa hoja mkuu
 
Watanzania kuongea na kufata mkumbo hamjambo, hivi kama si Makonda haya ungeyaandika lini na ulikuwa wapi kuyaweka hapa? Mnasubiri tukio likitokea kila mtu anaanza kuongea ...matukio tu, nchi ya matukio
ulitakaje sasa?
 
Mimi naomba mtoa mada utusaidie hili;Iwapo mkuu wa mkoa/wilaya amemsweka ndani mtumishi wa umma kimakosa je ni hatua gani mtumishi wa umma anatakiwa kuchukua dhidi ya mkuu wa mkoa/wilaya je ni fidia anastahili kulipwa au mkuu wa mkoa/wilaya atapatwa na adhabu gani?
 
Kuna mambo mawili ya kijinai na ya kimadai. Kuhusu jinai,kama itabainika kuwa Mkuu wa Mkoa au Wilaya ameyatumia madaraka yake vibaya aweza kushtakiwa kama nilivyoeleza kwenye bandiko langu. Pia,kama aliyekamatwa atamshtaki Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyeagiza kukamatwa kwake isivyo halali na kuthibitisha hivyo mahakamani,fidia yaweza kutolewa. Hilo litakuwa ni shauri la madai.
 
Nchi nyingi zilizofuata siasa ya kikomunisti ni ngumu sana kwa system zilivyowekwa za kudai haki.toka ktk tawala kwa mtumishi.

Angalia China,Urusi,North Korea,Cuba,iliyokuwa Yugoslavia.

Pamoja na makosa ya kuwekwa ndani kwa baadhi ya watumishi lakini si rahisi kuwaona wakienda kudai haki zao wakiwa ndani ya utumishi
 
Yawezekana mkuu
 
Back
Top Bottom