Fahamu mambo kumi yatakayofanya vyama vya upinzani kuanguka vibaya katika uchaguzi mkuu 2020

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Najua wengi mtanibishia lakini ukweli ni kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 upinzani wataanguka vibaya mnoo kuanzia level ya wabunge na madiwani mpka wenyeviti wa mitaa wataanguka vibaya mnooo.....

Haijalishi ni nani atakae peperusha bendera ya upinzani au mgombea uraisi atakuwa nani ila wapinzani wataumia sana kutokana na sababu zifuatazooo.....

1. Wananchi wengi wameshawastukia wapinzani tulio nao wengi wao ni waoga, walaghaiii na hawapo tayali katika kufanya siasa za kweli na mageuzi ya kwelii hivyo wananchi wanaona hawana sababu kujisumbua kwenda kuwapigia kura...

2. Wapinzani wetu wamekosa mbinu mbadalaa ya kuwadhibiti wabunge na madiwani wanaohama vyama vyao kwenda ccm hivyo kuwafanya wananchi kuvunjika moyo kwa sababu wanajua hata tukipambana kuhusu mbunge flani au diwani ashinde hata akishinda badae anajiuzulu na kuhama mwishoni wanaona bora wasige kuraa.

3. Hadi sasa hakuna mwananchi au raia anayeunga mkono upinzani ambae yupo tayali apigane kufa na kupona ili mbunge au diwani flani wa upinzani ashinde kwa sababu hata akipambana hadi kuumia mwisho wa siku atakuja kujiuzulu na kuhamia upande wa pili .

4. Mgogoro ndani ya cuf kati ya Lipumba na Seif ambapo hadi leo kesi ipo mahakamani

5.wananchi wamechoka kusikia malalamiko ya upinzani kila wakishidwa wanasingizia tume na katiba lakini cha kushangaza uchaguzi ukishapita huwasikii tena wazizungumzia kuhusu tume ya uchaguzi wala katiba itayowafanya uchaguzi mkuu 2020 waibuke na ushindi wanaodai kila siku wanaibiwa.

6.wapinzani kukubali kushiriki uchaguzi kwa tume ile ile na katiba ile ile wanayodai kila siku wanaibiwa kura .

7.viongozi wengi wa upinzani wamekuwa wababashaji lakini pia ni watu wasio aminika katika jamiii hawana msimamo
utashangaa tuu ""LEO YUPO HUKU KESHO YUPO KULE"" leo anazungumza ivi kesho anazungumza vilee halafu anakuja kuwaambia "siasa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu""

8.uwepo wa viongozi wa vyama vya upinzani kukaa muda mrefu madarakani bila kuachia ngazi kupata mawazo mapyaaa.

9.viongozi wengi wa upinzani wamekuwa ni watu wasio shaulikaaaaa

Kwa leo naishia hapa mengine yatafuatwa unaweza ukaendeleaaaa kuyasema yatayowafanya wapinzani waangukee 2020 ili kama juna viongozi wanasoma maoni haya wajirekebishee

Ni hayoo tuu kwa leo mengine kama unayo kuongeza ongeza.
 
Ukweli wenyewe ndiyo huu...........

NEC+Jeshi la Polisi=CCM

Jaribu kujiuliza swali moja tu dogo

Ni kwanini Mwenyekiti wako ana kihoro kupindukia anaposikia vyama vya upinzani??

Uthibitisho wa hili ni kuwa anaabuse power yake kwa kulitumia Jeshi la Polisi, ndivyo sivyo ili kutimiza matakwa yake ya kisiasa

Karibu kuimagine, hivi alitumia sheria ipi ndani ya nchi ambayo ilimwezeshs yeye apige marufuku vyama vya upinzani visifanye mikutano ya hadhara??

Wakati yeye na chama chake kila kukicha wanachaja mbuga nchi nzima kufanya kampeni??
 
Mbona kama sababu ni moja tu ya matumizi ya nguvu ya kijeshi na kutotumia akili
 
1. Manunuzi;
2. Kuwanyima fursa kufanya siasa huku wao wanafanya
3. Kesi za uchochezi
4. Wizi wa kura
5. Dola kuwaminyaa... Bungeni na Mtaani

Kula hizo tano kwanza zinakutosha
 
Ukweli wenyewe ndiyo huu...........

NEC+Jeshi la Polisi=CCM

Jaribu kujiuliza swali moja tu dogo

Ni kwanini Mwenyekiti wako ana kihoro kupindukia anaposikia vyama vya upinzani??

Uthibitisho wa hili ni kuwa anaabuse power yake kwa kulitumia Jeshi la Polisi, ndivyo sivyo ili kutimiza matakwa yake ya kisiasa

Karibu kuimagine, hivi alitumia sheria ipi ndani ya nchi ambayo ilimwezeshs yeye apige marufuku vyama vya upinzani visifanye mikutano ya hadhara??

Wakati yeye na chama chake kila kukicha wanachaja mbuga nchi nzima kufanya kampeni??
kulia lia hakukusaidii kitu,eti nec+polisi=ccm kama mtoto wa darasa la kwanza vile
 
Back
Top Bottom