Fahamu maisha ya Vladimir Putin wa Urusi

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
3,068
2,000

Fahamu kwa undani maisha binafsi ya kila siku ya rais wa Urusi Vradimil Putin​


Kwa kawaida hula kiwango kikubwa cha mayai ya kukaangwa kunywa uji

Kwa kawaida Putin huchelewa kuamka na kupata kifungua kinywa

Akiwa ni mmoja wa viongozi wa dunia wenye nguvu na ushawishi zaidi na mwenye ulinzi mkali, Rais wa Urusi amekuwa akiishi maisha yanayoaminiwa kuwa ya ulinzi mkali na zaidi akiepuka kuchangamana sana na watu wengine wa nje isipokuwa inapokuwa lazima. Hali hii imewafanya baadhi ya watu kujiuliza kuhusu maisha yake ya kawaida yako vipi?

Huchelewa kuamka​

Rais wa Urusi Vladimir Putin ni mtu wa kuamka kuchelewa asubuhi na hupata kifungua kinywa karibu saa sita za mchana.
Karatiba yake ya siku Putin pia husoma taarifa zinazowasilishwa kwake, zikiwemo za ujasusi

Ratiba yake ya siku Putin pia husoma taarifa zinazowasilishwa kwake, zikiwemo za ujasusi

Kwa kawaida hula kiwango kikubwa cha mayai ya kukaangwa kunywa uji ambao huandaliwa ndani ya bakuli pana pamoja na mayai ya kwale pamoja na sharubati ya matunda pembeni.
Taarifa za gazeti la Newsweek reports nchini Urusi zinaripoti kuwa viungo vya chakula chake anachokula "mara kwa mara hutoka katika mashamba ya kiongozi wa kidini wa Waothordox wa Urusi Patriarch Kirill."Na mara anapomaliza mlo wake, hunywa kikombe cha kahawa.

Putin hupenda kufanya mazoezi ya mwili katika ukumbi wa Gym

Putin hupenda kufanya mazoezi ya mwili katika ukumbi wa Gym

Kinachofuata baada ya mlo, ni muda wa mazoezi ya mwili. Gazeti la Newsweek nchini humo liliripoti kuwa Bw Putin hutumia muda wa saa mbili kuogelea. Na anapokuwa ndani ya maji hufikiria mambo mengi kuihusu nchi yake Urusi .
Baada ya kukamilisha mizunguko mingi ndani ya maji, Putin huwa haishii hapo, bali huingia katika ukumbi wa mazoezi (gym) na kuanza kunyenyua vyuma.


Muonekano na mavazi​


Putin hupendelea suti zilizoshonwa kwa mtindo wake aliouchagua mwenyewe

Putin hupendelea suti zilizoshonwa kwa mtindo wake aliouchagua mwenyewe

Bw Putin hutumia muda wa saa mbili kila siku

Bw Putin hutumia muda wa saa mbili kila siku

Rais huyu mwenye umri wa miaka 65 anasemekana kuwa makini sana kujenga muonekano wa mwili wake sawa na wanamichezo, na hivyo kuonekana kuwa na umbo la kiume ambalo wengi wamekuwa wakilitaja kuwa lenye mvuto.
Rais Putin ni mhafidhina, na ikapokuja katika chaguo lake la mavazi, hupendelea suti zilizoshonwa kwa mtindo wake aliouchagua mwenyewe, manukato pamoja na tai za nembo ya Valentino.
Mwaka 2015, alipigwa picha akifanya mazoezi na waziri Mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev. Kulingana na taarifa ya Esquire , mavazi yake ya mazoezi yalikwa na gharama ya dola 3,200.

Jumapili Putin husali na kuungama dhambi

Jumapili Putin husali na kuungama dhambi

Wavuti unaomilikiwa na taifa la Urusi - Russia Beyond the Headlines unaripoti kuwa nembo za mavazi anazopendelea Bw Putin Kiton na Brioni.
Rais huyu wa Urusi kwa kawaida huwa hafiki kazini mpaka baada ya saa sita mchana. Kwanza huketi chini kwenye dawati lake kusoma maelezo ya taarifa zilizowasilishwa kwake zikiwemo za ujasusi.
Taarifa hizi ni pamoja na za ujasusi wa ndani ya nchi na masuala ya kigeni, pamoja na kusikiliza baadhi ya sauti zilizorekodiwa kutoka kwa vyombo vya habari vya Urusi na vya kimataifa.

Mara moja moja, mshauri wake humuonesha video ya mtandaoni ya kumdhihaki yeye na serikali yake.
Rais wa Urusi ni mtu wa kufanya kazi sana usiku na mara nyingi huchelewa sana kulala akifanya kazi. Hufanya kazi zake vyema usiku, uliandika mtandao wa habari wa Urusi wa Newsweek.

Inakuaje anaposafiri nje ya nchi?​


Wakati anaposafiri nje ya nchi, ratiba ya Rais Putin ya siku huwa imesheheni mambo mengi zaidi. Kokote anakopokelewa kila kitu hubadilishwa kuanzia shuka, sabuni, vifaa vya usafi hadi mabakuli ya matunda.
Putin pia huwa hakubali chakula kilichoandaliwa na mwenyeji wake ambacho hakijaidhinishwa na Kremlin.

Putin hupenda mvinyo baada ya chakula

Putin hupenda mvinyo baada ya chakula

Awali jarida la The Telegraph liliripoti kuwa chakula anachokipenda zaidi Bw Putin ni Ice Cream aina ya pistachio . Aliwahi pia kumpatia zawadi rais wa uchina Xi Jinping aina hiyo ya ice cream wakati wa mkutano wa G20 summit wa mwaka 2017.
Miaka kadhaa iliyopita mgahawa wa St. Petersburg Podvorye ulikuwa na menyu iliyoitwa -Mlo wa mchana wa Vladimir Putin "The Lunch of Vladimir Putin" - ambao ulitengeneza chakula alichokipenda raisi huyo wa Urusi. Mara nyingi alikuwa akiagiza pale nyama inayoitwa "frying pan," yenye mchanganyiko wa vipande vya nyama vilivyokatwa katwa kwa umbo la ulimi, soseji, vipande vyembamba vya nyama isiyo na mifupa, na mikate ya kuokwa iliyochanganywa na mboga.
Mwaka 2010, mpishi wa Kremlin Anatoly Galkin alisema kuwa Bw Putin anapendelea mvinyo au bia.
Baadhi ya vyombo vya habari vinadai kuwa rais huyo huburudishwa kwa mvinyo mwekundu wa Uhispania- Spanish red wines, huku baadhi vikidai hupenda kunywa kiasi kidogo cha Vodka baada ya chakula.

Mchezo wa kuteleza kwenye barafu, ni mchezo anaoupenda na kuutengea muda

Mchezo wa kuteleza kwenye barafu, ni mchezo anaoupenda Putin na kuutengea muda

Ratiba ya kazi yake siku za wikendi huwa haina mambo mengi ya kufanya, ili kumpatia muda Bw Putin kuhudhuria mafunzo yake ya lugha ya Kiingereza. Jumapili wakati mwingine husali na kuungama.
Hatahivyo, maafisa wa Urusi ambao wako karibu na rais huyo wanasisitiza kuwa yeye sio Mkristo ," kulingana na gazeti la Newsweek.
Kila baada ya wiki chache, ratiba ya Bw Putin husititishwa ili kutoa fursa ya muda wake wa kibinafsi wa kucheza hockey, mchezo wa kuteleza kwenye barafu.

Putin akiwa na mbwa wake Buffy na Yume

Putin akiwa na mbwa wake Buffy na Yume

Rais huyo wa urusi hatazami tu mchezo, bali anacheza katika ligi, huku akizunguka zunguka dhidi ya miraba ya timu za walinzi wake.
Putin pia anawapenda wanyama. Anamiliki mbwa mweusi aina ya Labrador anayeitwa Konni, Yume wa aina ya Akita Inu , na mbwa aina ya Karakachan anayeitwa Buffy.
 

DellaPina

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
1,015
2,000
Ex.KGB anayewanyima usingizi nchi za magharibi na marekani yeye kazi yake kubadikishana na waziri mkuu wake tu madaraka mwenzake akiwa rais yeye ndiye waziri mkuu.yeye akiwa waziri mkuu medved ni rais.wanatakiwa wamuandae mtu mwenye msimamo kama wake aiendeshe urusi kwa kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom