Swahili AI
JF-Expert Member
- Mar 2, 2016
- 6,381
- 47,604
Wazee wa Pochi NENE mpo?
Wavulana wengi wana tabia ya kuweka mkoba (WALLET) yenye inchi nusu au zaidi ikitegemeana na wingi wa vitu vilivyopo kwenye mkoba huo kwenye mfuko wao wa nyuma wa nyonga ambao unaweza kuleta maumivu ya mgongo, kiuno, misuli, mifupa na mbali zaidi kuleta madhara kwenye mfumo wa neva.
Ukaliaji wa mkoba wako kwa muda mrefu unaweza kupelekea kuathiri mshipa wa Sciatic na kupelekea kupata ugonjwa wa Piriformis (Piriformis Syndrome).
Ugonjwa wa Piriformis ni hali ambayo misuli ya piriformis, iliyoko kwenye eneo la makalio, kusababisha maumivu ya misuli, kufa ganzi na kuuma nyuma ya mguu.
Nini cha kufanya kuepuka haya?
1. Kama kuna ulazima sana wa kubeba wallet yako, basi usikae ikiwa kwenye mfuko wako wa nyuma. Japo ni kama usumbufu toa weka mara kadha.
2. Scan vitambulisho vyako na hifadhi kwenye simu au mtandaoni ili iwe rahisi kuvifikia pale unapovihitaji.
3. Kwa miamala ya kifedha basi tumia mtandao kama gharama zipo ndani ya uwezo wako. KINGA NI BORA KULIKO TIBA!
HAYO NI BAADHI YA MAONI YANGU KUPUNGUZA MZIGO HUU HAPA CHINI👇👇👇👇.